Afrika Leo Jioni -Agosti 12,2024

Radio Fortune Africa -Habari Kamili

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa


GAVANA wa Mombasa Abdulswamad Nassir amekashifu Bunge la Kitaifa akisema imeshindwa kulinda ugatuzi huku serikali za kaunti zikiendelea kucheleweshewa mgao huku zikipunguziwa fedha.

Bw Nassir alisema ni Bunge la Seneti pekee ambalo limekuwa mstari wa mbele kulinda ugatuzi.

Gavana huyu amewakia wabunge akisema wameshirikiana na serikali kuu kukandamiza serikali za kaunti.

Akizungumza katika mkutano wa kisiasa huko Jomvu, Bw Nassir alisema serikali za kaunti zinafaa kupokea Sh400 bilioni.

Bunge la kitaifa lilipunguza fedha hizo hadi Sh380 bilioni.

“Inasikitisha kuwa Bunge la Kitaifa lilikwenda na kukubaliana na serikali kuu ya kwamba serikali za kaunti zipunguziwe fedha za ugatuzi kutoka Sh400 bilioni hadi Sh380 bilioni. Ninashukuru maseneta ambao wametuhakikishia kwamba watalinda ugatuzi,” alisema Gavana Nassir.

Aliitaka serikali kuu kuwajibika na kuhakikisha serikali za kaunti zinapokea fedha za ugatuzi kwa mujibu wa sheria na hata katiba.

Bw Nassir alisema licha ya serikali kuu kuwa na changamoto za ukusanyaji wa ushuru au mapato, mzigo huo haufai kubebwa na serikali za kaunti.

Alisema ni wajibu wa serikali kuu kupunguza matumizi yake endapo inakabiliwa na changamoto za kifedha badala ya kupunguza za ugatuzi.

“Kwanza nalikosoa Bunge la Kitaifa, mlifanya makosa kikatiba, nashukuru bunge la seneti kwa kulinda katiba. Hivi karibuni Tume ya Mgao wa Mapato Nchini (CRA) italeta Miswada ya Fedha katika Bunge la Seneti, kuna dalili kaunti kadhaa za Pwani zitaumia,” akaongeza naibu huyo kiongozi wa chama cha ODM.

Aliwasihi maseneta wahakikishe kuna usawa na haki katika ugavi wa fedha.

Bw Nassir pia alijitetea akisema amekuwa akitumia fedha za ugatuzi kwa ajili ya maendeleo ikiwemo kuhakikisha mishahara ya wafanyikazi inalipwa kwa wakati na wanakandarasi waliojenga barabara pia wanalipwa.

“Sijawahi kurejesha fedha kwa serikali kuu, hata kama tunacheleweshewa fedha kwa muda wa miezi. Kwanza kama serikali ya kaunti tunadai fedha zaidi,” akasema.

Alisema alipunguza ada za leseni kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ili kupiga jeki biashara.

Bw Nassir alikuwa anawajibu wanasiasa na wapinzani wake wakubwa ambao walimtuhumu kuwa hawekezi kwenye sekta ya biashara kwa kuwapa vijana na kina mama mikopo.

Wiki iliyopita wanasiasa wa Mombasa wakiwemo Seneta Mohammed Faki, Spika wa Bunge la Mombasa Aharub Katri, Mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi na wengineo walimkashifu Gavana Nassir.

Walisema ameshindwa kuwekeza kwenye sekta ya ajira miongoni mwa vijana kwa kuwapa mikopo ili wafanye biashara.

Wanasiasa wa Mombasa walidai kuwa kuna fedha ambazo Gavana Nassir alirejeshea serikali kuu kwa kushindwa kuzitumia kuimarisha ugatuzi.

Hata hivyo Bw Nassir aliwaambia waache kuingiza siasa kwenye suala tata la ajira akiwasihi washirikiane kuimarisha ugatuzi.

“Nitarejea hapa Jomvu kutoa fedha za vikundi kwa vijana na kina mama wafanye biashara,” alisema Bw Nassir.

Bunge la Kitaifa na Ugatuzi
Bunge la Seneti
Gavana Abdullswamad Nassir
Sh380 bilioni
Sh400 bilioni

MKUU wa Utumishi wa Umma Felix Koskei amesema serikali inalenga kuwajibikia Wakenya kifedha kwa kuandaa mikutano na warsha zake kwenye taasisi za serikali.

Bw Koskei amesema uamuzi huo umeafikiwa ili kubana matumizi ya pesa za serikali na kuelekeza rasilimali za taifa kwenye miradi ya maendeleo wala hakuna ubadhirifu katika matumizi ya pesa za serikalini.

“Kama serikali, tutaendelea kuhakikisha kila shilingi inayokusanywa kutoka kwa Wakenya walipa ushuru inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Tutahakikisha hakuna ubadhirifu na kuwepo matumizi bora ya raslimali,” akasema Bw Koskei.

Alikuwa akiongea jana katika Chuo cha Mafunzo ya Wanajeshi Kenya mjini Karen Nairobi katika hafla ya utoaji mafunzo kwa mawaziri 19 ambao waliapishwa Alhamisi wiki jana katika ikulu ya Nairobi.

“Mikakati ya kupunguza matumizi ya fedha ilianza zamani. Tuliteua mahala hapa kwa sababu ni asasi ya serikali, ni karibu na Nairobi na kwa sababu ni mazingira tulivu tunamoweza kuendesha shuguli yetu ya kutoa mafunzo bila kutatizwa,” akaongeza Bw Koskei.

Hapo awali ambapo mafunzo hayo kwa mawaziri yalikuwa yakifanyika katika hoteli za kifahari hususan mjini Naivasha.

Mkuu huyo wa watumishi wa umma alifafanua kuwa mafunzo hayo yanadhamiriwa kuwapa maarifa mawaziri wapya ujuzi wa kutekeleza majukumu yao, hususan kwa wanaojiunga kwa mara ya kwanza na baraza la mawaziri.

Bw Koskei alisema mafunzo hayo yanakusudiwa kuhakikisha uwajibikaji na kuzuia ubadhirifu wa raslimali za umma kwa kuhakikisha, “kila waziri na katibu wa wizara yuko mstari wa mbele kupiga vita ufisadi katika wizara na idara wanazoongoza mtawalia.”

“Tunataka kuona vita vikali dhidi ya ufisadi. Kuhakikisha utekelezaji wa miradi kote nchini unaendeshwa kwa njia inayoridhisha pasipo ubadhirifu wowote,” alisema.

Kuhusu mtindo wa mawaziri kujishaua kwa maisha ya kifahari ikiwemo mavazi, Mkuu wa watumishi wa umma alisema baraza jipya litapatia kipaumbele “huduma kwa Wakenya.”

“Tunataka kuona huduma inayojikita kwenye mfumo ambapo kila afisa wa serikali kuanzia waziri hadi mtu wa ngazi ya chini kabisa katika wizara, anatilia maanani zaidi kuhudumia wananchi. Tunataka mabadiliko kamili. Badala ya kuwa mabosi wanakuwa watumishi wa watu na hivyo ndivyo tunataka kuhakikisha tangu mwanzo.”

“Masuala ya maisha ya kifahari, majigambo kwa kujilimbikizia vinono, ni jambo ambalo tumekubaliana litazikwa katika kaburi la sahau. Tujishughulishe sasa na utowaji huduma kwa Wakenya,”

Mkuu huyo wa watumishi wa umma alifafanua kuwa mafunzo hayo yanadhamiriwa kuwapa maarifa mawaziri wapya ujuzi wa kutekeleza majukumu yao, hususan kwa wanaojiunga kwa mara ya kwanza na baraza la mawaziri.

Alisema kuwa Rais Ruto alishiriki kikao mapema Jumatatu na mawaziri wapya ambapo aliwapa “maagizo na ushauri thabiti kuhusu kinachotarajiwa kutoka kwao wanapoanza kazi.”

“Hatuna muda wa kutosha. Mawaziri waliotangulia walikuwa wamefanya kazi nzuri kwa kiwango fulani na hatutaki kasi hiyo ishuke. Tunataka hata utekelezaji wa kasi zaidi wa miradi. Rais aliwaeleza wazi kabisa, wajiandae upesi, wafanye kazi kwa karibu na makatibu wa wizara na kuhakikisha Wakenya wamehakikishiwa utowaji huduma.”

Mawaziri wapya wanatazamiwa kujifunza masuala kadhaa ikiwemo, kufahamishwa kuhusu wajibu wa baraza, hasa kwa wanaohudumu kama mawaziri kwa mara ya kwanza, kujuzwa kuhusu miradi inayondelea, mifumo ya oparesheni za serikali na wajibu wanaopaswa kutekeleza.

“Kwa mawaziri wapya, tunawapa mafunzo ili wafahamu kanuni za utumishi wa umma, wajibu wa baraza na jukumu la waziri binafsi, wanapoendesha shughuli zao katika afisi zao mtawalia.”

“Mafunzo haya yatawawezesha kuelewa serikali, kukutana, kushikamana na kuwa kikosi kimoja kitakachofanikisha ajenda aliyozindua Rais na kuwaahidi Wakenya.

fedha
matumizi
serikali
umma

IDADI ya washukiwa waliokamatwa na kufikishwa kortini kuhusiana na kupatikana kwa grunedi katika makazi ya kiongozi wa chama cha Safina, Jimi Wanjigi imefikia wanne.

Washukiwa wapya, Kennedy Ochieng Asewe na Josiah Augo Otimo walifikishwa mbele ya hakimu mwandamizi Robinson Ondieki mnamo Jumatatu, Agosti 12, 204.

Awali, Dancan Otieno na Calvin Odongo walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Bernard Ochoi na kuamuru wazuiliwe siku saba lakini wakili Willis Otieno akaomba uamuzi huo ubatilishwe akisema “Wanjigi amefichua grunedi hizo ni za polisi na wala sio za washukiwa hao wala yeye.”

Mahakimu hao walifahamishwa na Wakili Willis Otieno kwamba “Wanjigi amefichua kwamba grunedi hizo ziliwekwa ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa nje ya makazi yake mtaani Muthaiga na polisi usiku wa Agosti 8, 2024.”

Vile vile, Otieno aliwaeleza Mabw Ochoi na Ondieki kwamba “Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi, Gilbert Masengeli aliwaambia wanahabari Agosti 8, 2024 kwamba polisi walipata grunedi hizo ndani ya nyumba ya Wanjigi.”

Alisema Otieno: “Wanjigi amefichua katika kesi aliyowashtaki IG, Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) Mohammed Amin na Mwanasheria Mkuu kwamba polisi ndio waliweka grunedi hizo katika gari lililokuwa limeegeshwa nje ya makazi yake nyumba Nambari 44.”

Wakili huyo aliomba mahakimu wawaachilie huru Otimo, Asewe, Odongo na Otieno akisema “washukiwa hawa ni vibarua wa Wanjigi. Hawajui chochote kuhusu silaha hizi. Wanjigi amedai ni polisi walioziweka ndani ya gari lililoegeshwa nje ya makazi yake.”

Mahakama ilifahamishwa kwamba kuna picha za video zilizonukuliwa na kamera za CCTV zilizo katika makazi ya Wanjigi.

“Ushahidi upo. Wanjigi amedai grunedi ni za polisi. Washukiwa hawa hawajui chochote kuzihusu,” Bw Otieno aliambia mahakama.

Lakini viongozi wa mashtaka James Gachoka, Herbert Sonye na Everlyne Mutisya walipinga ombi la Otieno wakisema polisi wanahitaji muda kukamilisha uchunguzi.

Gachoka alisema grunedi hizo zitapelekewa wataalamu wa silaha kuzikagua kubaini zilikotoka.

Gachoka alisema polisi pia wanataka kutambua walikotoka washukiwa hao kwa vile hawakuwa na vitambulisho.

Awali, Otieno alisema polisi wamekaa na washukiwa hao kwa siku tano na wangekuwa wamekamilisha uchunguzi wao.

Alisema Asewe na Otimo walitiwa nguvuni mtaani Soweto Dandora na wala hawakutiwa nguvuni na polisi katika makazi ya Wanjigi.

Grunedi
Muthaiga
polisi
wanjigi

MBUNGE wa Makadara George Aladwa amemtaka Waziri mpya wa Vyama vya Ushirika na Biashara Ndogo Wycliffe Oparanya kutumia wadhifa wake kusaidia wakazi wa eneo la Magharibi mwa Kenya.

Bw Aladwa alisema kuwa wakati umefika ambapo jamii ya Mulembe inastahili kunufaika na uwepo wa viongozi wao ndani ya serikali jumuishi.

Mulembe, ni jina la majazi linalotumika kutambua jamii ya eneo la Magharibi mwa Kenya, Waluhya.

Bw Oparanya ni kati ya mawaziri ambao wanatoka mrengo wa Kinara wa Upinzani Raila Odinga ambao walinufaika kutokana na mabadiliko ya mwezi uliopita, Julai 2024, kwenye baraza la mawaziri.

“Sisi kama watu kutoka eneo la Magharibi hatujanufaika ilhali baadhi ya viongozi wetu wamekuwa wakisema wapo serikalini. Bw Oparanya naomba utumie wadhifa huu kuleta mabadiliko eneo letu,” akasema Bw Aladwa.

Alikuwa akizungumza kwenye ibada katika kanisa moja Makadara, maombi ambayo yalihudhuriwa pia na Bw Oparanya mwenyewe.

“Tafadhali saidia makundi ya akina mama na vijana kwa sababu wizara unayoshikilia ina umuhimu sana. Uwepo wapo serikalini unastahili kuhisiwa kupitia miradi ya maendeleo,” akaongeza mbunge huyo wa ODM.

Bw Aladwa alisema wanasiasa wa Magharibi wanaohudumu kwenye baraza la mawaziri hawafai kulala kazini na kwamba wanapaswa kumuiga Naibu Rais Rigathi Gachagua ambaye amekuwa akiwatetea sana wakazi wa Mlima Kenya.

“Gachagua amekuwa akisema serikali hii ni ya hisa. Hisa ya watu wa Magharibi ni hizi wizara mnazoshikilia,” akasema.

Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula wanaotoka eneo hilo, wamekuwa wakikashifiwa kwa kutofanya chochote kuhakikisha wanainua maisha ya wakazi wa eneo la Magharibi.

George Aladwa
Magharibi mwa Kenya
waziri
Wycliffe Oparanya

WANASIASA wa Nyamira wametofautiana kuhusu mahali ambapo chuo kikuu kinastahili kuanzishwa katika kaunti hiyo huku Rais William Ruto akianza ziara ya siku tatu eneo la Gusii leo.

Mbunge wa Mugirango Joash Nyamoko amesema jiwe la msingi la ujenzi wa chuo hicho litawekwa na Rais katika Shule ya Upili ya Kiabonyoru.

Hata hivyo, mwenzake wa Mugirango Mashariki Stephen Mogaka amesema suala la kuzinduliwa kwa ujenzi wa chuo hicho halipo katika shajara ya Rais.

Kando na wanasiasa hao wawili, Gavana Amos Nyaribo, wabunge Patrick Osero (Borabu) na Clive Gisairo wa Kitutu Masaba pia wapo katika mzozo huo kuhusu mahali pa ujenzi wa chuo hicho kipya.

Aidha, kuna mapendekezo mengine kuwa chuo hicho kinastahili kujengwa Manga katika eneobunge la Kitutu Masaba na shule za upili za Kebaso na Riakimai (Mugirango Magharibi).

Pia, Ikonge na Kiamogake kwenye eneobunge la Mugirango Kaskazini ni kati ya maeneo ambayo yametajwa, utata kuhusu kunakostahili kujengwa kwa chuo kikuu cha Nyamira ukiendelea kushamiri.

Kiabonyoru kwenye mpaka wa maeneobunge ya Borabu Kaskazini na Borabu pia imetajwa.

“Rais hajii eneo la Gusii kuzindua ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyamira. Anakuja kuanzisha ujenzi wa miradi mbalimbali hasa miundomsingi katika shule zilizopata ufadhili kutoka kwa serikali ya Kuwait,” akasema Bw Mogaka.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, Tume ya Elimu ya Juu (CUE) haijaamua eneo ambalo chuo hicho kitajengwa.

“Tulimweleza Rais kuwa baadhi ya miradi iliyozinduliwa haikuwa imeanza kutokana na ukosefu wa fedha. Tumemwambia asizindue ujenzi wa chuo kikuu kipya iwapo hakutakuwa na pesa za kuutekeleza ujenzi huo,” akasema Bw Mogaka.

Aliwataka wenyeji wasimakinikie uvumi unaoendelezwa na baadhi ya viongozi kuwa Rais anakuja Nyamira kuzindua ujenzi wa chuo kikuu.

Bw Nyamoko awali alikuwa amesema kuwa Rais Ruto atazindua ujenzi wa chuo hicho wakati wa ziara yake eneo la Gusii.

“Chuo Kikuu kitakuwa Kiabonyoru na mipango yote imekamilishwa huku Rais akitarajiwa kuzindua ujenzi wake,” akasema Bw Nyamoko wiki jana.

“Rais atazindua ujenzi wa mradi unaodhaminiwa na serikali ya Kuwait pale Kiabonyoru na kutangaza pia kuanzishwa kwa chuo hiki,” akaongeza Bw Nyamoko.

Rais Ruto alistahili kuanza ziara yake eneo la Gusii wiki jana lakini duru zinaarifu aliahirisha kutokana na viongozi wa eneo hilo kutokuwa tayari kuwa mwenyeji wake.

Pia, kuna madai eneo la Gusii linalalamika kutonufaika walivyotarajiwa baada ya baraza jipya la mawaziri kubuniwa kutokana na maandamano yaliyokuwa yakiendelezwa na Gen Z.

Kuhusu mahala pa ujenzi wa chuo kikuu, Bw Gisairo alimshutumu Bw Nyamoko akisema wanasiasa wa eneo hilo hawajakubaliana chuo hicho kijengwe Kiabonyoru.

“Tulikutana Mombasa na hatukuelewana kwa sababu kila moja alikuwa akitaka chuo hicho kijengwe eneo lake,” akasema Bw Gisairo.

Mbunge huyo alisema waliwaachia usimamizi wa Chuo Kikuu cha Kisii na CUE waamue eneo ambalo linastahili kwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Nyamira.

Bw Gisairo aliongeza kuwa Nyamira ina kaunti ndogo tano na raslimali pamoja na ujenzi wa taasisi za masomo unastahili kufanyika kwa usawa.

Kaunti ya Nyamira haina chuo kikuu na mjadala wa ujenzi wa taasisi hiyo ya juu ya elimu ulianza wakati wa enzi za Gavana wa kwanza marehemu John Nyangarama.

chuo kikuu
Kiabonyoru
nyamira
ruto

WAZIRI mpya wa Elimu Migos Ogamba anakabiliwa na kibarua kigumu huku miungano ya walimu nchini ikitangaza kuwa walimu watashiriki mgomo na kulemaza shughuli za elimu katika muhula wa tatu.

Bw Ogamba aliapishwa katika Ikulu ya Nairobi Alhamisi, Agosti 8, 2024 na anachukua usukani kwenye wizara ambayo tayari inakabiliwa na changamoto si haba.

Uongozi wa Chama cha Kutetea Walimu Nchini (KNUT) na ule wa Muugano wa Walimu Wakuu wa Shule za Upili na Vyuo Anuwai (KUPPET) umetangaza kuwa walimu watashiri mgomo wakati shule zitakuwa zikifunguliwa kwa muhula wa tatu mwishoni mwa mwezi huu, Agosti.

Alipofika mbele ya Kamati ya Bunge la Kitaifa iliyokuwa ikiwapiga mawaziri msasa, Bw Ogamba alisema alifahamu changamoto ambazo zilikuwa zikiathiri sekta hiyo.

Alitaja uhaba wa walimu, kukosekana kwa miundomsingi katika shule mbalimbali na wazazi kutohusishwa kwenye usimamizi wa shule kama baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zikiathiri sekta hiyo.

Iwapo mgomo wa walimu utafanyika muhula wa tatu basi watahiniwa wa mtihani wa gredi ya sita na wale wa kidato cha nne, watataabika kwenye maandalizi yao ya kukabili mitihani hiyo.

Baadhi ya matakwa ambayo yameibuliwa na walimu yanastahili kusuluhishwa na Tume ya Kuwaajiri Walimu Nchini (TSC).

Hata hivyo, Bw Ogamba ana kibarua cha kuzuia mgomo huo na hata itamlazimu kujifunza jinsi watangulizi wake walikuwa wakishughulikia utata huo.

Wanafunzi, wazazi, walimu pamoja na washikadau wengine wanasubiri kuona jinsi Bw Ogamba atashughulikia wanafunzi kujiunga na gredi ya tisa ambayo kupitia Mtaala wa Utendaji na Umilisi (CBC) ndio wa mwisho kwenye masomo ya shule ya msingi.

“Nitabadilisha tu sera ambazo hazifanyi kazi kwa sababu serikali ni ile ile,” akasema Bw Ogamba.

Waziri huyo alichukua hatamu za wizara yake Jumatatu, Agosti 12, 2024 lakini mtangulizi wake Ezekiel Machogu hakuwepo kumkabidhi afisi hiyo rasmi.

Bw Ogamba alikuwa mgombeaji mwenza wa Bw Machogu kwenye mbio za kusaka ugavana wa Kisii mnamo 2022.

MAHAKAMA ya Mazingira na Ardhi imetoa uamuzi ambapo mwanamke mmoja anatakiwa kulipa kanisa la Katoliki Dayosisi ya Nakuru Sh23 Milioni.

Sasa mwanamke huyo anatakiwa kurejesha pesa alizopokea kwa njia ya ulaghai baada ya kushtakiwa kwa kuuzia kanisa ardhi hewa.

Jaji Anthony Ombwayo alimwagiza Bi Hannah Wairimu Kahiga alipe pesa hizo zinazojumuisha Sh 19,800,000 ambazo kanisa lililipa kwa ununuzi wa shamba la ekari 11 katika eneo la Kiambogo, kaunti ndogo ya Naivasha na Sh 3, 960,000 kama fidia.

Uamuzi huo ulitolewa baada ya kubainika kuwa mshtakiwa aliuza shamba la mtu mwingine kwa kutumia hati bandia.

Bi Hannah Wairimu anadaiwa kushirikiana na maafisa katika afisi ya ardhi kuuza shamba hilo la ekari 11 ambalo ni sehemu ya shamba la Teresia Wanjiru Wangera aliyefariki 1981.

“Mshtakiwa wa Kwanza (Bi Wairimu) hajathibitisha kwa mahakama hii kwamba alipata hatimiliki kihalali na kiutaratibu alipouza mali hiyo kwa Mlalamishi (Kanisa Katoliki),” Jaji Ombwayo akaamua.

Kanisa kupitia wadhamini wake waliosajiliwa ambao maafisa wao wa sasa ni Maurice Muhatia, Askofu Mkuu Kisumu, baba Lawrence Mbogo na baba Simon Kamau walimwendea Bi Wairimu kwa nia ya kununua ardhi hiyo kwa mradi wa kanisa.

Askofu Mkuu Kisumu
baba Lawrence Mbogo
Bi Hannah Wairimu
kanisa la Katoliki Dayosisi ya Nakuru
MAHAKAMA ya Mazingira na Ardhi
Maurice Muhatia
Sh23 milioni
Shamba bandia

KWINGINEKO DUNIANI

Ripoti zilizofuata zilidokeza kwamba vikosi maalum vya Ukraine viliwafunza waasi hao kutumia ndege zisizo na rubani.

Kwa baadhi ya Waafrika, hiki kilikuwa kisa kingine cha mataifa ya nje kutumia bara hili kama uwanja wa umwagaji damu kwa wapinzani wao wenyewe.

Kama ilivyotabiriwa, utawala wa kijeshi nchini Mali, na serikali ya washirika katika nchi jirani ya Niger, zilijibu hatua hiyo kwa kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Kyiv.

Lakini jambo la msingi zaidi lilikuwa ni tamko la kambi ya kikanda, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas). Licha ya mvutano kati yake na tawala za kijeshi nchini Mali, Niger na Burkina Faso, ilikemea hatua ya Ukraine.

Ilitangaza kwamba “hataikubalina na uingiliaji wowote wa mataifa ya nje katika kanda hiyo kwani hatua hiyo ni tishio kwa amani na usalama katika Afrika Magharibi na kulaani vikali jaribio lolote linalolenga kuliingiza eneo hilo katika makabiliano ya sasa ya kijiografia”.

Msimamo huo mkali huenda umetokana na mapendekezo kwamba baadhi ya wanamgambo wa kijihadi walijiunga na waasi wa Tuareg katika kuendeleza mashambulizi ya Tinzaouaten.

Wizara ya mambo ya nje ya Senegal iliwasilisha malalamiko yake kwa balozi wa Ukraine mjini Dakar baada ya kuchapisha video ya Facebook kuhusu maoni ya bwana Yusov.

Wafuasi wa utawala wa kijeshi nchini Mali wakipeperusha bendera za Urusi wakati wa maandamano ya kuiunga mkono Urusi huko Bamako, Mali – Mei 2022Chanzo cha picha,AFP
Maelezo ya picha,Tangu mapinduzi ya 2020 nchini Mali, utawala wa kijeshi umewafukuza wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa na kuchukua msimamo wa kuunga mkono Urusi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba wiki iliyopita alizuru mataifa ya Malawi, Zambia na Mauritius. Lakini baada ya matamshi makali yaliyotolewa na Ecowas na Senegal sasa huenda akalazimika kushughulikia mzozo wa kidiplomasia ulioibuka kati ya nchi yake na Afrika Magharibi.

Kile ambacho serikali kadha za Afrika hasa katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara – hata zile ambazo kimya kimya hazina imani na Moscow – labda zitakiona kama ujio wa kijeshi wa Kyiv usio na manufaa kinaweza kuondoa nia njema iliyokuzwa kwa bidii katika miaka miwili iliyopita kupitia diplomasia ya amani ya Ukraine.

Mamluki wa Wagner – ambao sasa wamepewa jina rasmi la Corps Africa baada ya kuwekwa chini ya udhibiti wa serikali ya Urusi – walikuwa ameongeza wafanyikazi wake mara mbili hadi 2,000 nchini Mali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kwa hivyo taarifa za mashambulizi ya Tinzaouaten zilikuja kama mshtuko, hasa ikizingatiwa kwamba jeshi la Mali na vikosi vya Wagner viliuteka mji wa Kidal, “makao makuu” ya waasi wa Tuareg, Novemba iliyopita.

Tukio la Tinzaouaten limeashiria kurejea tena kwa mashambulizi ya kijihadi – na hivi karibuni wakiuungwa mkono na mshirika mpya.

Vidokezo vya Kyiv vya kuhusika moja kwa moja vinathibitisha ni kwa kiasi gani nchi hiyo iko tayari kwenda ili kufikia malengo yake katika mapambano dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin zaidi ya uwanja wa vita wa nyumbani.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ukraine kuingilia moja kwa moja operesheni za kijeshi za Corps Africa (Wagner) barani Afrika.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba mwezi Agosti na Septemba mwaka jana vikosi maalum vya Ukraine vilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani nchini Sudan kwa ajili ya kuunga mkono utawala wa kijeshi unaoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja, amekuwa ikizozania mamlaka na washirika wake wa zamani wa Rapid Support Forces (RSF) wanaongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu “Hemedti”, ambaye amesaidiwa na Wagner.

Ripoti zilizofuata zilidokeza kwamba vikosi maalum vya Ukraine viliwafunza waasi hao kutumia ndege zisizo na rubani.

Kwa baadhi ya Waafrika, hiki kilikuwa kisa kingine cha mataifa ya nje kutumia bara hili kama uwanja wa umwagaji damu kwa wapinzani wao wenyewe.

Kama ilivyotabiriwa, utawala wa kijeshi nchini Mali, na serikali ya washirika katika nchi jirani ya Niger, zilijibu hatua hiyo kwa kusitisha uhusiano wa kidiplomasia na Kyiv.

Lakini jambo la msingi zaidi lilikuwa ni tamko la kambi ya kikanda, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (Ecowas). Licha ya mvutano kati yake na tawala za kijeshi nchini Mali, Niger na Burkina Faso, ilikemea hatua ya Ukraine.

Ilitangaza kwamba “hataikubalina na uingiliaji wowote wa mataifa ya nje katika kanda hiyo kwani hatua hiyo ni tishio kwa amani na usalama katika Afrika Magharibi na kulaani vikali jaribio lolote linalolenga kuliingiza eneo hilo katika makabiliano ya sasa ya kijiografia”.

Msimamo huo mkali huenda umetokana na mapendekezo kwamba baadhi ya wanamgambo wa kijihadi walijiunga na waasi wa Tuareg katika kuendeleza mashambulizi ya Tinzaouaten.

Wizara ya mambo ya nje ya Senegal iliwasilisha malalamiko yake kwa balozi wa Ukraine mjini Dakar baada ya kuchapisha video ya Facebook kuhusu maoni ya bwana Yusov.

Wafuasi wa utawala wa kijeshi nchini Mali wakipeperusha bendera za Urusi wakati wa maandamano ya kuiunga mkono Urusi huko Bamako, Mali - Mei 2022
Maelezo ya picha,Tangu mapinduzi ya 2020 nchini Mali, utawala wa kijeshi umewafukuza wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa na kuchukua msimamo wa kuunga mkono Urusi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba wiki iliyopita alizuru mataifa ya Malawi, Zambia na Mauritius. Lakini baada ya matamshi makali yaliyotolewa na Ecowas na Senegal sasa huenda akalazimika kushughulikia mzozo wa kidiplomasia ulioibuka kati ya nchi yake na Afrika Magharibi.

Kile ambacho serikali kadha za Afrika hasa katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara – hata zile ambazo kimya kimya hazina imani na Moscow – labda zitakiona kama ujio wa kijeshi wa Kyiv usio na manufaa kinaweza kuondoa nia njema iliyokuzwa kwa bidii katika miaka miwili iliyopita kupitia diplomasia ya amani ya Ukraine.

Mamluki wa Wagner – ambao sasa wamepewa jina rasmi la Corps Africa baada ya kuwekwa chini ya udhibiti wa serikali ya Urusi – walikuwa ameongeza wafanyikazi wake mara mbili hadi 2,000 nchini Mali katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Kwa hivyo taarifa za mashambulizi ya Tinzaouaten zilikuja kama mshtuko, hasa ikizingatiwa kwamba jeshi la Mali na vikosi vya Wagner viliuteka mji wa Kidal, “makao makuu” ya waasi wa Tuareg, Novemba iliyopita.

Tukio la Tinzaouaten limeashiria kurejea tena kwa mashambulizi ya kijihadi – na hivi karibuni wakiuungwa mkono na mshirika mpya.

Vidokezo vya Kyiv vya kuhusika moja kwa moja vinathibitisha ni kwa kiasi gani nchi hiyo iko tayari kwenda ili kufikia malengo yake katika mapambano dhidi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin zaidi ya uwanja wa vita wa nyumbani.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ukraine kuingilia moja kwa moja operesheni za kijeshi za Corps Africa (Wagner) barani Afrika.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba mwezi Agosti na Septemba mwaka jana vikosi maalum vya Ukraine vilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani nchini Sudan kwa ajili ya kuunga mkono utawala wa kijeshi unaoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja, amekuwa ikizozania mamlaka na washirika wake wa zamani wa Rapid Support Forces (RSF) wanaongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu “Hemedti”, ambaye amesaidiwa na Wagner.

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment