Makala Ya Bao La Asubui.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

UBAYA wa kuonekana wewe ni mtu mwenye NGUVU na HODARI ni kuwa hakuna MTU ATAKUULIZA HALI YAKO.

Kuna wengi ambao HAWAJUI, HAWAWEZI KUAMINI na hawawezi KUKUBALI kuwa, kuna wakati na wewe huwa unapitia MAMBO MAGUMU.

Yaani, kwa sababu huwa UNAJITOA sana kwa ajili ya NDUGU zako, basi hakuna anayewaza kuwa kuna wakati na wewe huww UNAHITAJI MSAADA.

Kuna wale wanakuona huwa UNASAIDIA sana marafiki zako, basi huwa wanataka uwasaidie tu, hawawezi hata kukuuliza unahitaji nini.

Na hata siku UKISEMA UNAHITAJI MSAADA, hakuna anayechukulia SERIOUS kabisa.

Tatizo la wengi ni kuwa, wakikuona UNASAIDIA wengine, huwa wanaamini kuwa ni kwa sababu UNAVYO VINGI.

Kwa sababu hii, wengi ambao wamekuwa msaada kwa NDUGU, MARAFIKI au WAFANYAKAZI wenzao, wamejikuta WAKIACHWA PEKE YAO wanapohitaji msaada.

Kila ANAYEJITOA kwa ajili yako, naye pia ANAHITAJI kusaidiwa anapohitaji msaada. USIMUACHE PEKE YAKE!

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment