Maofisa nchini Lebanon wameripoti kwamba raia nchini humo wanapokea ujumbe wa simu kutoka kwa Israeli ikiwaonya kuondoka, Ofisi wa Waziri wa mawasiliano Ziad Makary ikithibitisha kupokea moja ya ujumbe huo.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ripoti hii imekuja baada ya jeshi la Israeli kutoa taarifa kwa raia wa Lebanon kuondoka katika maeneo yanayoelezwa kwamba yanakaliwa na wapiganaji wa Hezbollah.
Israeli imeapa kutekeleza mashambulio mazito dhidi ya wapiganaji hao wa Hezbollah wanaouungwa mkono na Iran.

Hili limetajwa kuwa onyo la kwanza kutoka kwa Israeli kwa raia wa Lebanon tangu kuzuka kwa mapigano katika ukanda wa Gaza karibia mwaka mmoja uliopita.
Shirika la habari la kitaifa nchini Lebanon National News Agency (NNA) limeripoti kwamba raia kutoka katika maeneo ya Beirut pamoja na sehemu nyengine walikuwa wanapokea ujumbe huo wa onyo ambao umetoka kwa jeshi la Israeli wakitakiwa kuondoka kwa haraka.

Shirika hilo limeeleza kwamba ujumbe huu wa onyo ni mojawapo ya vita vya kisaikolojia ambavyo Israeli inatumia.
Ofisi ya Makary iliokaribu na mji wa Beirut imethibitisha kupokea simu ambayo ilikuwa na ujumbe uliorekodiwa, ujumbe huo ukiwataka kuondoka kwenye jengo lao ilikuepuka kushambuliwa.
Watu wengine wemethibitisha kupokea ujumbe wa simu wenye onyo sawa na hilo kutoka kwa mtu ambaye nambari yake imefichwa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.