Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu yawekeza kwenye hospital za dharura

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Dunia imeshuhudia kuongezeka  kwa mizozo hali ambayo imezidi  kuongeza hitaji la huduma za afya za dharura.

Hospitali ya dharura  iliyojengwa na ICRC eneo la Gaza
Hospitali ya dharura iliyojengwa na ICRC eneo la Gaza © ICRC

Kukabili changamoto hii ,kamati ya kimataifa ya msalaba  mwekundu ;ICRC ,inaendelea kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya wanaotumwa kwenye maeneo ya mizozo kama vita ,kuweza kutoa huduma za dharura kwa muda mfupi.

Hospitali hizo za dharura zinajengwa kutumia hema
Hospitali hizo za dharura zinajengwa kutumia hema © ICRC

Katika mafunzo hayo yanayofanyika jijini Nairobi ,kwa mara ya pili ,Claire Durham mratibu wa mafunzo hayo ,amesema wahudumu hao wanajifunza kutumika kwa pamoja na kuweza kuweka hospitali kamili ndani ya saa 96.

“Tunalenga kuwaonesha kinachohitajika kuhudumu katika mazingira isiyo rafiki , na pia kukutana na wahudumu wengine ambao watahudumu pamoja ,hivyo basi sehemu ya mafunzo hayo ni kuweka pamoja timu inayofanya kazi pamoja na kwa haraka ,kwa sababu watatumwa sehemu na wanahitajika kuwasili sehemu na haraka kuweka vifaa vya kuhudumu kwa hiyo hii inawapa fursa kutangamana kabla kuanza kazi,”alielezea tulipozuru taasisi ya KCB mtaa wa Karen ,Nairobi ambapo mafunzo hayo yanafanyika

00:31

CLAIRE DURHAM Mratibu wa operesheni za hospitali za dharura ICRC

Wahudumu hao wa afya wanaotokea sehemu tofauti wanahitajika kuweka pamoja timu ,kuunda taratibu zinazohitajika kuwashughulikia waathiriwa wa mizozo.

Sehemu ya mafunzo hayo ni mazoezi ya kuigiza mazingira na hal tofauti za  dharura kuwatumia wagonjwa wa kuigiza kwa ushirikiano na shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya.

Paulin Banguti ni muuguzi katika chumba cha operesheni katika ICRC.

“ Hujui kesho watakuita kwa sababu gani ,unaweza kuitwa kwa sababu ya vita ,risasi au watu wameanguka wengi,Cholera au Malaria.Wakati tunakutana hivi tunaigiza mazingira tofauti za dharura,unasema ,ikiwa hivi tutajibu vipi?Tumejenga hospitali kutumia hema ambayo ina kila kitu cha msingi ,wakituita mahali kila kitu kimebomolewa tunatoa huduma zote za msingi ,kuna za dharura ,matunzo maluum;operesheni,yaani kila kitu kinachofanyika hospitali kwa muda mfupi ,”alielezea Paulin Banguti.

00:38

PAULIN BUNGUTI Muuguzi katika chumba cha operesheni ICRC

Kundi la ICRC linapokwenda kuweka hospitali hizo za muda  ambazo zinajengwa kutumia hema wanaweka mipango ya kupata maji yao ,umeme na miundo mbinu zingine zinazohitajika.

Baadhi ya nchi ambazo hospitali hizo zimefaidi ni nchi za Ethiopia ,Sudan ,Chad na Gaza

Kusambaza :

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment