Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Matumizi Juu Ya Kipato
ii. Kutumia Pesa Nyingi Kwenye “Sunk Cost”
iii. Kutokuuza Kwa Uwingi
Katika makala hii Leo tutajifunza kuhusu kitu cha kwanza.
Matumizi Juu Ya Kipato
Mara nyingi watu wakipata pesa za kuanza biashara huwa wanaziona nyingi sana.
Kuna watu ambao kwa mara ya kwanza wanashika pesa nyingi ni zile ambazo ndio wamezipata kwa ajili ya kuanza biashara na unakuta akili yao inakuwa kama imechanganyikiwa.
Kwa sababu hiyo, unakuta wanaanza kutumia pesa za biashara kwa mambo ambayo hayahusiani na biashara.
Yaani mtu anaweza hata kuchukua sehemu ya hiyo pesa na kununua gari, simu mpya, nguo mpya, kuanza kusaidia watu na pesa za biashara au hata kusafiri kwenda kutembea mahali.
Muda anakuja kushtuka, pesa zilizobakia kufanya nazo biashara zimeshaisha.
Kwenye somo la uhasibu nilipokuwa kwenye shahada ya kwanza Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, tulifundishwa kanuni 10 za uhasibu na Profesa Mussa Assad.
Moja ya kanuni aliyoisisitiza sana ilikuwa inaitwa “Business Entity” inayosema, wewe na biashara ni vitu viwili tofauti.
Yaani usitumie pesa zako za mtaji wa biashara kwa matumizi binafsi.
Matumizi yako binafsi yanatakiwa kutokana na faida utakayopata kwenye biashara unayofanya.
Usitumie pesa za biashara kuonesha kuwa umefanikiwa, tumia pesa za biashara kufanya biashara.
Ukihitaji kujifunza kwa kina vitu vingine vitatu VINAVYOPOTEZA MTAJI Wa biashara nashauri usome eBook MPYA ya MTAJI, Mbinu Rahisi Za Kupata Mtaji Wa Biashara.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.