AINA 5 Za MARAFIKI MIZIGO & NAMNA Ya KUISHI Nao…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Marafiki Wasiokiri Makosa Yao.

ii. Marafiki Wanaopenda Kuchukua Sifa Zote.

iii. Marafiki Wanaokuonea Wivu.

iv. Marafiki Wakosoaji Kwenye Kila Kitu.

v. Marafiki Ambao Hawapendi Kulipa.

Leo katika makala hii tutaangalia aina ya kwanza ya MARAFIKI MIZIGO.

– Marafiki Wasiokiri Makosa Yao.

Hawa ndio watu wanaojiita Mr Right.

Wanajiona wapo sahihi kwenye kila jambo.

Wanajiona wao ni bora katika kila jambo.

Watu ambao hata kama wao ndio wanakosea…

…wanatengeneza mazingira ya kukufanya wewe ndio uonekane mkosaji.

Watu ambao hawako tayari kuomba msamaha.

Wanajiona wako sawa kwenye kila jambo.

Ni marafiki ambao wanaamini chochote

wanachofanya ni sahihi.

Na ukitaka kukosana nao, basi jaribu kuwakosoa.

Hata wakija kwako ili kukuomba ushauri wanakuwa tayari wana majibu yao.

Hivyo hawataki uwashauri kinyume na matakwa yao.

Wanachotaka haswa ni kutafuta uhalali wa maamuzi yao kutoka kwako…

…na sio kujua mtazamo wako juu ya maamuzi yao.

Watu hawa ni mzigo sana unapokuwa karibu nao.

Wanataka kuwa juu yako siku zote na

kukukandamiza kwa kila jambo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment