Mkuu wa operesheni za umoja wa Mataifa za kulinda amani amewasili nchini DRC

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkuu wa operesheni za umoja wa Mataifa za kulinda amani, Jean-Pierre Lacroix, jana jioni aliwasili nchini DRC, ambako hivi leo ataanza ziara ya siku tano kwenye taifa hilo.

Jean-Pierre Lacroix, mjumbe wa katibu mkuu wa UN kuhusu operesheni za kulinda amani
Jean-Pierre Lacroix, mjumbe wa katibu mkuu wa UN kuhusu operesheni za kulinda amani UN Photo/Eskinder Debebe

Baadae hivi leo, Lacroix, anatarajiwa kukutana na rais Felix Tshisekedi, waziri mkuu Judith Suminwa pamoja na mawaziri wengine waliochaguliwa hivi karibuni kwenye serikali.

Katika ziara yake, mjumbe huyo wa katibu mkuu atajadiliana na viongozi wa nchi hiyo, kuhusu usalama na hali ya kibinadamu mashariki mwa nchi, wakati huu vikosi vya kulinda amani MONUSCO vikiendelea kuondoka.

Walinda amani wa MONUSCO wakiwa katika eneo la  Kitshanga, Mashariki mwa DRC, 11 Desemba, 2022. (File photo)
Walinda amani wa MONUSCO wakiwa katika eneo la Kitshanga, Mashariki mwa DRC, 11 Desemba, 2022. (File photo) © AFP – Guerchom Ndebo

Aidha, atajadiliana kuhusu mchakato wa mazungumzo ya amani yanayo ratibiwa na Angola ambayo yanaungwa mkono na umoja wa Mataifa pamoja na ushirikiano kati ya vikosi vya MONUSCO na vile SAMIDRC katika kutoa ulinzi wa raia huko Kivu Kaskazini na Ituri.

Lacroix pia atatembelea eneo la mashariki mwa nchi ambako atakutana na wahanga wa machafuko yanayoendelea.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment