Radio Fortune Africa-Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Ripoti mpya ya umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa inasema, Afrika inakabiliwa na mzigo mkubwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi na gharama za kukabiliana na hali hiyo.
REUTERS – STRINGER
Kwa mujibu wa shirika la hali ya hewa la umoja wa Mataifa, bara la Afrika linashuhudia ongezeko la kasi la kiwango cha joto kuliko wastani wa wa kawaida wa kidunia, ambapo limekuwa likiongezeka kwa nyuzi joto 0.3 kwa muongo mmoja kati ya mwaka 1993 na 2023.
Ukanda wa Afrika Kaskazini ndio umekuwa ukishuhudia ongezeko kubwa la kiwango cha joto, mji wa Agadiri nchini Morocco, ukirekodi kiwango kipya kilichofikia nyuzi joto 50.4, huku mataifa mengine yakishuhudia mvua zilizosababisha mafuriko.
Afrika imeathiriwa pakubwa na mabadiliko ya hali ya hewa licha ya kuchangia asilimia ndogo ya utoaji wa gesi chafu duniani.
Mkutano wa kimataifa wa COP29 ambao nchi ya Azerbaijan itakuwa mwenyeji mwezi Novemba mwaka huu, kwa sehemu kubwa ajenda itakuwa ni namna gani mataifa yaliyoendelea yataendelea kuwajibika kwa nchi masikini katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya halik ya hewa.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.