Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hivi unajua kuna wetu wengi sana wamekuwa na mioyo ya ukatili sio kwa sababu walitaka iwe hivyo, Ila kwa sababu ya yale waliyopitia…
Kuna watu waliumizwa na watu wao wa karibu, tangu wapitie hiyo hali, imewajengea moyo mgumu sana wa kutoamini watu wao wa karibu.
Kuna wale ambao waliteswa na kunyanyaswa huko nyuma, usifikirie eti watabakia kuwa watu wa kawaida. Mioyo imebakia na makovu.
Hivi unajua kuna watu ambao ni ngumu tena kuhisi Upendo? Yaani, wewe unaweza kudhani kuwa wanakupuuza au hawajali unachowafanyia.
Ila, ukija kuchunguza unagundua kuwa ni kwa sababu walipitia mambo magumu sana yaliyofanya moyo wao uwe na ganzi.
Hii ndio maana, kabla haujamshangaa na kumuhukumu mtu, tafuta kujua kilichomsibu, itakusaidia njia rahisi ya kuishi naye.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.