SIRI YA KUTENGWA KATIKA KUFIKIA HATUA MPYA YA JUU ZAIDI.

Nimebahatika kusoma biblia mara kadhaa, na kugundua jambo hili muhimu sana. MARA NYINGI KAMA SI ZOTE, MUNGU ANAPOTAKA KUMUINUA MTU HUANZA NA KUMTENGA NA WATU, MAZINGIRA, TABIA, NA MAZOEA YA AWALI AMBAYO YAWEZA MKWAMISHA KUFIKIA HATIMA ALIYOKUSUDIWA.

Ibrahimu alitengwa kwa kuambiwa ATOKE NA KUACHA WATU ALIOWAPENDA SANA ( Mwanz 12:1
Yakobo japo alionekana anamkimbia Esau ndugu yake asiuwawe, ila ukweli alikuwa anatengwa na mazingira ambayo yangemvuruga asifanikiwe, MAANA VITU VYA THAMANI HAVIPATIKANI KWENYE MAZINGIRA YA KAWAIDA, VIKO MAFICHONI NA KUVIPATA LAZIMA ULIPE GHARAMA YA JASHO, KAZI, MAOMBI, MAUMIVU, KUFUNGA, KUFUKUZWA, KUACHWA/ KUACHA BAADHI YA VITU NA WATU. ( Mwanz 27)

Musa alikimbia Misri, hatimaye akakutana na Mungu (Ebr 11:25) alichagua mateso ya WATU wa Mungu kuliko fahari ya Misri.

Yesu mwenyewe kabla hajaanza kazi, alijitenga kwa siku 40 akiwa na MAOMBI.

IPO mifano mingi Sana, ambayo muda hautoshi kuisema, KAMA HUJAGUNDUA ALAMA HII MUHIMU SANA YA MAUMIVU ILA YENYE FAIDA BASI JUA LEO NA JIANDAYE BADALA YA KULIA NA KUVUNJIKA MOYO, ANZA KUIONA GHARAMA HII KUWA NI ALAMA YA KUHAMA HATUA MOJA KWENDA NYINGINE. Hivyo jifunze kukiachia kimoja cha kukukwamisha ili upate kingine cha kukubariki, maana ukitaka vyote, Utaishia kupoteza vyote.

Upweke unaoupata uangalie vizuri, na kubali kulipa Gharama yake kwa KUACHA mapenzi ya Mungu yatimie ili uende hatua kubwa zaidi ya kile Mungu amekukusudia uwe.



CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!

Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.




Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment