Radio Fortune Africa -Kipindi Cha Matumaini
“Kama kware akusanyaye makinda asiyoyazaa, ndivyo alivyo mtu ajipatiaye mali, wala si kwa haki, katikati ya siku zake zitaachana naye, na mwisho wake atakuwa mpumbavu.”
(Yeremia 17:11).
Mali yeyote iliyopatikana kwa njia ya mkato (Uongo, utapeli, kuua, kudhurumu, kuuza mwili, nakadhalika) haiwezi kudumu hadi mwisho wa maisha ya mtu…..
Mafanikio yanahitaji mahusiano kati yako na yenyewe, ambayo itahusisha nidhamu na kulipa gharama.
Hiyo ndiyo njia pekee ya kuyapata, kuyatunza na kuyapa haki ili yawe mafanikio yako.
Na hii haihusishi mafanikio ya vitu kama vile nyumba, gari, biashara nakadhalika, bali hata kupata mke sahihi….
Huwezi kuwa na ndoa ya amani na ikadumu iwapo mke huyo umempata kwa kumuiba kwa mwanaume mwingine.
Mke wa hivyo ni ngumu sana kufika nae uzeeni labda ufe njiani au uishi nae kwa mateso makubwa, ni lazima hapa kati ataondoka na kwa mujibu wa andiko hili utabaki kuwa mpumbavu………
Hilo ndilo neno la BWANA…..
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.