VISA Na MIKASA ANAYOKUTANANAYO MKOMBOZI Wa FAMILIA…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

i. Mzigo Mzito Wa Kusaidia Wengi

ii. Majanga Yasiyoisha

iii. Upweke

iv. Hausaidiwi Na Uliowasaidia

Leo katika makala hii tutaangalia jambo la tatu.

– Upweke

Maisha ya mkombozi wa familia mara nyingi sana huwa ni ya upweke.

Hii ni kwa sababu watu huwa wanamini kuwa wewe ni mtu hodari usiyehitaji kufarijiwa kwenye chochote.

Ni kama wanaamini kuwa wewe huwa hausikii maumivu kabisa kwenye lolote.

Kwa sababu hii, watu wengi sana hawatakutafuta kukusalimia au kukujulia hali.

Wengi wao ambao watakutafuta ni wale ambao watakuwa wanahitaji msaada kutoka kwako.

Watu wengi huwa sio marafiki zako au ndugu zako wa karibu.

Mara nyingi huwa wanajitokeza pale wanapokuwa wanahitaji msaada wako.

Ukihitaji kujifunza kwa kina zaidi kuhusu visa na mikasa anayokutana nayo Mkombozi Wa Familia nashauri usome eBook yangu ya Vita Ya Mkombozi Wa Familia.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment