Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Napoleon Bonaparte aliwahi kusema…
“Ujasiri sio pale unapokuwa na nguvu za kuendelea…
…bali pale unapoamua kuendelea hata kama unaona HAUNA nguvu”
Kuna siku kama hizi zitakuwepo kwenye Maisha Yako.
Kila utakapokuwa unajiangalia utaona hauna kabisa nguvu za kusonga mbele.
Utakuwa unatamani kuacha kabisa unachofanya.
Utajiridhisha kuwa hakuna namna unaweza kufanikiwa tena.
Kwa sababu umefanya kila juhudi na hakuna kilichotokea.
Hata wanaokuzunguka watakuwa wanakuonea Huruma.
Na hata ukisema unaacha hakuna atakayeshangaa.
Siku hizi ni zile ambazo kila ukibakia peke yako…
…machozi yatakuwa yanakutiririka na MAUMIVU na HUZUNI.
Nyakati kama hizi ndio unahitaji ujasiri.
Wakati kama huu ambapo umejiridhisha kuwa hauna nguvu za kuendelea.
Hauna nguvu hata kidogo za kuchukua hatua moja mbele.
Hauna hata nguvu za kuzungumza tena.
Huu ndio wakati wako wa kuonyesha ujasiri wako.
Najua ujumbe huu ni wako.
Umekuja kwako kwa sababu kama ukiamua kuvumilia kidogo…
…na kufanya kitu leo mabadiliko Makubwa yatatokea.
Na utasahau kila unachopitia.
Don’t Quit, Don’t Stop, Keep Moving.
USIACHE KUFANYA.
USIACHIE NJIANI ENDELEA MBELE.
ENDELEA KUPAMBANA KWA AJILI YA MAONO YAKO MAKUBWA.
NDOTO ZAKO KUBWA.
ENDELEA KUJILAZIMISHA HATA UKISIKIA…
…HUNA NGUVU KABISA ZA KUENDELEA MBELE.
Una uwezo wa kulishinda hili.
Kuna nguvu ndani yako ya KUVUKA SALAMA katika hili.
UNA UWEZO mkubwa wa KUIBUKA mshindi.
Kuna JIBU lako liko KARIBU kabisa na wewe.
JILAZIMISHE leo kuwa na UJASIRI UPATE USHINDI.
Nasubiria USHUHUDA WAKO.
Don’t Quit!
Salamu ziwafikie watu wa Kisumu Nchini Kenya,hili ndilo Bao La Asubui.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.