Watu wengi wameumizwa na marafiki, media, maadui, shetani, au na watu waliowaamini sana, sababu kubwa ikiwa KUTOJUA MADHARA YA TAARIFA YA PILI AMBAYO WAMEITOA WAO WENYEWE WAKIDHANI WANASAIDIWA WASIJUE HIYOHIYO TAARIFA ITAKUWA SILAHA KALI YA KUWAUWA, KUWAHARIBU, KUWAUMIZA NA KUWALIZA.
Shetani alipokuja kwa Eva aliuliza taarifa ya pili ambayo ama hakuijua au hakuwa na uhakika nayo ila alitaka ushahidi wa muhusika mwenyewe ili apate njia ya kumuumiza na akafanikiwa na kuleta majanga ambayo mpaka leo tunayalipia.
Soma hii Mwanzo 3:1-6
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?… endelea kusoma majibu ya mwanamke… Mwanamke akampa taarifa na akadanganywa kwa ushauri ambao haukufaa.
HAIJALISHI UMEFANYA NINI, LIWE ZURI AMA BAYA MAADAMU ADUI YAKO, RAFIKI YAKO, MTU UNAYEMWAMINI, HANA TAARIFA YA PILI AMBAYO UKWELI WAKE NI WEWE PEKE YAKO UNAUJUA, TAFADHARI USIJARIBU KUMPA HIYO TAARIFA, UKIDHANI KWA KUMPA UTAJITETEA, UTAELEWEKA, UTAJISAFISHA, AMA ATAKUPA UHALALI FULANI. Kama mtu huyo kaonyesha kuitafuta kaa nayo, kwa nini ije ikuumize zaidi? haijalishi unasemwa nini upo ukweli unaoujua wewe, haijalishi unasifiwa ama kuchukiwa upo ukweli unaoujua akitokea mtu anatafuta uhakika wa ukweli huo jihadhari sana USIMPE.
Bora wewe ukaomba ushauri kwa mtu unayemwamini kuwa anaweza kukupa suluhu, kuliko mtu unayedhani anafaa kuitafuta kwa nguvu taarifa yako ya pili ya kilichotokea mwanzo ama kizuri ama kibaya NAKUONYA TENA USIMPE TAARIFA YA PILI KAA NAYO MOYONI MAANA HAIUI, HATA KAMA INAUMA, INATOKOTA, INAWASHA, INATOA MOSHI, JIKAZE USIITOE MUDA UTAKUSAIDIA KUISHINDA HALI HIYO. NYAMAZA NAYO KIMYA MUNGU ATAKUPA MLANGO WA KUTOKEA.
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.