Vunja urafiki na marafiki wabaya.

Bwana YESU KRISTO atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU.
Leo tunaangalia baadhi ya marafiki wabaya ili tuvunje urafiki nao.

Nini maana ya neno “Rafiki”?

Rafiki ni mwanaume au mwanamke unayeaminiana naye na mnashirikiana katika mambo mengi.

Najua Sana wako marafiki wema na wazuri Sana lakini ni muhimu pia kujua kwamba hata marafiki wabaya wapo.

Mithali 18:24 “Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.”

Sasa ni vizuri kutambua kwamba sio marafiki zako wote ni marafiki wazuri kwako, nitakufafanulia ndani ya somo hili la leo.

Nasema tena sio marafiki zako wote ni marafiki wazuri kwako, chunguza ndugu ili ubaki na marafiki wema tu.

Baadhi ya sifa za marafiki wabaya kwako na ambao hawakufai ni hizi.

  1. Rafiki yako anayekushawishi kutenda mabaya.

Kumbu 13:6 “Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;”

Rafiki anaweza kuwa hata ndugu yako au mzazi wako ndio maana unaweza kukuta kwenye familia mtoto humweleza Siri Mama na sio Baba kwa sababu tu kwake mama ni mama na rafiki, kumbuka hakuna urafiki bila kuaminiana hivyo hata katika kundi la ndugu zako Kuna mmoja ni ndugu na rafiki yako maana ndiye unayemwamini, huyo ni rafiki yako.

Sasa haijalishi una rafiki katika ndugu zako, wazazi wako, ukoo wako, familia yenu, mtaa wenu au kazini kwako lakini rafiki yako wa namna yeyote anayekushawishi kutenda mabaya yaani kufanya dhambi na machukizo huyo ni rafiki mbaya sana kwako.

Kuna watu wameshauriwa na ndugu zao au marafiki zao kwenda kwa waganga wa kienyeji, hao ni marafiki wabaya Sana.

Rafiki anayekushawishi umwache YESU KRISTO huyo ni rafiki mbaya sana.
Rafiki yeyote anayekushawishi kufanya Jambo lolote baya huyo ni rafiki mbaya kwako, vunja urafiki na rafiki mbaya.

  1. Rafiki wa wakati wa raha tu hakufai.

Mithali 14:20 “Maskini huchukiwa hata na jirani yake; Bali tajiri ana rafiki wengi.”

Rafiki wa wakati wa raha tu huyo hakufai, ikitokea shida rafiki yako anakukimbia, huyo hakufai.

Inawezekana uko vizuri kiuchumi ndio maana una marafiki wengi Sana, ndugu rafiki wa wakati wa raha tu hakufai.

Kuna mtu zamani alikuwa na cheo na kazi nzuri ndio maana alikuwa na marafiki wengi Sana lakini alipoondolewa kazini kwa Sasa hana rafiki hata mmoja, hiyo inaonyesha kwamba hakuwa na marafiki wazuri.

Ukiona rafiki yako ukipatwa na changamoto anakukimbia kisha ukikaa vizuri kiuchumi anarudi, huyo sio rafiki mzuri kwako Bali ni rafiki mbaya kwako, vunja mapema urafiki na rafiki wa namna hiyo.

Kuna watu akiumwa marafiki zake wote wanamkimbia lakini akiwa mzima na ana pesa wanarudi, ndugu Kama una marafiki wa namna hiyo vunja urafiki Leo na watu hao.

Kwanini ubaki na marafiki ambao ukiwa matatizoni au huna pesa unaonekana kwao Kama kitu Cha kutisha?
Zaburi 31:11 “Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Walioniona njiani walinikimbia.”

Rafiki ambaye ukiwa katika matatizo hakutaki lakini ukiwa katika raha anataka awe rafiki yako, huyo ni rafiki mbaya kwako, hakufai.

  1. Usikubali kuwa rafiki wa wapumbavu.

Mithali 13:20 “Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.”

Kuna marafiki wapumbavu, ukifanya urafiki nao ujue na wewe baaada ya siku chache utakuwa mpumbavu.

Mpumbavu ni mtu asiyemcha MUNGU.

Mpumbavu ni mtu anayejua Jambo fulani ni dhambi ila analitenda.

Mpumbavu ni mtu ambaye anajua MUNGU yupo lakini anatangaza MUNGU hayupo na hata akifanya dhambi anadhani MUNGU hatamuona.

Ndugu, usiwe na urafiki na watu wapumbavu.

Usiwe na urafiki na watu wanaomkataa YESU KRISTO kuwa Mwokozi wao.

Usikubali kuwa rafiki wa wapumbavu ili na wewe usije ukawa mpumbavu.

Ukiwa rafiki wa wapumbavu tarajia kupata madhara hivyo vunja urafiki na Mtu mpumbavu.

Vunja urafiki na rafiki mzinzi na mwasherati.

Vunja urafiki na rafiki muongo na tapeli.

Vunja urafiki na rafiki mtenda dhambi.

Vunja urafiki na rafiki anayekushawishi kutenda mabaya.

Vunja urafiki na rafiki mzushi na mpenda umbeya.

Vunja urafiki na rafiki mchawi.

Nakushauri ambatana tu na marafiki wema, wacha MUNGU,waliokoka na ni vielelezo vyema katika kuishi maisha matakatifu ya Wokovu wa KRISTO YESU.

Hakikisha rafiki yako ana YESU KRISTO na ana hofu ya MUNGU ndani yake.

Ndugu, Mche MUNGU katika KRISTO YESU Mwokozi na utaitwa heri.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.

Bwana YESU Amekaribia Kurudi.

Je, Umejiandaaje?

Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?

Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.



CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com

cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!

Copyrights Reserved @2019 FortuneBaraka Entertainments.




Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment