Makala Ya Bao La Asubui.

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Kwenye kila MAJIRA ya maisha yako, kuna mtu anakuwa ameandaliwa kuwa MFARIJI WAKO (Comforter).

Mtu huyu anakuwa amepewa moyo wa kukuonea huruma ya kipekee…

…na huwa yuko tayari kutumia MUDA wake kukufariji.

Mara nyingi sana watu wa namna hii wanaweza kuonekana kuwa ni wa kawaida sana na pengine HAWANA PESA, CHEO au MALI.

Unachotakiwa kujua ni kuwa, watu wa namna hii, huwa hawajaletwa KUKUPA VITU…

…ila wameletwa KUKUPA FARAJA ambayo wenye mali, pesa na cheo hawawezi kukupa.

Watu hawa wanaweza wasiwe na wewe kila siku, inawezekana sio watu ambao unawapa kipaumbele…

..ila MUNGU amewapa NGUVU ya KUKUVUSHA kwenye MAGUMU YAKO.

Hawa ni wale ambao ukiongea nao, ukitumia muda nao au ukiwaona…

…au kuwasikiliza huwa unajihisi kama kuna MZIGO MKUBWA umeondolewa kwako.

Changamoto ya watu wengi, huwa watu hawa tunawasahau kabisa wakishatusaidia na huwa hatuwapi nafasi tena.

Hata kwa sasa kwenye maisha yako kuna mtu wa namna hii AMEANDALIWA na AMETUMWA kwako.

Usikimbilie kutafuta msaada kwa wenye pesa, mali na vyeo tu…

…muombe Mungu akufungue MACHO yako umuone mtu wa namna hii pia, unamuhitaji sana.

Kama umejifunza kitu kupitia ujumbe huu naomba chukua hatua mpigie simu na kumshukuru aina hii ya mtu…

…ambaye Mungu aliwahi kumtumia kukuvusha katika magumu.

Ukishampigia simu njoo hapa comment maneno “Nimeshamshukuru”

Naomba kama umejifunza kitu fanya mambo haya mawili…

1. NIANDIKIE ulichojifunza na unachoenda kufanyia kazi kwenye comments kwa ufupi…

Salamu ziwafikie waakazi wa Jiji la Eldoret Nchini Kenya.Na hili ndilo bao la asubui.

All Rights Reserved ©Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment