Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Aina 5 Za Mitaji Wanazotumia Watu Wengi
Kuanzisha Biashara.
Ingawa kila mtu anahitaji mtaji kuanza kufanya biashara, ila watu wameanza kwa kutumia mitaji mbalimbali kuanza biashara zao.
Kwenye sura hii tutaangalia baadhi ya mitaji ambayo watu wameitumia kuanza biashara ili nawe uangalie ile ambayo itakufaa.
Aina Ya Kwanza: Wazo
Aina Ya Pili: Nguvu
Aina Ya Tatu: Bidhaa
Aina Ya Nne: Uaminifu
Aina Ya Tano: Pesa
Kwenye makala hii tutaangalia aina ya Nne ya mtaji.
Aina Ya Nne Ya Mtaji: Uaminifu
Wapo watu ambao walianza biashara zao kwa kutumia nguvu ya uaminifu wao.
Hawakuwa na pesa ila walikuwa wanaaminika na watu mbalimbali.
Wanachofanya ni kumuomba na kukubaliana na mtu mwenye bidhaa.
Kisha kuzichukua na kupeleka kuuza.
Kisha wanalipa gharama ya walikochukua na wao wanachukua cha juu.
Na kwa njia hii wanatengeneza faida.
Kuna watu wengi sana ambao wanafanya kazi ya kuuza vitu kwenye mitandao na hawana duka mahali popote.
Walichofanya ni kutumia uaminifu wao kwa kuwa na mahusiano mazuri na wenye maduka.
Na wewe sio lazima uwe na pesa ili uanze.
Unaweza na kujenga uaminifu wa kutosha na watu wakakuamini kukupa bidhaa zao.
Wakakuamini kutumia maeneo yao.
Au hata kukupa pesa unazotafuta bila masharti magumu.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.