Uganda: Sitowania urais ifikapo mwaka wa 2026: Muhoozi Kainerugaba

Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kiume wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza kuachana na mipango ya kuwania urais mwaka 2026, na badala yake atamuunga mkono baba yake.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkuu huyo wa Majeshi ya Uganda, kupitia ukurasa wake wa X ameandika kuwa, kwa sasa kazi yake kubwa ni kukiongoza kikosi cha UPDF.
Mkuu huyo wa Majeshi ya Uganda, kupitia ukurasa wake wa X ameandika kuwa, kwa sasa kazi yake kubwa ni kukiongoza kikosi cha UPDF. AP – Hajarah Nalwadda

Mkuu huyo wa Majeshi ya Uganda, kupitia ukurasa wake wa X ameandika kuwa, kwa sasa kazi yake kubwa ni kukiongoza kikosi cha UPDF.

Kainerugaba, ameongeza kuwa anamuunga rais Museveni ambaye hivi maajuzi alitimiza miaka 80 kuwania tena uongozi wa nchi hiyo.

Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kiume wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza kuachana na mipango ya kuwania urais mwaka 2026.
Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa kiume wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametangaza kuachana na mipango ya kuwania urais mwaka 2026. AFP – PETER BUSOMOKE

Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, hajatangaza rasmi kuwa atawania tena, lakini dalili zote zinaonesha kuwa kwa mara nyingine atapeperusha bendera ya chama tawala NRM wakati wa uchaguzi huo.

Kabla ya tangazo hili, Kainerugaba amekuwa akisema atawania uongozi wa nchi hiyo huku wachambuzi wa siasa wakisema ni wazi kuwa rais Museveni anamwandaa mwanaye ili amrithi katika miaka ijayo.

Muhozi amesema amechukua hatua hiyo ilikumuunga mkono baba yake
Muhozi amesema amechukua hatua hiyo ilikumuunga mkono baba yake AP – Bebeto Matthews

Aidha katika tangazo lake, Kainerugaba, amesema kuwa raia wa kawaida hawezi kuongoza Uganda na rais ajaye baada ya Museveni ni lazima awe mwanajeshi au polisi.

Kiongozi mkuu wa upinzani Bobi Wine, amesema ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, hajashangazwa na tangazo la Kainerugaba kwa sababu ni wazi kuwa baba yake atawania tena urais mwaka 2026.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment