Heshimu sana watu wanakuonyesha mlango ndio ule ukabisha ukapata ulichokitamani. Usiwachukulie poa,usiwadharau.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ni kawaida kwa kila mtu kutamani kuwa na mahusiano na mtu ambaye tayari yuko JUU na AMESHAFANIKIWA.

Yaani, kila mtu huwa anatamani kufahamiana na kujuana na Mfanyabiashara Marufu, Kiongozi Mkubwa, Msaani mkubwa n.k

Ila kwenye kanuni mojawapo ya maisha ni kuhakikisha kuwa unawekeza kwa wale ambao WANAINUKA PIA.

Yaani, kuna watu ambao leo HAWAKO JUU, Ila ukiangalia uwezo wao unaona kabisa kuna MAHALI wanaelekea. Hakikisha UMEWEKEZA KWAO.

Watu wengi wamejisahau na kutumia muda Mwingi kuwekeza kwa watu ambao tayari WAMESHAFIKA Juu na wakasahau kuwekeza kwa watu ambao wako kwenye MCHAKATO wa KUPANDA JUU.

Angalia kwenye “field” yako, usihangaike tu na wale ambao wameshapanda tayari, angalia na wale ambao wanapanda JUU PIA.

Kama umeipenda makala hii…

1. NIANDIKIE ulichojifunza kwenye comments kwa ufupi…

2. SHARE makala hii na mtu mmoja unayemjali…

Muda wowote ukiwa tayari nikusaidie kutimiza malengo yako hizi ndio namna 4 ninazoweza kukusaidia.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment