Uganda: Bobi Wine kufanyiwa upasuaji baada ya kujeruhiwa kwenye mguu.

Radio Fortune Africa-Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Wakili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Bobi Wine, amethibitisha kwamba mteja wake anatarajiwa kufanyiwa upasuaji, siku moja baada yake kujeruhiwa kwenye mguu wake.

Wakili wa Bobi Wine anasema mteja wake alijeruhiwa baada ya bomu la kutoa machozi kulipukia katika eneo alikokuwa.
Wakili wa Bobi Wine anasema mteja wake alijeruhiwa baada ya bomu la kutoa machozi kulipukia katika eneo alikokuwa. REUTERS – Abubaker Lubowa

Awali chama chake kilikuwa kimeripoti kwamba kiongozi huyo wa upinzani alipigiwa risasi kwenye mguu wake wakati wa mvutano kati yake na maofisa wa polisi.

Bobi Wine, 42, mkosoaji mkubwa wa rais wa Uganda Yoweri Museveni alikuwa katika mji wa Bulindo, karibia kilomita 20 kutoka jiji kuu la Kampala, wakati chama chake cha National Unity Platform (NUP) kiliripoti kutokea kwa tukio hilo.

Ili kuonyesha maudhui haya X (Twitter) maudhui, unahitaji kuidhinisha kipimo cha hadhira na vidakuzi vya matangazo.KubaliDhibiti chaguo langu

George Musisi, wakili wa mwanasiasa huyo, ameiambia AFP kwamba mteja wake kwa sasa hayuko katika hali ya hatari ila kwa mujibu wa madaktari wake anahitaji kufanyiwa upasuaji ilikuondoa vipande vya bomu la machozi kutoka kwenye mwili wake.

Aidha wakili wake amedai kwamba polisi walikuwa wanamlenga kimakusudi mwanasiasa huyo wa upinzani.

Polisi nchini Uganda mara kwa mara wamekuwa wakikabiliana Bobi Wine pamoja na wafuasi wake wa NUP
Polisi nchini Uganda mara kwa mara wamekuwa wakikabiliana Bobi Wine pamoja na wafuasi wake wa NUP REUTERS – Abubaker Lubowa

Siku ya Jumanne, picha kwenye mitandao ya kijamii zilimuonyesha Bobi Wine maarufu kama Robert Kyagulanyi akiwa amelala chini akionekana mwenye uchungu mwingi kabla yake kupelekwa katika hospitali Nsambya.

Musisi, wakili wa Wine aidha ameeleza kwamba tukio hilo lilitokea baada ya maofisa wa polisi kuanza kurusha mabomu ya machozi kuelekea eneo ambapo alikuwa akikutana na wafuasi wake katika mjini Bulindo.

“Bomu la machozi lilipuka katika eneo alipokuwa amesimama na kumjeruhi kwenye mguu wake.” Alieleza wakili wake.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameonekana kutowavulia viongozi wa upinzani wanaokosoa uongozi wake
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameonekana kutowavulia viongozi wa upinzani wanaokosoa uongozi wake AP – John Muchucha

Polisi nchini Uganda siku ya Jumanne walisema kwamba wataanzisha uchunguzi katika tukio hilo ikiwemo madai ya kwamba Bobi Wine alipigwa risasi.

Wine kupitia chama chake cha NUP amekuwa akikosoa utawala wa Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 40.

Aligombea dhidi ya rais Museveni katika uchaguzi wa mwaka wa 2021 ambapo alipoteza, uchaguzi ambao hata hivyo upizani ulitupilia mbali kwa madai ya kuwepo kwa udaganyifu mkubwa.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment