Unapojiandaa kuingia mwaka mpya.

Leo naanza hivi.

Kila wakala wa shetani aliyekupangia ratiba yake, huyo mpambe wa shetani na ratiba yake wasifanikiwe katika jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.

Kila wakala wa shetani anayekupangia ratiba ya kukuondoa duniani aondoke yeye katika jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.
Ndugu, kaa vizuri na YESU KRISTO na MUNGU atatimiza hesabu ya siku zako.

Kutoka 23:26 “Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza.”

Aliyesema hutabeba mimba katika ndoa yako, ratiba yake naifuta katika jina la YESU KRISTO hivyo atashangaa utabeba mimba na kuzaa.
Mchawi aliyekurushia roho ya kuharibu mimba, aharibikiwe yeye huku wewe uliye mimba ukizaa katika jina la YESU KRISTO Mwokozi aliye hai.

MUNGU atimize hesabu za kuishi kwako duniani, wachawi na nguvu za giza wasikatishe kamwe uhai wako.

Hata kama kuzimu walikuandikia wewe kufa, nakuomba ambatana na MUNGU katika KRISTO YESU maana yeye huwapa kuishi hata walioandikiwa kufa .

Zaburi 102:20 “Ili akusikie kuugua kwake aliyefungwa, Na kuwafungua walioandikiwa kufa.”



CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com

cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!

Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.




Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment