Moja ya kitu ambacho hakifundishwi sana ni somo kuhusu viumbe hawa wenye nguvu, ambao Mungu aliwaumba kwa makusudi mbalimbali. Leo natamani tuangalie Malaika wanaohudumia kiti cha enzi cha Mungu, na kama itapendeza wakati mwingine tutashirikishana zaidi kile Biblia inasema kuhusu Malaika.
1. Makerubi wenye mabawa manne
Hawa wanapatikana Ezekiel 1, soma pia 10:1-20 na 48:18-19
Hawa wana mabawa manne, na sura nne, ya mfano wa Mwanadamu, Tai, Ng’ombe na Simba, pia wana magurudumu kila moja, na wanamacho kila upande kuanzia miili yao hadi gurudumu, na juu yao kuna kitu kama anga ambalo ndipo kuna kiti cha Enzi cha Mungu.
2. Maserafi
Hawa wanapatikana Isaya 6
Wao wana mabawa sita, ila mawili huyatumia kuruka, mawili hufunika nyuso zao, na mawili miguu yao, (maana utukufu wa Mungu ni kama moto ulao, hutumia mabawa hayo kujilinda na kudhurika). Hawa wako juu ya kiti cha Enzi na hawakomi kumtukuza Mungu kwa kusema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu…
3. Wenye uhai wanne
Hawa wanapatikana Ufunuo 4
Wanafanana na Makerubi wa Ezekiel 1 isipokuwa hawa wana mabawa sita na wapo katikati na pembeni mwa kiti cha Enzi, pia hutumia Mabawa yao kujilinda na utukufu wa Mungu MAANA MUNGU NI MOTO ULAO. Wengine wanaamini hawa ni Mikael, Gabriel, Raphael na Urieli.
4. Rusifa
Huyu aliumbwa akiwa mkuu na mzuri kuliko Malaika wote, kama Biblia isemavyo Ezekiel 28:13-15. Huyu alikuwa Kerubi, afunikaye, alitiwa mafuta na kupewa theruthi moja ya Malaika, na alikuwa kiongozi wa sifa na kuabudu kabla hajaasi. Baadaye aliasi kwa kuponzwa na uzuri wake na akang’olewa na kutupwa Duniani, Huyu ndiye Ibilisi, Shetani, Joka la Zamani na Mshitaki Ezekiel 28:16…. Uf 12:7-10. Alianguka na theruthi ya Malaika ambao ndio mapepo, majini nk, na hawa ndio chanzo cha matatizo yote. Asante Yesu maana kwa Damu yake ushuhuda wake na Jina lake tunawashinda hawa wote.
Hawa ni Baadhi ya Malaika na Kazi zao kama Biblia isemavyo.
5. Kuna Malaika waliokosa, na wamefungwa kwenye vifungo vya giza, hawa ni tofauti na wale theruthi moja iliyoanguka na Shetani.
Hawa wanapatikana Mwanzo 6, Yuda 1:6-7 2petro 2:4-5.
Ni vyema kujua Malaika na utendaji wao, na Biblia imewaandika sana, naamini andiko hili litakupa shauku ya kusoma na kujifunza zaidi maana ni somo pana sana. Hapa sijaongelea Malaika aliyepambana na Yakobo na hakujitambulisha jina, 32:22-28 Huyu naamini ni yuleyule aliyemtokea Manoa kumpa habari za kuzaliwa Samson, MAANA NAYE ALIGOMA KUTAJA JINA LAKE Waamuzi 13:17-18.
Kuna Malaika walihusika kupeleka habari, kupigana, kusaidia watu, kuongoza, kutoa watumishi Jela, kuua adui, wameonekana wakiwa na panga, Lakini wakati mwingine wameonekana na umbo la wanadamu, na watu wamewapokea au kuwakataa kwa kutokujua ama kujua, kumbuka wale walielekea Sodoma na Gomora walivyopokelewa na Ibrahimu na akawapikia na wakala.
Jambo zuri zaidi Mungu kampa mwanadamu heshima zaidi ya Malaika. Haleluya
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.