Afrika Leo Mchana -Habari Kamili Agosti 26,2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

FAMILIA za maafisa wa polisi wa Kenya waliotumwa Haiti zimelalamika kwamba bado hazijalipwa tangu walipoanza oparesheni ya kudumisha amani nchini humo.

Haya yamejiri miezi miwili baada ya Balozi wa Amerika Antony Blinken kuagiza kutolewa kwa Sh14.1 bilioni kufadhili oparesheni hiyo iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa (UN).

Fedha hizo vilevile zinadhamiriwa kununua vifaa vya kijeshi kwenye handaki zilizopo katika jiji kuu la Port-au-Prince, ambapo polisi wa Kenya wanafanyia shughuli zao.

Katika mahojiano na jamaa wa familia kadhaa za polisi wa Kenya waliochelea kutajwa wakihofia unyanyapaa, walisimulia masaibu ya kifedha kutokana na kucheleweshewa malipo.

Wengine walilalamika kuwa, huku shule zikifunguliwa Jumatatu, Agosti 26, 2024 hawana uwezo wa kulipa karo na kuwanunulia watoto wao vifaa vinavyohitajika kwa muhula wa tatu wakati mitihani ya kitaifa inatarajiwa kuanza.

“Shule zinafunguliwa na kila mara ninapowasiliana naye, ninachopata tu ni, bado hatujalipwa,” alisema jamaa mmoja wa familia.

Alishangaa ni nini mume wake anafanya Haiti ilhali hawezi kugharamia mahitaji licha ya kuhakikishiwa wangepata malipo ya ziada.

Jamaa wa afisa mwingine wa polisi alisema watoto wake huenda wakakosa kurejea shule ikiwa hawatalipwa fedha hizo.

“Kusema kweli tuna tatizo hapa kwa sababu hata kugharamikia chakula na mahitaji mengineyo kumeanza kuwa changamoto,” zilisema dumu. Radio Fortune Africa imethibitisha tatizo hilo na baadhi ya maafisa wa polisi walio Haiti ambao, hata hivyo, hawakutaka kulijadili kwa kina na badala yake kutuelekeza kwa familia zao Kenya.

Kikosi cha kwanza cha polisi wa Kenya kiliwasili Haiti Juni 25, 2024 baada ya kupokezwa bendera ya Kenya siku iliyotangulia na Rais William Ruto.

Kikosi cha pili kilitumwa Julai 16, 2024 na kuongeza idadi hiyo kuwa 394 lakini bado hawajatimia maafisa 1,000 waliopangiwa kutumwa.

Maafisa hao wanajumuisha kikosi cha kukabiliana na ghasia (GSU), Kikosi Maalum na Kikosi cha Kupiga Doria Mpakani (BPU).

Tulipowasiliana naye kuhusu malalamishi hayo, Kaimu Inspekta Jenerali Mkuu wa Polisi, Gilbert Masengeli alisema “maafisa watapata malipo yao kwa wakati.”

Katibu katika Wizara ya Masuala ya Kigeni, Korir Sing’oei na Mshauri wa rais kuhusu Usalama wa Kitaifa, Monicah Juma, hawakujibu maswali yetu.

Wiki iliyopita, kundi linalofahamika kama Caribbean Community (CARICOM) lilitoa taarifa likisema oparesheni hiyo inagubikwa na changamoto tele ikiwemo upungufu wa vifaa, uhaba wa fedha na kuchelewesha kubuni taasisi za serikali.

Timu hiyo ilialikwa na Mkuu wa Baraza la Rais kuhusu Mageuzi Haiti, Leslie Voltaire.

Katika mikutano hiyo iliyofanyika kati ya Agosti 11 na 16 na Waziri Mkuu wa Haiti, Garry Conille, timu hiyo iliorodhesha changamoto zinazokabili Polisi wa Haiti (HNP) na vikosi vya polisi wa Kenya.

Rais Ruto wa Kenya aagiza NYS kupata mafunzo ya Bunduki.

Rais William Ruto aagiza matumizi ya bunduki yashirikishwe kwenye mafunzo ya Shirika la Vijana la Huduma kwa Taifa (NYS); asema yatasaidia maafisa hao kulinda taifa watakapohitajika.

TANGAZO la kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa anapanga kuachana na siasa za humu nchini ili kutekeleza majukumu katika asasi kuu ya Umoja wa Afrika (AU) limechochea mvutano kuhusu urithi wa uongozi ndani ya ODM

Bw Odinga alitoa tangazo hilo kwenye kikao na wanahabari wiki jana jijini  Nairobi akiwa ameandamana na Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi.

Aliweka wazi kwamba sasa ataelekeza juhudi zake katika kampeni za kuwania cheo cha mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

“Kuanzia sasa sitajihusisha zaidi na siasa za Kenya kwani nitalenga zaidi kampeni katika mataifa yote barani Afrika. Hii ni awamu ya mpito kutoka kuzamia siasa za Kenya na kuingia katika siasa za bara la Afrika,” Bw Odinga akawaambia wanahabari katika afisi ya Bw Mudavadi.

“Nitaanza kuhudumia bara la Afrika nikichaguliwa na hiyo itakuwa Februari mwaka ujao,” akaongeza.

Gavana wa Siaya James Orengo, ambaye ni mwanasiasa mkongwe na mwana mapinduzi ni miongoni mwa wale ambao majina yao yametajwa kama wanaoweza kumrithi Bw Odinga.

Duru katika chama hicho zilisema kuwa Bw Orengo anaungwa mkono na magavana wenzake kutoka Nyanza na eneo la Magharibi.

Gavana wa Kisumu Profesa Peter Anyang’ Nyong’o ambaye anahudumu muhula wake wa mwisho pia anasema kuwa ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu kurithi kiti cha Bw Odinga.

Idadi kubwa ya wafuasi wa ODM wanatoka Luo Nyanza hali inayowafanya wengine kuamini kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa kiongozi atakayechukua nafasi ya Bw Odinga atatoa eneo hilo.

Bw Orengo amekuwa mwaminifu kwa Bw Odinga tangu kifo cha babake Jaramogi Oginga Odinga.

Gavana huyo ambaye ni wakili maarufu anajivunia sifa kama mwanasiasa jasiri  ambaye amedumu katika siasa za upinzani kwa miaka.

Yeye na Bw Odinga walianza kutembea pamoja kisiasa mwishoni mwa miaka ya 80 na 90  wakati ambapo walikuwa miongoni mwa wanasiasa wachanga waliopigania ukombozi wa pili.

Bw Orengo ni miongoni mwa viongozi wakuu wa ODM ambao Bw Odinga aliwaacha nje alipojaza nafasi kuu chamani zilizoachwa wazi na wale walioteuliwa mawaziri.

Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kitaifa kuchukua mahala pa John Mbadi aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.

Gavana wa Mombasa Abdullswamad Nassir, mwenzake wa Kisii Simba Arati na Seneta wa Godfrey Osotsi waliidhinishwa na Kamati Kuu ya ODM kuwa manaibu kiongozi wa chama.

Watatu hao walichukua nafasi iliyosalia wazi kufuatia kuteuliwa kwa Ali Hassan Joho na Wycliffe Oparanya kuwa mawaziri wa Madini na Ustawi wa Vyama vya Ushirika, mtawalia.

Mnamo Jumapili Bi Wanga aliambia Taifa Leo kwamba ni mapema kwa mjadala kuhusu ni nani atachukua wadhifa wa kiongozi wa chama kuanza.

Alisema wanaomezea mate kiti hicho wasubiri hadi Bw Odinga atakapotwaa cheo cha mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.

NAIBU Rais Rigathi Gachagua ametaja mashindano ya kisiasa yanayogubika Mlima Kenya kama yaliyo kati ya viongozi wanaopigania maslahi ya jamii na wasaliti.

Kauli hii huenda ikawakasirisha wakosoaji wake hasa wanaoegemea mrengo wa Rais William Ruto.

Bw Gachagua amewapa makataa ya hadi Disemba 31, viongozi wa kimaeneo ambao “hawasikizi raia” (akirejelea wakosoaji wake) kubadilisha mkondo la sivyo watajipata mashakani katika Uchaguzi Mkuu 2027.

“Mimi ni mtu ninayezunguka vijijini nikisikiza raia. Naweza kuwahakikishia kuwa wapigakura tayari wamefanya maamuzi makuu 2027 na ninahofia baada ya muda wa makataa hayo kukamilika, mtaachwa nyuma,” alisema Naibu Rais katika Kaunti ya Kiambu, Agosti 17.

Huku akiwa na wabunge na magavana wapatao 20 pekee kutoka Mlima Kenya wanaomuunga mkono, Bw Gachagua amekiri kambi yake ni ya walio wachache, kwa sasa, lakini akasisitiza kuwa: “Ni heri niwe na wanajeshi wachache ninaoweza kutegemea kuliko kuwa miongoni mwa vigeugeu.”

Huku akiimarisha kampeni yake inayolenga kuunganisha Mlima Kenya kwa kutuliza hali ya kutoridhishwa eneo hilo, matukio ya hivi majuzi kisiasa ukiwemo ukuruba wa Rais Ruto na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, Naibu Rais anageuza mkondo hatua baada ya nyingine.

Kwa wachanganuzi wengi wa siasa, Bw Gachagua anapolalamika kuhusu mahasimu wake kutoka Eneo la Kati, jina linalowajia mara moja ni Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro – anayeambatana na Rais katika ziara zake nyingi.

Bw Nyoro wikendi alikuwa katika hafla za kumkaribisha mwandani wa Bw Odinga aliyeteuliwa majuzi katika Baraza la Mawaziri, Wycliffe Oparanya.

Katika siku za hivi karibuni, Mbunge wa Laikipia Mashariki, Mwangi Kiunjuri, amegeuka taswira ya kumpinga Naibu Rais Mlima Kenya, huku majibizano kati ya wawili hao yakigeuka upesi mashambulizi ya kibinafsi.

Wawili hao wametumia maneno ya kudhalilishana kiasi kwamba wazee wametangaza mipango ya kuwapatanisha.

“Tungependa viongozi hawa wawili wawe marafiki. Kuna mambo fulani wanayorushiana ambayo yanakiuka kanuni zetu kama jamii. Inaweza kutokea tu ikiwa heshima kati yao imesambaratika. Tutajenga upya heshima hizo,” alisema Mzee wa Baraza la Jamii ya Agikuyu, Wachira Kiago.

Bw Kiunjuri amechukua usukani wa kumshambulia Bw Gachagua alipoachia Kiongozi wa Wengi Bungeni, Kimani Ichung’wa akisema Naibu Rais anataka kusakama mustakabali wa eneo hilo kisiasa.

Mtazamo huu umekita katika chama United Democratic Alliance (UDA) ya Rais huku Katibu Mkuu wa chama hicho, Hassan Omar, akimshutumu Bw Gachagua kwa kujaribu kujipatia cheo cha mlinzi wa eneo hilo.

“Rais na wafuasi wake hatatishwa na mtu aliyejipandisha cheo kama mlinzi. Hakuna mtu atakayeshikilia funguo za eneo lolote ifikapo 2027 kwa sababu Wakenya wamekata kauli kuwa wanataka mitazamo ya kitaifa kufanikisha serikali za siku za usoni,” alisema Bw Omar, akitetea mkutano wa Rais Ruto uliofanyika ikulu na viongozi kutoka Mlima Kenya ambapo Naibu Rais hakuwepo.

Hassan Omar
mlima kenya
mwangi kiunjuri
Naibu Rais Rigathi Gachagua
Omba msamaha
Rais William Ruto
uda

MWANAFUNZI Mkenya, anayesomea nchini Algeria amehukumiwa kifungo cha miezi miwili gerezani licha ya tuhuma za kudungwa kisu na mwenzake mwenzake akauguza majeraha mabaya.

Duru zinaarifu, Mkenya huyo alidungwa kwa kisu na Mpalestina akiwa katika chumba cha malazi na inashangaza kuona kesi iligeuzwa akawekelewa makosa.

Ian Koima Kiprotich, 24, anayesomea Shahada ya Uzamili ya Usanifu katika Chuo Kikuu cha Constantine 3, alihukumiwa mnamo Jumanne, Agosti 20, 2024 na mahakama ya Algeria katika kesi ambayo hakuwakilishwa na wakili yeyote.

Hata hivyo, wanafunzi wa Kenya nchini Algeria, wamelaani hukumu hiyo wakisema Kiprotich alinyimwa haki, na wanataka ukweli ufanyike kwa mwenzao.

Kulingana na mwanafunzi mmoja Mkenya ambaye aliomba tulibane jina lake, wawili hao waligombana na Kiprotich alidungwa kisu mara tano.

Alikimbizwa katika Hospitali ya Centre-Universitaire de Constantine akiwa katika hali mbaya na kulazwa kwa siku tatu chini ya uangalizi maalum.

Lakini aliporuhusiwa kutoka hospitalini, Kiprotich alishtuka kukamatwa na kushtakiwa kwa “kumshambulia” mwanafunzi wa Kipalestina na kuitusi familia yake.

“Alidungwa kisu mara kadhaa shingoni, pajani na tumboni na mwanafunzi Mpalestina na mara akaanguka chini huku akivuja damu nyingi na kupoteza fahamu,” alisema mwanafunzi huyo Mkenya.

Wanafunzi hao walisema wanafunzi watatu kutoka Malawi, Uganda na Tanzania walioshuhudia zogo hilo, walifika kumuokoa na kumkimbiza hospitalini.

“Nashukuru Mungu kwamba maisha ya mwenzetu yaliokolewa na wanafunzi hawa watatu. Alikuwa akivuja damu nyingi kama ilivyothibitishwa na damu iliyotapakaa chumbani mwake,” mwanafunzi huyo Mkenya aliongeza.

Kiprotich hakuweza kumudu wakili wa kibinafsi na aliomba wakili wa umma, lakini juhudi zake za kumpata ziliambulia patupu.

Cha kushangaza ni kwamba, aliyemshtaki alipewa wakili wa umma mara moja kumwakilisha mahakamani, huku Kiprotich akipewa mkalimani shughuli za mahakama zilipokuwa zikiendeshwa kwa Kiarabu.

Mkalimani ni mtafsiri wa lugha.

“Kiprotich alinyimwa haki. Alikuwa na mashahidi watatu tayari kutoa ushahidi. Alinyimwa kesi ya haki kwa sababu hakuwa na muda wa kutosha na uwakilishi wa kisheria kuandaa utetezi wake,” alidokeza mwanafunzi huyo.

Aliongeza, “Mashahidi walikuwa tayari kutoa ushahidi kwamba Kiprotich alikuwa chumbani mwake wakati wa shambulio hilo. Lakini walitishiwa na mshambuliaji.”

Mwanafunzi mwingine wa Kenya, ambaye hakutaka jina lake litajwe pia, alisema shambulio hilo halikuchochewa.

“Kiprotich alikuwa chumbani mwake. Haikuwa vita. Kiprotich amenyimwa haki. Aliyemshtaki ana historia ya utovu wa nidhamu”.

Mwanafunzi mwingine alidai kuwa wakati fulani wa kesi hiyo, vita vya Israel dhidi ya Gaza vilitajwa, huku wakili anayemwakilisha mwanafunzi huyo wa Kipalestina akisema kuwa Algeria inapaswa kutetea Wapalestina wanaoteseka katika vita vya Gaza.

algeria
Dungwa kwa kisu
Kukosa haki
MKENYA
Mpalestina
mzozo

KWINGINEKO DUNIANI

Muhtasari

  • 22 wauawa baada ya vitambulisho vyao kukaguliwa Pakistan
  • Urusi yafanya shambulizi la ndege zisizo na rubani kwenye mji mkuu wa Ukraine
  • Australia: Sheria ya kutowaadhibu wanaokataa kupokea simu baada ya kazi yaanza kutekelezwa
  • Kenya: Miungano ya kutetea maslahi ya walimu yatofautiana kuhusu mgomo
  • Mwanamume mzee zaidi duniani: ‘Sina siri ya kipekee ya kuishi miaka mingi’
  • Mkurugenzi Mtendaji aliyekamatwa hana ‘chochote cha kuficha’ – Telegram
  • Muingereza auawa katika shambulizi la kombora nchini Ukraine

Moja kwa Zaidi ya makombora 100 na droni zilitumika katika mashambulizi – ZelenskyZelenskyChanzo cha picha,EPARais wa Ukraine Volodymr Zelensky amesema hivi punde kuwa zaidi ya makombora 100 na takribani ndege 100 za mashambulizi zilirushwa na Urusi usiku kucha.Anasema kuwa lengo kuu lilikuwa “miundombinu muhimu ya kiraia” katika mikoa mingi ya Ukraine, akitoa mfano wa mashambulizi dhidi ya Kharkiv, Kyiv, Odesa na maeneo ya magharibi.Katika chapisho kwenye Telegram, Zelensky anaongeza kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa vifaa vya nishati, lakini anasema kazi ya ukarabati inaendelea na wafanyakazi “watafanya kazi ya ukarabati saa nzima”.Anaendelea kutoa wito kwa washirika wa Magharibi kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu na kuwaruhusu kupiga maeneo nchini Urusi ambayo mashambulizi yanaanzishwa.Unaweza kusoma;Vita vya Ukraine: ‘Hakuna kusalimisha eneo lolote la Ukraine kwa Putin’- ZelenskyJe, ndege za kivita za Marekani F-16 zitasaidia Ukraine kuishinda Urusi?Mshirikishe mwenzako, Zaidi ya makombora 100 na droni zilitumika katika mashambulizi – ZeleWatatu wauawa wakati Urusi ikifanya mashambulizi makubwa ya anga kote UkraineHuduma za dharura za Ukraine zinatafuta vifusi vya jengo lililolengwa katika siku za hivi majuziChanzo cha picha,ReutersTunaweza kukuletea habari za hivi punde asubuhi ya leo wakati Urusi ikifanya mashambulizi makubwa ya anga dhidi ya Ukraine.Msururu wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora yalianza kote nchini usiku wa Jumatatu.Milipuko ilitanda katika miji kadhaa katika mikoa 15 kulingana na Waziri Mkuu wa Ukraine Maafisa wa mkoa wanasema takribani watu watatu wameuawa nchi nzima iko chini ya tahadhari ya uvamizi wa anga.Tumeshuhudia kukatika kwa umeme huku mashambulizi ya Urusi yakilenga miundombinu ya nishati na maji.Wakazi wa Kyiv wanatafuta makazi katika vituo vya treni .Jirani wa Ukraine, Poland, anasema kuwa jeshi lake la anga limeanzishwa kwa sababu mashambulizi yamekaribia anga ya Poland.Tunasikia kwamba Ukraine imekabiliana na mashambulizi ya ndege yake isiyo na rubani lakini kwa kiwango kidogo zaidi.Mshirikishe mwenzako, Watatu wauawa wakati Urusi ikifanya mashambulizi makubwa ya anga kote Ukraine

  1. 22 wauawa baada ya vitambulisho vyao kukaguliwa Pakistan.Watu wenye silaha wamewaua takriban watu 22 kusini-magharibi mwa Pakistan baada ya kuwatoa kwenye magari yao kwa nguvu na kuangalia utambulisho wao, maafisa wanasema.Shambulio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo kwenye barabara kuu ya mkoa wa Balochistan, ambapo vikosi vya usalama vinapambana na ghasia za kidini, kikabila na wanaotaka kujitenga.Watu hao waliokuwa na silaha walikagua hati za utambulisho, wakiripotiwa kuwatenga wale kutoka Punjab ili wapigwe risasi, kabla ya kuwasha moto magari, maafisa walidai.Kundi la wapiganaji wa Baloch Liberation Army (BLA) limedai kuhusika na mashambulizi hayo katika wilaya ya Musa Khel.”Idadi ya wanamgambo hao ilikuwa kati ya 30 hadi 40. Walisimamisha magari 22,” alisema Najibullah Kakar, afisa mkuu wa eneo hilo, ameliambia shirika la habari la AFP.”Magari yaliyokuwa yakisafiri kwenda na kurudi Punjab yalikaguliwa, na watu kutoka Punjab walitambuliwa na kupigwa risasi.”BLA imesema ilikuwa inalenga wanajeshi wanaosafiri wakiwa wamevalia kiraia, kulingana na shirika la habari la Reuters.Waziri Mkuu Shehbaz Sharif “alihuzunishwa sana” na tukio hilo na “kulaani shambulio hilo la kigaidi” katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake.Balochistan ni jimbo kubwa zaidi la Pakistani lakini, ingawa lina rasilimali nyingi kuliko majimbo mengine, ndilo lenye maendeleo duni.Mshirikishe mwenzako, 22 wauawa baada ya vitambulisho vyao kukaguliwa Pakistan
  2. Urusi yafanya shambulizi la ndege zisizo na rubani kwenye mji mkuu wa Ukraine.Chanzo cha picha,ReutersUkraine na Urusi zilikabiliana kwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani Jumatatu asubuhi.Serhiy Popko, mkuu wa utawala wa kijeshi huko Kyiv, alisema kwenye jukwa la Telegram kwamba hadi ndege zisizo na rubani 10 ziliharibiwa zilipokaribia mji, katika eneo karibu na Kyiv.Utawala wa kijeshi katika eneo la mji mkuu ulieleza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine katika eneo hilo ilishiriki katika kuzima shambulio hilo, baada ya “kugundua mienendo ya ndege zisizo na rubani za adui.”Walioshuhudia waliripoti kusikia milipuko karibu na Kyiv siku ya Jumatatu wakati mifumo ya ulinzi ya anga ya Ukraine ikionekana kuzima shambulio la angani, Reuters iliripoti.Kwa upande wa Urusi, Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilisema Jumatatu kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ya Urusi iliharibu ndege 20 zisizo na rubani zilizorushwa na Ukraine dhidi ya nchi hiyo usiku kucha.Ndege tisa zisizo na rubani ziliharibiwa katika eneo la Saratov, tatu katika eneo la Kursk, na mbili katika maeneo ya Belgorod, Bryansk na Tula, wizara hiyo ilisema kwenye mtandao wa Telegram.Pia unaweza kusoma:Reuters: Urusi na Ukraine kubadilishana wafungwa siku ya Jumamosi – watu 115 kila upandeUkraine yaendelea kusonga mbele ndani ya eneo la UrusiUrusi: Hali katika eneo la Belgorod ‘ni tete’, – GavanaUrusi lazima ilazimishwe kuleta amani – ZelenskyPutin: ‘Lazima tumfukuze adui nje ya eneo letuWanajeshi wa Ukraine wapo kilomita 30 ndani ya eneo la UrusiKwa nini Ukraine imeanzisha mashambulizi ya mpakani dhidi ya Urusi?Mshirikishe mwenzako, Urusi yafanya shambulizi la ndege zisizo na rubani kwenye mji mAustralia: Sheria ya kutowaadhibu wanaokataa kupokea simu baada ya kazi yaanza kutekelezwa.Chanzo cha picha,Getty ImagesNchini Australia, sheria ya kutowaadhibu wafanyakazi wanaokataa kupokea simu baada ya saa za kazi kumalizika imeanza kutekelezwa.Hatua hii imetoa fursa kwa watu wanaohisi kulazimishwa kupokea simu au kusoma ujumbe kutoka kwa waajiri wao baada ya kumaliza kazi ya siku.Sheria hiyo mpya inaruhusu wafanyikazi kupuuza mawasiliano baada ya saa za kazi ikiwa wataamua kufanya hivyo, bila kuogopa kuadhibiwa na wakubwa wao.Zaidi ya nchi 20, haswa za Ulaya na Amerika Kusini, zina sheria sawa na hiyo.Sheria hiyo haikatazi waajiri kuwasiliana na wafanyikazi baada ya saa za kazi, badala yake, inawapa wafanyikazi haki ya kutojibu isipokuwa kukataa kwao kuwe kutazingatiwa kuwa hakuna sababu ya kufanya hivyo.Mshirikishe mwenzako, Australia: Sheria ya kutowaadhibu wanaokataa kupokea simu baada ya kazi yaanza kutekelezwa
  3. Saa 4 zilizopitaKenya: Miungano ya kutetea maslahi ya walimu yatofautiana kuhusu mgomo.Chanzo cha picha,ReutersShule zimefunguliwa nchini Kenya kwa muhula wa tatu huku kukiwa na mkanganyiko kati ya Muungano wa walimu wa Shule za Msingi KNUT na Muungano wa walimu wa Shule za Sekondari KUPPET.Miungano hiyo ya kutetea maslahi ya walimu, awali ilikuwa imetangaza kuanza rasmi kwa mgomo hii leo wakati shule za zinafunguliwa.Lakini jana jioni, muungano wa KNUT ulitangaza kusitisha mgomo wa waalimu ukionyesha nia ya kutoa fursa kwa Tume ya Walimu nchini Kenya – TSC kutimiza ahadi zake.Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa KNUT, Collins Oyuu alitangaza kuwa malalamishi ya walimu yanashughulikiwa kiutawala.Hata hivyo, Muungano wa Walimu wa Shule za Sekondari KUPPET, ulitangaza kuendelea na mgomo wao na kusema kwamba hakuna aliyewasiliana nao kusikiliza matakwa yao.Tume ya chama cha walimu TSC, ilijitetea kwa kusema kuwa tayari imeanza kushughulikiwa baadhi ya matakwa ya walimu na kuwasihi kufika shuleni kama ilivyopangwa.Baadhi ya wanayotaka yaangaziwe ni pamoja na kuchelewesha waalimu kupandishwa vyeo, walimu tarajali kupewa kazi za kudumu, mazingira mabaya ya kufanyia kazi na mengineo.Mshirikishe mwenzako, Kenya: Miungano ya kutetea maslahi ya walimu yatofautiana kuhusu mgomo
  4. Saa 5 zilizopitaMwanamume mzee zaidi duniani: ‘Sina siri ya kipekee ya kuishi miaka mingi’.Chanzo cha picha,PA MediaMwanamume mwenye umri mkubwa zaidi duniani ametangaza kuwa hana “siri ya kipekee” kueleza kuhusu kuishi kwake miaka mingi alipokuwa akisherehekea kutimiza miaka 112.John Tinniswood, ambaye alizaliwa Liverpool tarehe 26 Agosti 1912, aliiambia Guinness World Records “hakujua kabisa” kwa nini ameishi miaka mingi namna hiyo.Mwanamume huyo ambaye anaishi katika nyumba ya kutunza wazee huko Southport, alikua mwanamume mzee zaidi duniani mnamo mwezi Aprili wakati Juan Vicente Pérez Mora wa miaka 114 alipofariki dunia.Alisema alikuwa “mchangamfu sana wakati wa ujana wake” na “alitembea kweli kweli”, lakini aliamini “hakuwa tofauti” na mtu mwingine yeyote, akiongeza kuwa: “Kuishi miaka mingi au michache, ni kitu ambacho huna uwezo nacho.”Bw Tinniswood, ambaye alizaliwa mwaka ambapo meli ya Titanic ilizama, alisema anatimiza miaka 112 “akiwa na matumaini ya kipekee”.”Kwa nini nimeishi miaka mingi hivyo, sijui hata kidogo,” alisema. “Siwezi kufikiria siri yoyote ya kipekee niliyo nayo.”Nilikuwa na shughuli nyingi kama kijana, nilitembea sana … Ikiwa hilo lilikuwa na uhusiano wowote na umri mrefu, sijui.”Lakini kwangu, sio tofauti. Hakuna cha upekee hata kidogo.”Bw Tinniswood alizaliwa miaka 20 baada ya klabu yake ya kandanda anayoipenda zaidi ya Liverpool kuanzishwa.Alikuwa na miaka miwili wakati Vita vya Kwanza vya Dunia vinaanza na alikuwa ametoka tu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 27 Vita vya Pili vya Dunia vilipoanza.Pia unaweza kusoma:Nchi 10 ambazo watu wanaishi muda mrefu zaidi na kile tunachoweza kujifunzaMshirikishe mwenzako, Mwanamume mzee zaidi duniani: ‘Sina siri ya kipekee ya kuishi miaka mingi’
  5. Saa 6 zilizopitaMkurugenzi Mtendaji aliyekamatwa hana ‘chochote cha kuficha’ – Telegram.Chanzo cha picha,AOP.Press/CorbisProgramu ya kutuma ujumbe Telegram imesema Mkurugenzi Mtendaji wake Pavel Durov, ambaye alikamatwa nchini Ufaransa siku ya Jumamosi, “hana cha kuficha”.Bw Durov alikamatwa katika uwanja wa ndege kaskazini mwa Paris chini ya kibali cha makosa yanayohusiana na programu hiyo, kulingana na maafisa.Uchunguzi huo unaripotiwa kuhusu ukosefu wa kuzuia misimamo mikali zaidi, huku Bw Durov akishutumiwa kwa kukosa kuchukua hatua za kuzuia uhalifu kwenye programu hiyo.Programu hiyo inashutumiwa kwa kushindwa kushirikiana na vyombo vya sheria kuhusu ulanguzi wa dawa za kulevya, maudhui ya ngono ya watoto na ulaghai.Telegram ilisema katika taarifa kwamba “usimamizi wake uko ndani ya viwango vya tasnia na uboreshaji kila wakati”.”Ni upuuzi kudai kwamba jukwaa au mmiliki wake anawajibika kwa matumizi mabaya ya jukwaa hilo,” programu hiyo ilisema.Telegram iliongeza kuwa Bw Durov husafiri Ulaya mara kwa mara na kuongeza kuwa anafuata sheria za Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Huduma za Kidijitali, ambayo inalenga kuhakikisha mazingira salama na ya kuwajibika mtandaoni.”Takriban watumiaji bilioni moja duniani kote hutumia Telegramu kama njia ya mawasiliano na kama chanzo cha habari muhimu,” taarifa ya programu hiyo iliandika.”Tunasubiri utatuzi wa haraka wa hali hii. Telegram iko pamoja nanyi nyote.”

TheHeartBeatofAfrica

WIMBI LA SIASA MAREKANI

UMEWAHI kutazama runinga, ukamuona mtu wa kwenu kijijini, ukatamani kumuuliza ‘ulipotelea wapi? Mbona hututembelei nyumbani’?

Juzi nilitamani kumuuliza maswali hayo rais wa 44 wa Amerika, Barrack Obama, alipotoa hotuba ya kusisimua ajabu kwenye Kongamano la Kitaifa la chama cha Democrat (DNC).

Nakuapia nitamuuliza maswali hayo nikikutana naye kwenye mitaa ya jiji la Washington, D.C. anakoishi baada ya kustaafu mnamo mwaka 2017.

Nitamkumbusha kauli yetu sisi Waafrika – na yeye ni mmoja wetu – inayosema kwamba ahadi ni deni, nayo dawa ya deni ni kulipa.

Ana deni letu kwa kuwa alituahidi kwamba akistaafu angetutembelea nchini Kenya mara kwa mara, sasa hana majukumu mengi kama zamani, lakini bado hajatimiza ahadi hiyo.

Tunamsubiri.

Japo sasa ni mstaafu, nadhani Obama anathamini amani na heshima zake zaidi.

Mambo yanayoendelea nchini Kenya yanaweza kukufanya kichaa, ukaokota takataka na kula kwenye mapipa ya taka pamoja na nguruwe, ukajifedhehesha.

Hata ingekuwa wewe, ungejisumbua kuzuru nchi ambako mambo yanakwenda visivyo, kuna wafanyakazi hewa wa serikali wanaolipwa mishahara, shule hewa za umma zinazopata migao ya fedha kila mwaka? Unaweza?

Hata ingekuwa wewe, ungezuru nchi ambako mibabe iliyoambatwa na taasubi ya kiume inamtimua ofisini, tena kwa kurudia, gavana wa kike kwa sababu haiamini inapaswa kuongozwa na mtu anayevaa rinda?

Mwanguko wa Kawira Mwangaza wa Meru ni ithibati ya kiza kinachotutawala.

Mwangaza akipata kiza mahakamani, Meru itakumbukwa milele kwa kulima mirungi ya kulewesha, kuuzia nchi nzima mbolea yenye mchanga na kuwadhalilisha wanawake.

Amini usiamini, watu wenye heshima zao kama Obama mwana wa K’ogelo wana akili razini zisizowaruhusu kujipaka matoke wakitagusana na watu wachafu, wasio na tatizo wakipigana miereka na nguruwe.

Kenya ni nchi inayojulikana sana ughaibuni kwa mambo makuu inayofanya duniani, lakini baadhi ya yanayofanyika ndani ya nchi ni ya kuudhi, na wengi hawangetaka kunasibishwa nayo.

Tufagieni nyumba yetu ili tuwafukuze viroboto, kupe, funza, vipepeo, viwavi na wadudu wote waharibifu ili tuepuke maradhi na fedheha, tuwavutie watu wa heshima kutoka kote duniani, watalii, wawekezaji na hata wasomi wazito.

Rais Obama, aliye na asili ya Kenya kwani marehemu babake alikuwa Mkenya, amerejea kwenye ulingo wa siasa kwa fujo, si kuwania urais tena, bali kumpigia debe mwandani na mwanafunzi wake wa kisiasa: Bi Kamala Harris.

Pamoja na mkewe, Michelle Obama, wameleta mwamko mpya katika chama cha Democrat na siasa za Amerika kwa jumla, wakatukumbusha miaka ambapo waliishi Ikulu ya White House na heshima za watu walioleleka na kuelimika vizuri.

Kelele za kuwashangilia zingekutoboa masikio, sikwambii na jumbe zao zilizo kama manukato, za kuwapa Waamerika matumaini.

Waliwakumbusha Waamerika unoko wa Donald Trump, miaka minne aliyoishi Ikulu na machafuko aliyoleta, migawanyiko aliyoibua, mbegu ya chuki aliyopanda, wakawahimiza wamzuie kuendelea na sinema hiyo kwani, kwa kawaida onyesho la pili huwa baya zaidi.

Kamala, ambaye ndiye Makamu wa Rais wa Amerika, anawania urais dhidi ya mrithi wa Obama, Trump, dume tatanishi kupitiliza ambalo huwatukana matusi ya nguoni wanawake, huchukia watu Weusi, huigiza walemavu na kusema heri wafe, hudharau maskini.

Hakika, Obama angehusishwa, hata kwa mbali sana, na moja kati ya mambo hayo ya kuudhi alipokuwa madarakani, angetafutiwa njia za kumtimua na kumsawiri kama mtu aliye na hulka ya mnyama.

Michelle alizungumzia jinsi Trump alivyojikakamua kuwachochea Waamerika kuwaogopa na kuwachukia yeye na mumewe, mbinu ambazo Trump amekuwa akitumia kumdhalilisha Kamala, aliyezaliwa na mama Mhindi na baba mweusi kutoka Jamaica.

Raha iliyoje kuwaona makada wa ngazi za juu wa chama cha Democrat wakiwakumbusha Waamerika kwamba siasa za chuki na matusi hazifai, kuwaasa wafanye siasa za uungwana na wala si za chuki anaoeneza Trump.

Kwenye kongamano hilo, Kamala aliidhinishwa rasmi kubeba mwenge wa chama cha Democrat, thibitisho kwa Trump kwamba hakika atakutana naye kwenye midahalo miwili inayotarajiwa kutoa cheche kali mwezi ujao, na ndani ya debe mnamo Novemba 5.

Haikosi thibitisho hilo linamkosesha usingizi Trump; chama cha Democrat kilimgeuzia kibao hivi majuzi kilipomshawishi Rais wa sasa, Joe Biden, asiwanie dhidi yake kwa sababu ya uzee, kikamuunga mkono Kamala.

Amini usiamini, kugeuziwa kibao ghafla kulimpa Trump kichaa, akaanza kuropokwa, akashindwa kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni, watu wake wakaungama kibao kimekula kwake, akasubiri Democrat wamalize kongamano lao ili ajue ataanzia wapi tena!

Daah! Msisimko ninaoshuhudia huku hauna mfano wake. Watu wanaweka nembo za kumdhihaki Trump na kumsifia Kamala kwenye magari yao bila kificho, wakitazamana wanacheka kana kwamba kuambiana ‘tusubiri siku ya kura ifike tumtie adabu fidhuli!’

Kambi ya Trump imedhihaki utasa wa wanawake wasio na watoto kwa kufuga paka badala ya kuzaa na kulea watoto, nao wamejibu kwa kuweka picha za paka kwenye madirisha ya magari yao na kutangaza: “Mimi ndimi mwanamke mfugaji paka!”

Mapema leo nilikutana na bi-vizee waliokuwa na nembo hizo waakiendelea na shughuli zao madukani. Nao wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 wakiketi chini kwenye maegesho na kuichekea kwa furaha nembo hiyo.
Vimwana hao waliovalia kaptura kutangaza haki zao na uhuru wanaofurahia kwa kuwa wanawake nchini Amerika waliapa kumzuia Trump kuwa chochote nchini mwao.

Suala tata la marufuku ya uavyaji mimba ambalo Trump amekuwa akilitumia kusawiri Democrat kama chama cha wauaji limemgeuka vibaya kwa kuwa limefafanuliwa kwa mapana na marefu.

Ajabu akidi ni kwamba limetokea kuwaunganisha wanawake wa vyama vyote viwili dhidi ya Trump kwa sababu marufuku hiyo pia inawanyima misaada wa kisayansi walio na changamoto ya kutunga mimba kwa kujamiiana kikawaida.

Mbinu ya wanasayansi kuunganishia kwenye maabara yai la mwanamke na mbegu ya mwanamume na kisha kuyapanda kwenye kizazi cha mwanamke ni marufuku kwenye majimbo mengi.

Trump na wenzake kwenye chama cha Republican wamenukuliwa wakishangilia hali ya taharuki iliyosababishwa na maruguku hiyo, jambo ambalo limemfanya adui nambari moja wa wanawake.

Wameapa kujitokeza kwa fujo kumpinga kwa kumchagua Kamala.

Suala la haki za wanawake limetokea kuugubika msimamo wa kuudhi wa chama cha Democrat kuunga mkono ushoga, mashoga nao wanaonekana kujifunza kutotanua vifua, kutotembea kwa mwendo wa aste-aste na kutoonyesha bendera yao ya upinde wa mvua hadharani.

Kwa ufupi, hata mambo ya kuudhi ambayo kwa kawaida huhusishwa na Democrat yanafumbiwa macho kwa sababu hayana uzito kama maudhi ya Trump, mhalifu aliyekutwa na hatia mara 34, ila aliyediriki kuwania wadhifa wa kuilinda na kuitetea Katiba ya Amerika.

Muujiza usipomtendekea Trump kati ya sasa na siku ya Uchaguzi Mkuu, ataingia kwenye kumbukumbu kama mwanasiasa aliyekomeshwa na wanawake alipothubutu kutumia unoko kushinda uchaguzi.

Kwa sasa, yeye na wao ni pamba na moto!

AMERIKA
Barrack Obama
donald trump
joe biden
Kamala Harris
Kawira Mwangaza
kogelo
Michelle Obama
obama
Uchaguzi Mkuu
USA
Waafrika

KIPENGA CHA MICHEZO

BINGWA wa Michezo ya Jumuiya ya Madola mbio za mita 100, Ferdinand Omanyala amejizolea Sh767,845 baada ya kukamata nafasi ya pili kwenye duru ya 12 ya riadha za Diamond League mjini Silesia nchini Poland, Jumapili.

Mshikilizi huyo wa rekodi ya Afrika ya sekunde 9.77, alitimka vizuri na kukamilisha umbali huo kwa 9.88.

Alimaliza katikati ya mshindi Fred Kerley kutoka Amerika (9.87) na Ackeem Blake kutoka Jamaica (9.89).

Bingwa wa Olimpiki 2020, Marcell Jacobs kutoka Italia aliridhika na nafasi ya nne kwa 9.93.

Mshindi na nambari tatu walituzwa Sh1.2 milioni na Sh447,910, mtawalia.

Wanawake washamiri

Nelly Chepchirchir naye alitawala mbio za 1,000m kwa dakika 2:31.24 akifuatwa na Muingereza Jemma Reekie (2:32.56), bingwa wa dunia na Jumuiya ya Madola mbio za 800m Mary Moraa (2:33.43) na Mganda Halimah Nakaayi (2:33.44), mtawalia.

Nyota wa Norway, Jakob Ingebrigtsen naye alivunja rekodi ya dunia ya Mkenya Daniel Komen akinyakua taji la 3,000m kwa dakika 7:17.55.

Jagina Komen alishikilia rekodi hiyo ya dunia ya umbali huo ya dakika 7:20.55 tangu 1997.

Ingebrigtsen alifuatiwa kwa karibu na Waethiopia Berihu Aregawi (7:21.28), Yomif Kejelcha (7.28.44) na Haile Telahun (7:30.97) na Mkenya Ronald Kwemoi (7:31.57) katika usanjari huo.

diamond league
jumuiya ya madola
Marcell Jacobs
michezo
poland
sekunde 9.77

All Rights Reserved © Cantona Group PLC


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment