Rais wa Kisiwa cha Comoro Azali Assoumani aliyeshambuliwa kwa kisu wiki iliyopita na kujeruhiwa,ameonekana kwa mara ya kwanza.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kiongozi huyo ameonekana, kwenye mkanda wa Video akiwa, amefungwa bandeji zito upande wa kushoto wa kichwa chake.
Rais Assoumani ameonekana, akitabasamu wakati akishuka kwenye gari lake, katika majengo ya rais jijini Moroni.
Baadaye, alionekana pia akisalimiana na washauri na mawaziri wake, kabla ya kuchukua majalada na kuanza kuyasoma.
Hii ndio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 kuonekana, baada ya kushambuliwa na mwanamume aliyetambuliwa kuwa mwanajeshi, wakati akihudhuria mazishi ya kiongozi wa kidini Salimani-Itsandra, wiki iliyopita nje kidogo ya jiji kuu Moronoi.
Baada ya kutoonekana hadharani wiki hii wakati ya maadhimisho ya Maulid, maswali yalizuka kuhusu afya ya kiongozi huyo ambaye ripoti zinasema, ameahirisha ziara yake jijini New York kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoanza Septemba tarehe 22.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.