Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, hapo jana alipokea tathmini ya mchakato wa mazungumzo ya amani yanayoratibiwa na Angola toka kwa waziri wa mambo ya nje wa Luanda, Tete Antonio, jijini Kinshasa.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ziara ya Tete nchini DRC, imekuja siku chache kupita tangu mawaziri wa mambo ya nje wa DRC, Angola na Rwanda, wakutane mjini Luanda kwa mazungumzo zaidi yaliyolenga kufikia muafaka kuhusu mchakato utakavyokuwa na kuwasilishwa kwa wakuu nchi.
Waziri huyo amesisitiza utayari wa rais João Lourenço, kufanya kazi kwa karibu na watu wa Congo katika kuhakikisha amani inarejea mashariki mwa nchi hiyo na kutoa nafasi ya shughuli za uchumi na maendeleo kufanyika kwa utulivu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Angola, licha ya tofauti zilizoshuhudiwa katika kikao cha juma lililopita, Rwanda na DRC zote kwa pamoja zimekubaliana kimsingi kuheshimu mchakato wa amani wa Luanda.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.