Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore
Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso imesema imefanikiwa kuzuia majaribio kadhaa ya mapinduzi yaliokuwa yamepangwa na afisa wa juu wa jeshi.

Hili limethibitishwa na Waziri wa usalama, ambaye amemtaja aliyewahi kuwa kiongozi wa kijeshi Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, kuhusika, huku washukiwa wengine wakikamatwa.
Luteni Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba, aliondolewa madarakani mwaka wa 2022.
Miongoni mwa watu wengine wanaozuiliwa kwa kuhusika na jaribio hilo ni pamoja na Ahmed Kinda, kamanda wa zamani wa kitengo maalum cha jeshi.
Damiba alichukua madaraka mwezi Januari mwaka wa 2022 baada ya kuangusha utawala wa aliyekuwa rais Roch Marc Christian Kabore.

Baada ya miezi minane madarakani, Damiba aliondolewa na kapteni Ibrahim Traore, mwenye umri wa miaka 34 ambaye kwa sasa ndiye rais wa kijeshi.
Chini ya utawala wa Traore, Burkina Faso imekatisha uhusiano wake na mkoloni wake wa zamani nchi ya Ufaransa na kuonekana kuegemea upande wa Urusi.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.