DRC: Raia Kamituga wakabiliwa na changamoto kuelekea utoaji wa chanjo ya Mpox

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inatarajiwa kuanza kuchoma chanjo ya Mpox tarehe 2 ya mwezi Oktoba katika kampeni ambayo hata hivyo inakabiliwa na changamoto kadhaa.

Serikali ya DRC inatarajiwa kuanza kuchoma chanjo ya mpox wiki ijayo.
Serikali ya DRC inatarajiwa kuanza kuchoma chanjo ya mpox wiki ijayo. © Moses Sawasawa / AP

Raia katika mji wa Kamituga, Mji wenye utajiri wa madini mashariki mwa taifa hilo, wanamatumaini ya kuwa miongoni mwa watu walioratibiwa kupokea dozi za kwanza za chanjo hiyo ya Mpox.

Lakini licha ya wakaazi wa Kamituga kuwa tayari kupata chanjo hiyo muhimu kujilinda dhidi ya maambukizo, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya usafiri miongoni mwa zengine.

Hapa kuna barabara moja peke inayoingia kwenye mji huo wa Kamituga, hali inayoifanya kuwa vigumu kwa magari yaliobeba chanjo za mpox kuwasili kwa wakati na kuwafikia watu wengine walio vijijini na maeneo yalioko mpakani.

Chanjo ya mpox ikiwasili jijini Kinshasa kutoka kwa Umoja wa Ulaya  Tarehe 5 ya mwezi  Septemba 2024.
Chanjo ya mpox ikiwasili jijini Kinshasa kutoka kwa Umoja wa Ulaya Tarehe 5 ya mwezi Septemba 2024. © EUROPEAN UNION / AFP

Sehemu kubwa ya wakaazi kwenye mji huo hutumia malori kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyengine, wachache walio na uwezo, wakifanikiwa kutumia usafiri wa texi.

Kando na malori na texi, wakaazi wengine wanalazimika kutumia usafiri wa pikipiki kuwapeleka kwenye hospitali pamoja na kufanya shughuli zengine kwa kuwa ndio njia rahisi ya usafiri inayopatikana kwa haraka.

Mji wa huo ambao uliripoti mlipuko wa Mpox mwezi Septemba mwaka wa 2023, unapatikana umbali wa kilomita 180 sawa na maili 112 kutoka katika mji wa Bukavu mashariki mwa DRC.

Wahudumu wa afya wakiwahudumia wakimbizi kwenye kambi mashariki mwa DRC ambapo maambukizo ya mpox yameripotiwa.
Wahudumu wa afya wakiwahudumia wakimbizi kwenye kambi mashariki mwa DRC ambapo maambukizo ya mpox yameripotiwa. © Arlette Bashizi / Reuters

Usafiri wa pikipiki umetajwa na waakazi kuwa hatari kwa sababu ni rahisi kuambukizwa mpox haswa mhudumu wa pikipiki anapogusana kwa ukaribu na mgonjwa aliyeambukizwa.

Licha ya mamlaka katika mji wa Kamituga kuripoti kwamba unakaliwa na karibia wakaazi 280,000, raia wanasema huenda idadi ya wakaazi inakaribia laki tano.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment