Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Eneo la pili ambalo unatakiwa kulizingatia katika kujenga nidhamu ya pesa ni kuweka akiba.
John D. Rockefeller, Mmarekani aliyewahi kuwa tajiri nambari moja duniani aliwahi kusema “If you cannot save money, the seeds of greatness are not in you”
(Kama ukishindwa kuweka akiba ya pesa, basi mbegu za ukuu haziko ndani yako).
Inapofika kwenye suala na akiba, kwanza usianze na kiwango kikubwa sana.
Anza na kidogo ambacho hakitakusumbua na hakikisha unaweka akiba mfululizo bila kuacha.
Lengo hapa ni kujenga TABIA na sio UKUBWA WA KIWANGO.
Jambo la pili ni kuhakikisha kuwa kila kiwango chako kinapoongezeka na wewe uwe unaongeza kiwango chako cha akiba.
Hivyo ni vizuri kujiwekea asilimia ya kiwango cha kipato chako ambacho utakuwa unaweka akiba.
Jambo la tatu na muhimu ni kuwa usiweke akiba KUTOKA KWENYE KILICHOBAKIA baada ya kutumia, bali weka akiba KABLA HAUJATUMIA.
Yaani akiba yako ndio matumizi ya kwanza kwenye bajeti yako.
Ili akiba yako usiitumie hovyo hasa pale unapokuwa haujajenga nidhamu maalumu ya kifedha…
…nakushauri iweke mahali ambapo kuichukua haitakuwa RAHISI au ITAKUPA USUMBUFU.
Maeneo hayo ni kama kwenye VICOBA, SACCOSS, Fixed Deposit, Mifuko ya Pamoja(Mf. UTT) n.k.
Hii itakusaidia kutotoa haraka.
Sikushauri kuweka akiba kwenye salio la simu yako!!!
Je, wewe mwaka huu unapanga kuweka akiba ya kiasi gani kila mwezi?
UMECHOSHWA na hali uliyonayo?
Uko SERIOUS Unataka nikusaidie KUTIMIZA MALENGO YAKO?
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.