Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore
Umoja wa Mataifa unasema karibia watu 3,661 wameuawa nchini Haiti mwaka huu peke katika machafuko yanayotekelezwa na magenge yenye silaha.

Watu wenye silaha wamekuwa watatiza usalama wa raia haswa katika mji mkuu wa Port-au-Prince, ambao kwa sehemu kubwa unadhibitiwa na magenge hayo.
Karibia raia laki sita waliripotiwa kupoteza makaazi yao katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka huu wa 204, watu 1,280 wakiripotiwa kujeruhiwa kwenye machafuko hayo.

Kwa mujibu wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR), wanawake 295 na watoto 63 wamejeruhiwa.
Katika kipindi hicho, karibia watu 893 wakiwemo watoto 25 waliripotiwa kutekwa ambapo watekaji wao walidai kulipwa kikombozi kabla ya kuwaachia.

Takwimu za hivi karibuni za Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR), zinaonyesha kwamba karibia watu 3,661 wameuawa tangu mwezi Januari mwaka huu, kutokana na kuongezeka kwa machafuko.
OHCHR imetoa wito kwa mamlaka ya Haiti ya jamii ya kimataifa kuchukua hatua zaidi kuhakikisha kwamba raia wanalindwa.
Katika ripoti yake shirika hilo la UN linasema makundi yenye silaha yamebadili mbinu zake za oparesheni. Licha ya waathiriwa kuuawa kwa kupigwa risasi, baadhi walinyongwa mchana kwa kudaiwa kutoa taarifa kwa maofisa wa usalama.
Mwezi Oktoba mwaka wa 2023, Baraza la Usalaam katika Umoja wa Mataifa lilikubali kutumwa kwa kikosi cha kimataifa cha polisi wanoongozwa na Kenya kwenda nchini Haiti kusaidia kurejesha usalama.
Soma pia#kenya kutuma polisi zaidi nchini #haiti
Rais wa Kenya William Ruto akizungumza katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, amesema nchi yake inalenga kuwatuma polisi 2,500 kwenda nchini Haiti kufikia mwezi Januari.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.