Polisi nchini Tanzanian wamepiga marufuku maandamano yaliokuwa yamepangwa na upinzani kulalamikia kuongezeka kwa matukio ya utekaji na kuuawa kwa wanachama wake.
Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Chama kikuu cha upinzani katika taifa hilo la Afrika Mashariki Chadema kilikuwa kimetoa wito wa kufanyika kwa maandamano makubwa katika mji mkuu wa kibiashara Dar es Salaam tarehe 23 ya mwezi Septemba iwapo serikali haitoanzusha uchunguzi kubaini waliko wanachama wake waliotoweka.
Msemaji wa polisi David Misime amewaambia wanahabari kwamba maandamano hayo yamepigwa marufuku na kwamba polisi watawakabili watu watakaokiuka agizo hilo.

Kulikuwepo na matumaini kwamba Tanzania ilikuwa inaingia katika kipindi kipya cha demokrasia na uhuru nchini ya uongozi wake rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alichukua mikoba kutoka kwa mtangulizi wake Magufuli baada ya kifo chake cha ghafla mwezi Machi mwaka wa 2021.
Rais Samia alikuwa ametoa marufuku iliokuwa inawazuia wapinzani kushiriki maandamano pamoja na kuondoa vikwazo dhidi ya vyombo vya habari.

Mwezi Agosti, viongozi 520 wa Chadema na wafuasi wao walikamatwa nchini Tanzania kuelekea mkutano wao kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana ambapo baadhi yao waliachiwa baadaye kwa dhamana.
Kwa mujibu wa kiongozi wa chama cha Chadema, mamlaka nchini Tanzania inawaua na kuwateka wanachama wake akiwemo Ali Mohamed Kibao, ambaye alipatikana akiwa ameuwa baada ya kutekwa.
Aidha Mbowe alieleza kwamba wameamua kuandamana kwa ajili ya kulinda maisha yao na nchi yao.
Mwezi uliopita, chama cha mawakili kwenye taifa hilo kilisema kwamba watu 83 walitekwa au kupotea kati ya mwaka wa 2016 na 2024.
Mbowe amewataka wakuu wa polisi na wale wa Intelenjisia kujiuzulu kutokana na visa hivyo vya kutekwa na kutoweshwa kwa watu. Vilevile ametoa wito kwa polisi wa Uingereza kusaidia katika uchunguzi kuhusiana na visa hivyo.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.