Bao La Asubui -Agosti 8,2024.Kabla hujarusha Jiwe-Jichunguze…

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Uwe na REHEMA kwa wengine!…

____Kwenye haya maisha utakutana na wengi sana WATAKAOKUKOSEA…

Na wengine WATAKUUMIZA…

Mbaya zaidi wengine watakuwa ni watu wako wa KARIBU sana.

Au wale ambao HAUKUWATARAJIA.

Ni rahisi sana kuingia kwenye MTEGO wa kuwa mtu wa KUHUKUMU…

Na kuwasema WENGINE VIBAYA.

Hebu jikumbushe:

Hivi wewe ni MKAMILIFU…

Na HAUJAWAHI KUKOSE hata siku MOJA?

Hivi ni kweli haujawahi KUSAMEHEWA na wengine ULIOWAKOSEA?

Kuna wakati UKIJITAFAKARI unaweza kugundua kuwa kuna MAKOSA mengi UMEFANYA…

Ila ni kwa sababu WATU HAWAYAJAYAJUA BADO.

Uwe na REHEMA kwa wengine…

Ni mbegu nzuri ya wewe pia kupata REHEMA utakapokosea.

Unakumbuka neno hili watu walipomtaka Yesu amuhukumu mwanamke aliyestahili kuuwawa?

Akawaambia….

”Asiye na Dhambi Aanze Kuchukua Jiwe na Kumpiga…”.

Baada ya muda, washtaki wote walipotea.

Kabla HAUJARUSHA JIWE…

…kwanza CHUNGUZA MOYO WAKO.

Uwe na Rehema kwa Wengine.

Salamu ziwafikie wakaazi wa mkoani Mbeya Nchini Tanzania

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment