Wanaokupiga vita wanaogopa ukuu wako kesho.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

VITA unayopigwa haitokani sana na ulivyo au ulichonacho leo.

Wengi wanaokupiga vita ni kwa sababu wanaogopa ukuu wako wa kesho.

Hii ndio maana, kuna wakati utaona mtu amekuzidi kila kitu Ila bado anapambana na wewe.

Yaani, anaweza kukuzidi Cheo, Pesa, Kujulikana n.k Ila ukashangaa bado anapambana ufeli.

Wengi wameshachungulia kinachokuja mbele yako, WANAKUOGOPA utakavyokuwa kesho.

Wanaogopa UKUU WAKO.

Hii ndio maana, usishangae kwa nini wengine HAWAPIGWI VITA Kama wewe.

Ni kwa sababu hawana MBEGU YA UKUU Kama yako.

Usikae mkao wa KUONEWA HURUMA.

Pambania HATIMA YAKO na UILINDE ili wasikupoteze.

Wengine HAWANA HURUMA na wewe, wako tayari kufanya lolote.

Mungu AKUPE UJASIRI kupambana na UPATE USHINDI.

Kama umeipenda makala hii…

1. NIANDIKIE ulichojifunza kwenye comments kwa ufupi…

2. SHARE makala hii na mtu mmoja unayemjali…

Muda wowote ukiwa tayari nikusaidie kutimiza malengo yako hizi ndio namna 4 ninazoweza kukusaidia.

Salamu ziwafikie watu wa Kampala nchini Uganda

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment