Afrika Leo Jioni -Agosti 28,2024

ALIYEKUWA Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu maarufu kama Baba Yao, mkewe Susan Wangari na mwanakandarasi walijitetea Jumanne Agosti 27, 2024 katika kashfa ya Sh588 milioni ya ujenzi wa barabara 2018 huku mahakama ikifunga kesi hiyo waliyoshtakiwa miaka mitano iliyopita.

Hata hivyo, Waititu alijipata taabani alipoulizwa jinsi alivyomuuzia mwanakandarasi Charles Chege shamba alilolipwa pesa zinazodaiwa zilitoka Kaunti ya Kiambu kabla ya kuwa mmiliki wake rasmi.

Kutokana na kuuziwa huko kwa shamba, hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Milimani, Thomas Nzioki, alifahamishwa kwamba Bw Waititu alipokea kwa njia ya ufisadi zaidi ya Sh25 milioni kutoka kwa Bw Chege akijua pesa hizo zilipatikana kwa njia isiyo halali kutoka kwa Serikali ya Kaunti ya Kiambu, ambapo Waititu Gavana alikuwa.

Waititu alihudumu kama Gavana wa Kiambu kati ya 2017 na 2020.

Gavana wa zamani Kiambu, Bw Ferdinand Waititu akiwa kortini mnamo Agosti 27, 2024. PICHA|RICHARD MUNGUTI

Bw Chege ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya Testimonies Enterprises Limited (TEL) iliyoteuliwa kwa njia tata kujenga barabara katika Kaunti ya Kiambu, aliuziwa shamba lililoko Nairobi na Waititu.

Akijitetea, Bw Waititu alisema alipewa idhini ya kuuza shamba hilo mnamo Januari 2018, lakini hati alizotoa kortini kama ushahidi zilionyesha aliliuza bila hatimiliki.

Waititu, Susan na Charles Chege mmiliki wa TEL walijitetea na kuhojiwa na kiongozi wa mashtaka Faitha Mwila.

Waititu na wenzake walijaribu kujiondolea lawama katika kashfa hiyo.

Mahakama ilifunga kesi dhidi yake (kukamilika kuskizwa) na kuamuru itajwe Oktoba 3, 2024 washtakiwa wawasilishe ushahidi wao wa mwisho kabla ya hukumu kutolewa.

Waititu, mkewe na Chege wamekanusha mashtaka dhidi yao.

Wako nje kwa kwa dhamana.

Mfanyabiashara Charles Chege anayeshtakiwa pamoja na Ferdinand Waititu.

WASHUKIWA saba wanaohusishwa na ongezeko la visa vya ulaghai wakijifanya maajenti wa kazi katika nchi za kigeni mjini Eldoret, wametiwa mbaroni.

Washukiwa hao walikamatwa baada ya msako mkali uliofanywa na makachero kutoka idara ya Upelelezi wa Jinai na Uhalifu (DCI).

Polisi walinasa washukiwa hao katika afisi zao wakiendeleza shughuli zao za kila siku.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu Benjamin Mwanthi alisema kuwa kukamatwa kwao kumefuatia vidokezo kutoka kwa wananchi kuhusiana na shughuli za kutiliwa shaka za mashirika husika.

Maafisa wa upelelezi walipovamia afisi hizo walipata watu ambao walikuwa wakitafuta kazi wakiwa wamepanga foleni katika baadhi ya ofisi hizo za maajenti walaghai kwa ahadi ya kuajiriwa ughaibuni.

Kulingana na Bw Mwanthi, mashirika mengi ya kutoa ajira hizo jijini humo yamekuwa yakifanya kazi bila vibali halali.

Bw Mwanthi alifichua kuwa washukiwa zaidi ya kumi walifanikiwa kukwepa mtego wa polisi

JUMUIYA ya Mamlaka ya Kimataifa kuhusu Maendeleo (IGAD) imependekeza sera ya watoto ambayo itaongoza mataifa wanachama katika udhibitishaji wa haki za watoto.

Sera hiyo inakiri kuwa nchi tofauti zilizomo katika jumuiya ya IGAD zinakumbana na matatizo mbalimbali katika kudhibiti haki za watoto.

Changamoto hizo ni pamoja na vita, vurugu, umaskini, mazingira yasiyomkinga mtoto, kufukuzwa makwao, kutopata huduma za afya, na elimu.

Katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya IGAD, watoto huratibu idadi kubwa.

Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Somalia, South Sudan, Sudan na Uganda, ndio nchi wanachama wa muungano huo.

Nchini Djibouti, kwa mfano watoto wanachangia idadi ya watu wote kwa asilimia 36, Eritrea 46, Ethiopia 46, Kenya 44, Somalia 54, Sudan Kusini 51, Sudan 47 na Uganda asilimia 52.

Changamoto ambazo watoto hawa hupitia katika juhudi za kuwakinga hutokana na watu binafsi, familia na hata jamii kwa ujumla.

Hata hivyo, sera hii ya watoto inanuia kuangazia elimu, lishe bora, usafi wa maji, mazingira na tabianchi, haki na usawa, amani pamoja na ulinzi wa watoto.

Ili watoto hao wanufaike, IGAD iliwahusisha katika mijadala ya kutengeneza sera hii ili maoni yao pia yakadiriwe.

Dkt Victoria Anib, Mkuu wa Maendeleo ya Jamii katika IGAD akihakikisha ahadi ya sera hiyo alisema, “Tunataka kuhakikisha kuwa sera hii inaangazia sera za kitaifa bila kuzipuuza bali kujazilia mapengo yaliyomo.”

Isitoshe, IGAD ilisema kuwa sera hii itasaidia nchi za jumuiya kuwa mstari wa mbele kupigania haki na ustawi wa watoto ili watoto wote watimize wanachonuia maishani.

WAKATI Faith Thuo, 27, alipokuwa mjamzito alianza kupata maumivu kichwani, ujauzito wake ulipokuwa na miezi sita.

Bi Thuo alimwona daktari wake wa uzazi akapewa tembe kadhaa lakini maumivu yale hayakutoweka ndiposa akalazwa.

Vipimo tofauti mwilini mwake vilionyesha kuwa Bi Thuo alikuwa akiugua ugonjwa wa Kisukari unaotokana na ujauzito (gestational diabetes).

“Hapo awali sikuwa na ugonjwa wowote ule wa Kisukari,” anasema.

“Nilianza matibabu lakini sababu ya ugonjwa huu kujulikana ukiwa umechelewa ilibidi nijifungue kabla wakati kutimia (baada ya wiki 37).”

Kwa sababu ya ugonjwa huo, mtoto wake Bi Thuo alizaliwa akiwa mkubwa sana (kilo 3.9).

“Viwango vyangu vya sukari vilirejea kawaida baada ya kujifungua. Niliposhika mimba tena, niliugua ugonjwa huu tena na mtoto wangu akazaliwa akiwa na uzito wa kilo 4.”

Kama ilivyokuwa ada, baada ya kujifungua viwango vya sukari vilirudi hali yake ya kawaida lakini kwa muda tu. “Hivi sasa vinadhibitiwa.”

Ugonjwa huu wa Kisukari ni upi?

Dkt Odero Ong’ech, mtalaamu wa afya ya uzazi katika Nairobi Reproductive Health Services, anasema kuwa ugonjwa wa Kisukari unaompata mama akiwa mja mzito ni mojawapo ya ujauzito ulio na hatari sana (high risk pregnancy).

Kwa wanawake wengi, viwango vyao vya sukari hurejea kama awali wanapojifungua. “Hii ndiyo tofauti ya ugonjwa huu wa Kisukari na hayo mengine; ule unaofanya kongosho kutotengeneza insulini (diabetes type 1) na ule unaofanya kongosho kutengeneza insulini kidogo (diabetes type 2),” anasema Dkt Odero.

Mwanamke aliye na hatari ya kuugua ugonjwa huu wa Kisukari sababu ya kuwa mjamzito ni yule anayetoka kwenye familia ambayo wengi wa wanafamilia wake wanaugua ugonjwa wa Kisukari.

Pili, Dkt Odero anasema ni mwanamke mwenye uzito wa kupindukia (obesity), alikuwa na ugonjwa huu alipokuwa na mimba hapo awali, amejifungua watoto wakubwa (walio na zaidi ya kilo 4), watoto wake wamekuwa wakifariki tumboni (still-births) na wale walio na matatizo ya kihomoni kwa mfano, wanaougua polycystic ovarian syndrome (PCOS).

“Visa vya ugonjwa huu wa PCOS vimeongezeka sana sasa sababu ya kutozingatia lishe bora na afya njema,” anafafanua.

Dkt Odero Ong’ech, mtalaamu wa afya ya uzazi katika Nairobi Reproductive Health Services.
“Nchini Kenya, ugonjwa huu unaathiri angalau asilimia 4 ya wanawake huku asilimia 14 ikirekodiwa duniani. Hata hivyo, idadi haswa ya wanawake nchini inaweza kuwa zaidi sababu ripoti za aina hii hazizingatiwi kwa kina,” anaeleza Dkt Odero.

Utajuaje unaugua ugonjwa huu?

Ugonjwa huu huweza kujulikana katika kipindi cha pili cha ujauzito (second trimester) angalau kutoka wiki 20 hadi 28. Dkt Odero anasema kuwa wakati huo mama hufanyiwa vipimo mbalimbali kuangalia viwango vyake vya sukari.

“Kwa mfano, mama huyo anaweza akapimwa viwango vyake vya sukari kabla hajala chochote au apatiwe sukari nyingi ili mwili wake upigane nayo almaarufu oral glucose tolerance test (OGTT). Iwapo sukari hiyo itaathiri mwili wake basi itaonyesha na tutarekebisha kupitia matibabu mbalimbali.”

Hali kadhalika, Dkt Odero anasema kuwa vipimo vya viwango vya sukari hupendekezwa kwa kina mama wote wajawazito. Kwa wale wanaotoka katika maeneo yenye mapato ya chini, Dkt Odero anashauri kupimwa kwa kutolewa damu kwa kidole (fasting blood sugar) ili kutathmini viwango hivyo vya sukari.

“Pia, kina mama hao wanaweza wakafanyiwa vipimo vya HbA1C ambavyo huangalia wastani wa viwango vyako vya sukari kwa kipindi cha miezi mitatu.”

Mama mjamzito ataweza kujua kama anapata dalili za ugonjwa huu wa Kisukari iwapo anakunywa maji mengi, anaenda haja ndogo sana, ana hamu nyingi ya kula, na anaongezea uzito wake sana. Lakini, iwapo ugonjwa huu umeendelea sana mwilini, Dkt Odero anasema kuwa uwezo wa kuona kwa mama huyo huathiriwa.

“Cha kushangaza ni kwamba, wanawake wengi wajawazito huugua ugonjwa huu bila wao kujua,” anaeleza.

Ili kudhibiti ugonjwa huu, Dkt Odero anasema kuwa ushirikiano wa watalaamu mbalimbali; wakiwemo madaktari wa afya ya uzazi, Kisukari (endocrinologist) na mtalaamu wa lishe (nutritionist) huzingatiwa. Japo tembe (oral hypoglycemic drugs) husaidia kurekebisha hali hiyo, wagonjwa wengine hudungwa sindano za insulini.

Athari za ugonjwa huu kwa mama na mtoto

Iwapo ugonjwa huu hautadhibitiwa ipasavyo, Dkt Odero anafafanua kuwa madhara yake yatamwandama mtoto na mama.

Athari zake kwa mtoto ni pamoja na kuwa mkubwa zaidi (fetal macrosomia) anazaliwa kwa njia ya upasuaji, azaliwe kabla viungo vyake havijakua vizuri (congenital abnormalities), au azaliwe kabla muda wake kufika (preterm babies).

Isitoshe, mtoto huyu anaweza akafia tumboni mwa mamake, au mapafu yake yachelewe kukua.

“Hii ndiyo changamoto kubwa sana ambayo tunakumbana nayo lakini mtoto huyu hupatiwa dawa za kusaidia mapafu yake kukua.”

Kwa upande wa pili, athari za ugonjwa huu kwa mama zinaweza kumfanya apoteze maisha yake au awe mgonjwa mahututi.

Dkt Odero anaongezea kuwa iwapo viwango vyake vya sukari havitadhibitiwa, mama anaweza kuwa kipofu (diabetic retinopathy), figo zake zishindwe kufanya kazi ipasavyo, au mishipa yake iathirike.

“Mama huyu pia yupo katika hatari ya kuugua shinikizo la damu, prekilampsia au augue ugonjwa wa Kisukari maisha yake yote.”

Diabetes
kisukari
Kupoteza mtoto
Mama mjamzito

Dkt Odero Ong’ech, mtalaamu wa afya ya uzazi katika Nairobi Reproductive Health Services. PICHA|HISANI

SERIKALI kwa ushirikiano na Bodi ya Majani Chai Nchini (TBK) imeanzisha kampeni ya kuimarisha ubora wa majani chai yanayozalishwa nchini.

Katibu wa Wizara ya Kilimo Paul Rono na Afisa Mkuu Mtendaji wa TBK Willy Mutai wamesema shughuli ya kuchunguza upya taratibu za utoaji leseni kwa viwanda vya kibinafsi vya majani chai itaanzishwa kwa lengo la kuimarisha ubora wa bidhaa hiyo.

Hayo yanajiri baada ya Gavana wa Bomet Hillary Barchok, mwenzake wa Kericho Dkt Eric Mutai na Naibu Mwenyekit wa Shirika la Ustawi wa Majani Chai Nchini (KTDA) kufanya mkutano mjini Bomet kujadili njia za kuimarisha mapato ya wakulima wa zao hilo.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na wakurugenzi kutoka zoni nane za KTDA na madiwani kutoka maeneo kunakokuzwa majani chai kwa wingi.

“Tunaaangalia upya masuala ya utoaji leseni kama sehemu ya utekelezaji wa mageuzi katika sekta ya majani chai kuhakikisha kuwa viwango vya ubora vinavyozingatiwa na viwanda vya KTDA katika ununuzi wa majani chai mabichi pia vinazingatiwa na viwanda vya kibinafsi kote nchini,” Dkt Ronoh akasema.

“Sharti tuhakikishe kuwa ubora wa majani chai unadumishwa katika ngazi zote za utayarishaji zao hili. Hiyo ndio itatuwezesha kuendelea kushikilia rekodi ya kuwa miongoni mwa mataifa yanayouza nje majani chai kwa wingi na kutuletea fedha nyingi za kigeni,” Dkt Ronoh akaeleza wakati wa mkutano na wakurugenzi wa KTDA na wakulima katika kiwanda cha majani chai cha Tirgaga, Kaunti ya Bomet.

Bw Mutai (Afisa Mkuu wa TBK) alisema maafisa wa ukaguzi kutoka bodi hiyo wanaendesha kampeni ya maeneo kunakokuzwa majani chai kuwaelimisha wakulima kuhusu haja ya kuzingatiwa ubora katika uzalishaji.

“Aidha, kampeni hiyo inalenga kuhakikisha kuwa viwanda vya kibinafsi havikiuki kanuni kuhusu uzingatiaji wa ubora.” akaeleza.

Bw Mutai alisema TBK imepata habari kuwa baadhi ya wafanyabiashara wanachuuza majani chai, hali inayochangia wakulima kupata hasara kwa sababu wanapokea malipo duni na hawalipwi bonasi.

KWINGINEKO DUNIANI

1.Wiki chache baada ya kuandaa mashindano ya Olimpiki, michezo hiyo ya msimu wa joto inaanza ngwe yake ya mwisho leo na sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya wanariadha wanaoishi na ulemavu. Waandaaji wanaahidi maonyesho ya kusisimua wakati wa ufunguzi.

2.Jeshi la Israel limetuma vifaru ndani kabisaa ya mji wa Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, na kufanya mashambulizi kote katika ukanda huo wakati likipambana na wanamgambo wanaoongozwa na Hamas.

3.Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa uingereza Kier Starmer wamekubaliana kuanzisha mpango wa pamoja wa kukabiliana na uhamiaji haramu kupitia njia ya kuvuka bahari. Kuhusu mada nyingine Starmer amesema anataka kuanzisha ukurasa mpya wa mahusiano na Umoja wa Ulaya, lakini akisisitiza kwamba nchi yake haiwezi kurudi ndani ya Umoja huo wa Ulaya.

4.Urusi imesema nchi za Ulaya zitalipa zaidi kwa ajili ya mahitaji ya gesi ikiwa Ukraine haitarefusha mkataba na Urusi wa kupitishia gesi hiyo ambao unafikia mwisho wake tarehe 31 mwezi Desemba.

  1. Jeshi la Israel laanzisha operesheni kubwa Ukingo wa Magharibi.Chanzo cha picha,EPATakriban Wapalestina 11 wameuawa na wanajeshi wa Israel kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, maafisa wa afya wa Palestina wanasema.Watano waliripotiwa kuuawa katika shambulizi la anga katika kambi ya wakimbizi ya al-Far’a, na sita katika shambulio la ndege zisizo na rubani huku mapigano yenye kuhusisha silaha yakiendelea huko Jenin.Vikosi vya usalama vya Israel vilisema vinafanya “operesheni ya kukabiliana na ugaidi ” huko Jenin na Tulkarm.Hii inaonekana kuwa operesheni kubwa ya Israeli, na takriban miji minne ya Palestina inalengwa kwa wakati mmoja – Jenin, Tulkarm, Nablus na Tubas.Ripoti za Wapalestina zinasema kuwa, barabara kuu za kuelekea Jenin zimefungwa kutokana na mapigano yenye kuhusisha silaha katika kambi ya wakimbizi ya mji huo.Shambulio la anga la Israel linasemekana kulenga gari katika kijiji jirani saa za alfajiri.Wanajeshi wa Israel wanasemekana kuingia katika hospitali moja huko Jenin na kuwazuia watu wawili huko Tulkarm.Uvamizi wa kijeshi wa Israel huko Nablus unaripotiwa kulenga kambi mbili za wakimbizi huko.Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz alisema kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) “limekuwa likifanya kazi kwa nguvu zote tangu jana usiku katika kambi za wakimbizi za Jenin na Tulkarm ili kubomoa miundo mbinu ya kigaidi ya Iran na makundi ya Kiislamu iliyoanzishwa huko”.Aliishutumu Iran, ambayo inaunga mkono kundi la Jihad la Palestina na Hamas, kwa kutaka kufungua kile alichokiita “mapigano ya pili” dhidi ya Israel katika Ukingo wa Magharibi.Soma zaidi:Waziri wa Israel azua mgogoro kwa kupendekeza ujenzi wa sinagogi katika msikiti wa al-AqsaJe, Hezbollah ina uwezo gani wa kijeshi na inaweza kuanzisha vita vikubwa dhidi ya Israel?LIsrael na Hezbollah zakabiliana katika mapigano makaliMshirikishe mwenzako, Jeshi la Israel laanzisha operesheni kubwa Ukingo wa Magharibi
  2. Namibia yazuia meli inayoshukiwa kubeba shehena ya jeshi la Israel.Chanzo cha picha,ReutersMeli inayoshukiwa na mamlaka ya Namibia kubeba shehena ya kijeshi iliyokusudiwa kutumiwa katika vita vinavyoendelea Gaza imezuiwa kutia nanga katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.Waziri wa Sheria wa Namibia Yvonne Dausab aliviambia vyombo vya habari vya serikali kuwa meli hiyo ilisimamishwa kwa sababu ilikuwa na “vifaa vyenye vilipuzi vinavyopelekwa Israel”.Meli ya MV Kathrin, ambayo ilianza safari kutoka Vietnam, ilikuwa imeomba ruhusa ya kutia nanga katika bandari ya Walvis Bay – kabla ya kuelekea kaskazini, kwenye njia inayoshukiwa kuelekea Mediterania kupitia Mlango Bahari wa Gibraltar.Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalikuwa yameonya kwamba Namibia ingeweza kuhusishwa na ukiukaji wa haki za binadamu kama ingeruhusu meli hiyo kutia nanga.Haijulikani ni kwa nini meli hiyo ilitaka kutia nanga, lakini vyombo vinavyosafiri kwa muda mrefu huwa vinasimama ili kupata mahitaji wanayohitaji kwa kipindi hicho, kupumzika, kupakua au kubeba mizigo.Desemba mwaka jana, jirani na mshirika wa Namibia, Afrika Kusini walifungua kesi inayoendelea katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ikidai Israel inafanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.Israel imekanusha madai ya mauaji ya halaiki na kusema kuwa “hayana msingi”.Mzozo huo ulianza baada ya Hamas kuanzisha shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa kwa Israel tarehe 7 Oktoba, ambapo takriban watu 1,200 waliuawa na wengine 251 kuchukuliwa mateka.Jeshi la Israel kisha lilianzisha kampeni ya kumaliza kundi la Hamas na zaidi ya watu 40,430 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.Soma zaidi:Vita vya Gaza: Israeli hupata wapi silaha zake?Israel na Hezbollah zakabiliana katika mapigano makaliVita vya Gaza: Je, uwepo wa jeshi la Israel katika eneo la Philadelphi ni mafanikio kwa Netanyahu?Mshirikishe mwenzako, Namibia yazuia meli inayoshukiwa kubeba shehena ya jeshi la Israel
  3. Afrika kusubiri kwa muda mrefu kupata chanjo ya mpox.Chanzo cha picha,ReutersNchi za Afrika ambazo zimeathirika na mpox zitalazimika kusubiri muda mrefu zaidi kupata chanjo hiyo.Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, Afrika CDC, vinasema imeweka mpango wa bara hili kukabiliana na ugonjwa huo ili upata chanjo mwezi Septemba.“Tunataka kuweka juhudi zetu zote sehemu moja. Afrika itakuwa na mpango mmoja wa kukabiliana na mpox na bajeti moja. Tunataka kuimarisha uwezo wa nchi kutumia chanjo hizo zitakapopatikana,” Dk. Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Afrika CDC alisema.Hata hivyo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kitovu cha mlipuko huo, haitapokea michango iliyoahidiwa ambayo ilitarajiwa wiki hii.Nigeria ilipokea dozi 10,000 za chanjo ya Bavarian Nordic, Jumanne -msaada kutoka Marekani.Nchi hiyo ilikuwa imeanza mchakato wa kupata chanjo hizo hata kabla ya mpox kutangazwa kuwa dharura ya kiafya duniani.Vikwazo vya udhibiti na changamoto za manunuzi zimesababisha kuchelewa huko.Afrika pia inataka kupata chanjo zake kama bara na sio kama nchi moja moja.Soma zaidi:Homa ya Nyani: Tofauti tano kati ya Mpox na Uviko 19Je, tunapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu Homa ya Nyani?Mshirikishe mwenzako, Afrika kusubiri kwa muda mrefu kupata chanjo ya mpox
  4. Waendesha mashtaka waomba adhabu ya kifo kwa watuhumiwa wa “jaribio la mapinduzi” DRC.Chanzo cha picha,AFPWaendesha mashtaka wa umma katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wameomba watu 50 wapewe adhabu ya kifo kwa kufanya kile ambacho jeshi linakiita “jaribio la mapinduzi” lililotokea mnamo mwezi Mei.Mwendesha Mashtaka wa Kijeshi Luteni Kanali Innocent Radjabu alitoa wito huo wakati wa kusikilizwa kwa kesi katika mahakama ya kijeshi ya Kinshasa.Hata hivyo alimtaka hakimu kumuepusha mshtakiwa mmoja kutokana na adhabu ya kifo, akisisitiza kwamba ana matatizo ya kisaikolojia.Miongoni mwa washtakiwa wanaokabiliwa na hukumu ya kifo ni Wamarekani watatu.Mnamo 19, Mei walikuwa sehemu ya kundi lililojihami ambalo lilishambulia nyumba ya aliyekuwa Waziri wa Uchumi Vitale kamerhe, ambaye sasa anahudumu kama mkuu wa Bunge la Kitaifa.Pia walivamia ofisi ya rais wa nchi hiyo.Tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo Juni 7, washtakiwa hao wamekuwa wakikabiliwa na mashtaka kuanzia “mashambulizi, ugaidi, kumiliki silaha kinyume cha sheria na zana za kivita, kujaribu kuua, kuua,” miongoni mwa mengine.Upande wa utetezi unatarajiwa kuwasilisha kesi yake siku ya Ijumaa.Mwezi Machi, serikali ya DRC ilirejesha hukumu ya kifo, na hivyo kusababisha ukosoaji kutoka kwa makundi ya kutetea haki za binadamu.Soma zaidi:‘Mungu ndiye aliyetuma majeshi yake ya mbinguni ili kutuokoa na kifo’ – Mke wa Vital KamerheMwanamume aliyehusika na jaribio la mapinduzi DRC ni nani?Mshirikishe mwenzako, Waendesha mashtaka waomba adhabu ya kifo kwa watuhumiwa wa “jaribio la mapinduzi” DRC
  5. Meli iliyoshambuliwa na Wahouthi huenda inavuja mafuta – Marekani.Chanzo cha picha,ReutersMeli ya mafuta iliyoshambuliwa na waasi wa Houthi wa Yemen katika Bahari ya Shamu wiki iliyopita bado inawaka moto na huenda iwaka inavuja mafuta, ikulu ya ya Marekani inasema.Majaribio ya kunusuru meli ya MV Sounion inayomilikiwa na Ugiriki yamezuiwa na Wahouthi, ambao wametishia mashambulizi zaidi, Pentagon inaongeza.Meli hiyo imebeba zaidi ya tani 150,000 – au mapipa milioni moja – ya mafuta ghafi, na kuna uwezekano ikawa na uvujaji mkubwa kuwahi kushuhudiwa miongoni mwa meli katika historia iliyorekodiwa.Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya Yemen, wanasema wamekuwa wakishambulia meli katika Bahari ya Shamu kwa muda wa miezi 10 kuunga mkono Wapalestina katika vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.Wameripotiwa kuzamisha meli mbili na kuua takriban wafanyikazi wawili.Mara nyingi wamedai kwamba wanalenga meli zenye kuhusishwa tu na Israeli, Marekani au Uingereza.Meli ya Sounion ilishambuliwa kwa mara ya kwanza na milio ya risasi kutoka kwa boti mbili ndogo Jumatano iliyopita, kisha ikarushiwa makombora matatu ambayo hayakujulikana ni ya aina gani, yalisababisha moto na kuiacha bila nguvu ya injini, ofisi ya Operesheni ya Biashara ya Bahari ya Uingereza ilisema.Wafanyakazi wake 25 waliokolewa na meli ya kivita ya Ulaya siku moja baadaye na kupelekwa Djibouti.Meli hiyo ya mafuta ilishambuliwa tena – Wahouthi walichapisha video inayodaiwa kuwaonyesha wakiichoma moto.Soma zaidi:Meli ya mafuta yawaka moto baada ya shambulio la kombora la Houthi‘Utajiri wa mafuta waifanya nchi hii kujihisi kuwa na hatia’Mshirikishe mwenzako, Meli iliyoshambuliwa na Wahouthi huenda inavuja mafuta – Marekani

TheHeartBeatofAfrica

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024

Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment