Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://radioslist.com/online/ke/fortuneafrica.html#infomore
Kinara wa muungano wa upinzani wa Lamuka nchini DRC Martin Fayulu amemwambia mkuu wa operesheni za kulinda amani wa UN, Jean-Pierre Lacroix, kuushawishi Umoja wa Mataifa kuunga mkono mpango wake wa mazungumzo ya kitaifa kwa ajili ya upatanisho wa Wakongo.
Martin Fayulu aliitoa kauli hiyo hapo jana wakati alipokutana na mkuu huyo wa operesheni za kulinda amani za umoja wa Mataifa, Jean-Pierre Lacroix, ambaye yuko ziarani nchini Jamhuri ya kidemokrasiaya Congo, ambako ameendelea kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali nchini humo,
Mabali na Fayulu, Jean Pierre Lacroix pia alikutana na waziri wa mambo ya nje wa DRC Thérèse Wamba Wagner ambapo alisema jumuiya ya kimataifa inafuatilia kwa ukaraibu mchakato wa upatikanaji wa amani ya mashariki mwa nchi hiyo.
Baada ya kutangamana na wawakilishi wa sacred union, Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anayehusika na operesheni za ulinzi na amani, alikutana na Emmanuel Shadari kutoka FCC na Didier Mumengi, mwakilishi wa Dénis Mukwege, ambapo kwa pamoja walijadili juu ya hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota mkoani Kivu kaskazini na Ituri kufuatia hali ya mapigano, mashariki mwa DRC, na kwamba ipo haja ya kukomesha vita hiyo.
Kabla ya kuondoka Kinshasa kuja mashariki, Jeanpierre Lacroix amefahamisha kuwa Umoja wa Mataifa kupitia MONUSCO wanaunga mkono mpango wa mazungumzo kati ya Wakongo, katika kukabiliana na changamoto kutoka Mashariki, huku akitoa wito kwa tabaka la kisiasa kutilia maanani mchakato wa Nairobi na Luanda kuhusu amani ya mashariki mwa Nchi hiyo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.