Chuma Hunoa Chuma

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Aina 5 Za Mitaji Wanazotumia Watu Wengi Kuanzisha Biashara:

Aina Ya Kwanza: Wazo

Aina Ya Pili: Nguvu

Aina Ya Tatu: Bidhaa

Aina Ya Nne: Uaminifu

Aina Ya Tano: Pesa

Leo katika makala hii tutaangalia aina ya kwanza ya MTAJI.

Aina Ya Kwanza: Wazo

Kuna watu ambao mtaji wao wa kwanza ilikuwa ni kuwa na wazo.

Wazo ambalo linatekelezeka na linaloweza kuaminika na watu wengine.

Watu wa aina hii walifanikiwa kuwashirikisha watu wengine.

Na wakaweza kupewa mtaji pesa/bidhaa ili kuanza biashara wanayotaka.

Ili utumie mtaji huu, moja ni LAZIMA wazo lako lionekana kuwa linatekelezeka bila shaka.

Na pili uwe na uwezo wa kulielezea vizuri.

Hakikisha wazo lako unalielezea kwa watu ambao wanaweza kuwa na UTAYARI.

Na wana UWEZO wa kuwa sehemu ya utekelezaji wa wazo hilo.

Kuna watu wengi sana ambao unakuta wanatafuta mtaji.

Ila ukiwauliza kuhusu wazo lao la biashara hawana uwezo wa kulielezea.

Jifunze kujenga uwezo wa kufanya “Elevator Pitch”.

Uwezo wa kuelezea wazo lako kwa mtu ndani ya sekunde 90 (Dakika 1.5).

Ili kumvutia na akupe nafasi ya kukusikiliza zaidi.

Hii imetokana na fikra kwamba, ikitokea umekutana na mtu wa muhimu kwenye “lift”.

Lift ambayo inapanda/kushuka ghorofani na unatakiwa kutumia muda huo mfupi kumueleza ili akuelewe.

Hii inamaanisha wewe mwenyewe lazima uwe

umelielewa sana.

Kumbuka watu wengi ambao unatamani kuwaeleza wazo lako ili wakuunge mkono wako bize sana.

Na pia huwa wanapata maombi kutoka kwa watu wengi sana.

Watu wakiamini wazo lako, wanaweza kuweka pesa kwenye wazo lako.

Tena bila wewe kuhitaji kuweka pesa yoyote ile.

Kitu kikubwa kwenye kuelezea wazo lako ni kuonesha namna ambavyo pesa itakayowekezwa itarudi kwa muda

mfupi.

Na uendelevu wa biashara katika kutengeneza faida.

Watu wengi wanataka kupata uhakika wa pesa zao kurudi.

Na pia kuendelea kupata faida ya muda mrefu kutokana na uwekezaji wao.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment