Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi imethibitisha kuzuiliwa kwa raia wake watatu nchini Chad.

Kwa mujibu wa Wizara hiyo, raia hao watatu wanaoshikiliwa nchini Chad ni pamoja na Maxim Shugaley, Samer Sueifan na E. Tsaryov, ikisema serikali ya Moscow imechukua hatua stahiki kuhakikisha wanaachiwa huru.
Shirika la habari la Urusi RIA Novosti limesema Shugaley na Sueifan, ambao limewataja kuwa wanasosholojia, wamekuwa wakizuiliwa katika uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Chad tangu tarehe 19 ya mwezi Septemba.
RIA Novosti imeeleza kwamba watu hao wanazuiliwa bila ya kueleza sababu za kushikiliwa kwao baada yao kuzuru Ufaransa, mshirika wa Chad bila ya kuwepo kwa matatizo.

Moscow pia imeeleza kwamba raia wa Belarus naye pia anazuiliwa, ikimtaja raia huyo kama A. Denisevich.
Serikali ya Urusi ipo kwenye mawasiliano ya karibu na mamlaka nchini Chad kuhusiana na suala hilo.
Shugaley anaoongoza shirika la kiraia la Foundation for the Defence of National Values, shirika ambalo ni sehemu ya kundi la wanahabari ambalo Marekani imelihusisha na wapiganaji wa Wagner.

Shugaley, 58, kwa upande anakabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa kuhusishwa na kuwa na ushirikiano na aliyekuwa mkuu wa Wagner Prigozhin.
Anatuhumiwa kwa kuongoza propaganda na upotoshaji wa ajili ya mamluki wa Wagner.
Shugaley na Sueifan waliwahi kukamatwa nchini Libya mwezi Mei mwaka wa 2019 wakituhumiwa kuwa kupanga njama ya kuhitilifiana na uchaguzi mkuu wa urais kwa niaba ya Moscow.
Waliachiwa huru mwezi Desemba mwaka wa 2020 baada ya kuzuiliwa kwa kipindi cha miezi 18.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.