Mapambano yetu ni tofauti.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore

Usisahau kuwa, mapambano yetu yako tofauti. Yaani, kuna watu ambao wametokea kwenye familia ambazo wanajipambania wao, Hawana mzigo wa watu wengine.

Lakini, kuna watu ambao wametokea kwenye familia ambazo, inabidi awapambanie wadogo zake na hadi wazazi wake.

Watu hawa Wawili hawawezi kufanana kwenye vipaumbele vyao vya maisha.

Hii ndio maana, usishindane na mtu ambaye hujui aina Yake ya mapambano.

Kuna wakati watu wanaweza kukuona umechelewa sana kupiga hatua, wengine wanaweza kukuona kama ni mzembe au mtu usiyejielewa.

Wengine wanakulaumu na kukucheka kwa sababu haujajenga, haujanunua gari, hauvai Nguo za gharama n.k Ila hawajui aina ya mapambano unayokabiliana nayo.

Usikate tamaa kwa sababu unaonekana umechelewa ukilinganishwa na wengine.

Endelea kupambana kwa namna iliyo sahihi kwako. Kila mtu yuko ukurasa tofauti wa maisha.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment