Empowerment Mathematics

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Njia 4 Za Kutambua Kiwango Cha MTAJI Wa BIASHARA Ambacho Unahitaji.

Kabla haujaanza kutafuta mtaji, ni muhimu kujua kiwango cha mtaji unaoutafuta.

Kuna njia nne za kutambua kiwango cha mtaji unaokufaa:

a. Gharama Za Awali Za Kuanza Biashara.

b. Gharama Za Uendeshaji Wa Biashara.

c. Fuatilia/Jifunze Kwa Wanaofanya Tayari.

d. Uwe Na Bajeti Iliyoandikwa.

Leo tuanze kwa kuangalia njia ya kwanza.

a. Gharama Za Awali Za Kuanza Biashara.

Fuatilia kujua kiwango cha gharama za kila kitu unachohitaji ili kuanza biashara yako.

Ili kupata gharama kamili ni muhimu kuandika mchakato wa biashara (Business Process).

Yaani unajaribu kuangalia tangu unaponunua/kuzalisha bidhaa hadi kuuza.

Hii itakusaidia kutoacha gharama yoyote inayohusika.

Watu wengi wanapotafuta mtaji huwa wanaangalia vitu vichache tu.

Kama vile gharama ya kodi ya eneo la biashara, kununua, kusafirisha na kuuza.

Wanasahau kuna gharama zingine kama vile vibali, leseni n.k.

Hakikisha unaandika chini kila gharama inayohitajika kuanza biashara yako.

Ili usije kuanza biashara na unajikuta ulichonacho hakitoshi kabisa na unafeli njiani.

Natumai umejifunza kitu.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment