Marekani: Kamala Harris na Donald Trump kukutana kwenye mdahalo

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kamala Harris na Donald Trump, wanatarajiwa kuchuana vikali kwenye mdahalo wa Televisheni baadaye siku ya Jumanne, kuelekea uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Novemba.

Makamu wa rais wa nchini Marekani Kamala Harris  na Rais wa zamani Donald Trump kukutana kwenye mdahalo
Makamu wa rais wa nchini Marekani Kamala Harris na Rais wa zamani Donald Trump kukutana kwenye mdahalo AP

Mdahalo huu wa kwanza na wa pekee kati ya Makamu wa rais Harris atakayepeperusha bendera ya chama cha Democratic na rais wa zamani Trump, mgombea wa chama cha Republican, utatazamwa na mamilioni ya Wamarekani na watu wengine duniani.

Wachambuzi wa siasa za Marekani wanasema, Harris mwenye umri wa miaka 59 ana fursa ya kipekee kupitia mdahalo huo, kutafuta uungwaji mkono kwa wapiga kura ambao hawajamfahamu vema, baada ya kuchukua nafasi ya rais Joe Biden aliyetangaza mwezi Julai kuwa, hatowania tena.

Mdahalo huu unafanyika wakati kura za maoni kutoka mashirika ya New York Times na Siena yakionesha kuwa Trump anaongoza kwa asilimia 48 dhidi ya Kamala Harris akiwa na asilimia 47.
Mdahalo huu unafanyika wakati kura za maoni kutoka mashirika ya New York Times na Siena yakionesha kuwa Trump anaongoza kwa asilimia 48 dhidi ya Kamala Harris akiwa na asilimia 47. AFP – BRENDAN SMIALOWSKI,PATRICK T. FALLON

Naye Trump, mwenye umri wa miaka 78, anatarajiwa kutumia mdahalo huo, kupata majibu ya moja kwa moja kutoka kwa mpinzani wake kuhusu masuala ya uchumi na uhamiaji.

Aidha, itakuwa mara ya kwanza kwa wagombea hao wawili kukutana ana kwa ana kwenue mdahalo huo ulioandaliwa na kituo cha ABC jijini Pennsylvania, huku Harris akitarajiwa kuonesha kuwa anaweza kuongoza Marekani.

Mdahalo huu unafanyika wakati kura za maoni kutoka mashirika ya New York Times na Siena yakionesha kuwa Trump anaongoza kwa asilimia 48 dhidi ya Kamala Harris akiwa na asilimia 47, huku ushindani mkali ukitarajiwa kwenye baadhi ya majimbo.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment