Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore
Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, inaendelea kusikilisha kesi iliyofunguliwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya jirani yake Rwanda, ambapo inaituhumu Kigali kwa kukiuka uhuru wa nchi yake na kuwahami waasi.

Katika kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa katika mahakama ya EAC yenye makao yake mjini Arusha, Tanzania, Kinshasa inasema kando na kuwahami waasi wanaotatiza usalama wa nchi yake, Kigali pia imewatuma wanajeshi kwenye ardhi yake.
Raia wa mashariki mwa DRC wamekuwa wakikabiliwa na utovu wa usalama kutoka kwa makundi yenye silaha zaidi ya 120, Makundi hayo yakiripotiwa kutaka kudhibiti sehemu za madini sawa na kuonyesha ubabe kati yao.
Licha ya kutaka kudhibiti maeneo ya uchimbaji madini, baadhi ya makundi yao yenye silaha yameripotiwa kutekeleza mauaji ya mamia raia.
Congo imekuwa ikiituhumu Rwanda kupitia wanajeshi wake kwa kutatiza usalama kwenye sehemu hiyo ya nchi yake, tuhuma ambazo hata hivyo Kigali imekanusha.
Wanajeshi wa Rwanda kati ya Elfu tatu na nne, wanasaidiana na waasi wa M23 kupigana nchini DRC kwa mujibu wa ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa ya mwezi Julai.

Kesi hiyo inaendelea ikiwa imepita siku moja baada ya Rais wa DRC, Felix Tshisekedi kuliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuiekea Rwanda vikwazo kwa kuwahami waasi wa M23.
Mahakama ya EAC inasikiliza kesi kutoka katika nchi wanachama ikiwemo Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda, Uganda na imeidhinishwa na Umoja wa Mataifa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.