Beijing: Kogamano la ushirikiano kati ya China na bara Afrika limeanza.

Radio Fortune Africa-Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Mkutano wa ushirikiano kati ya mataifa ya Afrika na China, unaanza leo jijini Beijing baada ya kuwasili kwa viongozi mbalimbali wa Afrika.

Cheza – 00:56

Senegal's Economy Minister Abdourahmane Sarr, Senegal's Foreign Minister Yassine Fall, China's Foreign Minister Wang Yi, China's Commerce Minister Wang Wentao, chairman of the China International Deve
Masuala ya uongozi, siasa na usalama, pia yatajadiliwa kwenye mkutano huo unaoanza leo hadi siku ya Ijumaa. REUTERS – Tingshu Wang

Kwenye mkutano huo, ushirikiano kwenye masuala ya uchumi hasa maendeleo ya miundo mbinu ndio ajenda kubwa inayowaleta pamoja viongozi wa mataifa ya Afrika na nchi ya China.

Waziri wa Mambo ya nje wa China, Wang Yi amesema makubaliano yatakayoafikiwa kwenye mkutano huo, yanalenga kuimarisha zaidi uhusiano wa Afrika na China, lakini pia kuwawezesha watu kupata maendeleo.

Marais kutoka  nchi za Afrika wanahudhuria kongamano hilo ambalo wanatarajiwa kushinikiza ushirikiano zaidi haswa katika masuala ya miundombinu.
Marais kutoka nchi za Afrika wanahudhuria kongamano hilo ambalo wanatarajiwa kushinikiza ushirikiano zaidi haswa katika masuala ya miundombinu. © Yin Bogu / Xinhua via AP

China inatarajiwa kutangaza ahadi ya uwekezaji mkubwa kwa ujenzi wa miundombinu barani Afrika kwa kutoa mikopo  ya fedha kwa mataifa mbalimbali , na kutoa mchango  wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa mataifa ya Afrika.

China's Foreign Minister Wang Yi delivers a speech at the ministerial conference of the 2024 Summit of the Forum on China-Africa Cooperation (FOCAC) in Beijing, China September 3, 2024
China inalenga kuimarisha ushawishi wake zaidi barani Afrika, ikionekana kutoa upinzani kwa nchi za Magharibi kwenye bara hilo. REUTERS – Tingshu Wang

Wakuu wa mataifa ya Afrika pia kupitia mkutano huu, wanatarajiwa kufungua milango zaidi kwa wawekezaji wa China kwenye nchi zao, kuwekeza kwenye sekta mbambali kama madini na kilimo.

Masuala ya uongozi, siasa na usalama, pia yatajadiliwa kwenye mkutano huo unaoanza leo hadi siku ya Ijumaa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment