Umeshawahi Kupitia “Wilderness Training”?

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Hiki ni kile Kipindi ambacho unabakia peke yako mithili ya mtu aliyeachwa jangwani bila msaada.

Yaani, ni Kama kila mtu amekuacha na hana mpango na wewe.

Walizoea kukutafuta hawapatikani tena, na wale unaowatafuta hawakujali tena.

Yes, kuna wengine uliwasaidia na ulidhani kwa nafasi na uwezo wao wanatakiwa kukusaidia kwa Sasa, Iła hautawaona tena.

Ni Kipindi cha kupitia Jangwani ukiwa unapewa mafunzo kwa ajili ya kule unakoelekea.

Kipindi na majira haya, ndoto nyingi sana zinakufa na watu wengi sana wanapoteza tumaini, usiwe mmoja wao.

Kama leo unapitia hali hii napenda kukumbusha kuwa, haitakuwa ya mwisho na wewe sio wa kwanza.

Usikate tamaa kuendelea kufukuzia ndoto yako KUBWA kwa sababu ya changamoto ya muda Mfupi unayoipitia.

Utavuka salama, Tena utavuka kwa ushindi. Baada ya Jangwa ni Faraja, Don’t Give Up.

Kama umeipenda makala hii..

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment