Kenya: Mafuta ya kupika yasiokidhi viwango yazua wasiwasi jijini Mombasa

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Nchini Kenya wiki iliyopita, Shirika la kukadiria ubora wa bidhaa (KEBS), lilibainisha kuwa mafuta ya kula yasiyokidhi viwango, yaliingizwa nchini humo mwaka uliopita, hali ambayo imezua taharuki miongoni mwa watumiaji jijini Mombasa.

Inaelezwa kwamba mafuta hayo yaliingizwa nchini Kenya mwaka uliopita.
Inaelezwa kwamba mafuta hayo yaliingizwa nchini Kenya mwaka uliopita. © Albane Thirouard/RFI

Afisa mkuu mtendaji wa KEBS Esther Ngari amesema sampuli ya mafuta ya kupika walizochukua na kufanyiwa uchunguzi zilifeli ubora unaohitajika nchini Kenya kwa kuwa hazikuwa na virutubishi A.

Tulifanya uchunguzi kwa makasha manane na majibu tuliyopata yanaonyesha zimefeli, kwa kadiri ya shirika la kukadiria ubora wa bidhaa inavyohusika haya makasha yalikataliwa.” alisema Esther Ngari.

Doris Wasu, anamiliki duka katika mtaa wa Mishomoroni jijini Mombasa.

Kabla haijatufikia sisi serikali inafaa izuie na ichunguze kwanza, sisi tunanunua, tunafanya biashara, sasa hatuwezi kutofautisha kati ya mafuta mazuri na mabovu.” alieleza Doris Wasu mkaazi wa Mishomoroni.

Peter Charles ni mfanyibiashara anayepika na kuuza chakula kwa umma, anatoa maoni yake kuhusu mafuta hayo.

“Tunaomba serikali kwamba bidhaa ambayo inatumika kutengeneza chakula ikazidi kufanyiwa uchunguzi ili kuboresha afya ya wananchi.”

Tayari lita milioni 32 ya mafuta hayo imeuzwa humu nchini.  Serikali ya Kenya iliagiza lita milioni 53 ya mafuta ya kupika kutoka mataifa ya Misri, Malaysia na Indonesia.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment