Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

RAIS William Ruto ametetea vikali hatua yake ya kujumuisha upinzani kwenye serikali ya Kenya Kwanza kupitia uteuzi wa baadhi ya wanasiasa wa Azimio, kujiungva na Baraza lake la Mawaziri.
Akizungumza katika Kaunti ya Embu Jumatano, Agosti 7, 2024, Rais Ruto alisema hatua hiyo itamsaidia kuletea nchi maendeleo.
Akifafanua, kiongozi wa nchi alisema kupitia serikali ya umoja wa kitaifa watasaidiana kuangazia changamoto zinazozingira nchi.

“Niliapa kuunganisha Wakenya wote, na juzi nimetengeza serikali inayojumuisha kila mtu. Hata wale walikuwa wanapiga kelele nje, nimewaambia kujeni tuketi pamoja ndio hii pesa tutafute pamoja, madeni tulipe pamoja, na ushuru tutafute pamoja,” Rais alisema.
Julai 2024, siku chache baada ya kuvunja Baraza lake la Mawaziri, Rais Ruto aliteua Mabw John Mbadi kuwa Waziri wa Fedha na Hazina ya Kitaifa, Opiyo Wandayi (Kawi), Gavana wa zamani Mombasa Hassan Joho (Madini na Uchumi Samawati na aliyekuwa Gavana wa Kakemega, Wycliffe Oparanya kusimamia Wizara ya Vyama vya Ushirika na Maendeleo ya Biashara Ndogo Ndogo na zile za Kadri, wote wakiwa ni wanasiasa wa upinzani – Azimio.
Kufuatia kuendelea kupanda kwa gharama ya maisha na uchumi ambapo Dkt Ruto amekuwa akikosolewa kwa kuongeza ushuru wa ziada (VAT) hasa kwa bidhaa muhimu za kimsingi, wakosoaji wake wamempa jina la utani la Zakayo.
Zakayo ni mhusika kwenye Biblia ambaye alikuwa mtoza ushuru tajiri na mkuu wa watoza ushuru Jericho, ambapo Yesu alipokuwa akipita eneo hilo alitaka kumwona.
Hata hivyo, hakuweza kumwona kwa sababu ya kimo chake cha ufupi akiwa kwenye umati mkubwa wa watu waliojitokeza, hivyo basi akalazimika kupanda mti aina ya mkuyu.
Yesu alipomwona, alimtaka ashuke haraka akisema yeye – Yesu atakuwa mgeni nyumbani kwake na watu waliposkia hayo wakaanza kunung’unika, wakilalamika ameenda kwa mtu mwenye dhambi.
Rais Ruto amenukuliwa mara kadha akihoji hashtuliwi na watu kumuita Zakayo.
Akitetea uteuzi wa wanasiasa kadha kutoka Azimio kujiunga na Baraza la Mawaziri wa serikali ya Kenya Kwanza, alidai yeye hataki kuitwa Zakayo pekee yake.
“Mimi sitaki kuwa Zakayo pekee yangu, kila mtu akuje akuwe Zakayo hapa ndani,” Dkt Ruto aliambia umma eneo la Kanyuambora, Mbeere Kaskazini kufuatia ziara yake Kaunti ya Embu.
Katika kile kilionekana kama kuainisha uwazi wa utendakazi wake hasa katika ukusanyaji ushuru, Rais alisema fedha hizo zinapokusanywa huelekezwa kwenye akaunti ya Hazina ya Kitaifa.
“Kwani ile ushuru inakusanywa inapelekwa kwa akaunti yangu (Ruto)? Inapelekwa kwa akaunti ya Hazina ya Kenya. Kila mtu akuje hapa tuongee hiyo maneno, vile tutalipa madeni, vile tutatafuta ushuru, vile tutapanga maendeleo ili Kenya iende mbele,” alifafanua.

KAIMU Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli amewaagiza maafisa wa polisi kufuata sheria wakitekeleza majukumu yao, siku moja tu kabla ya maandamano yanayopangwa ya Nane Nane.
“Kila Mkenya kwa mujibu wa sheria ana uhuru wa kuandamana, kulalamika na kukusanyika kulingana na sheria. Hilo kila mtu analifahamu sana. Na pale uhuru wa mmoja unapoishia, ndipo wa mwingine unapoanzia. Tunatawaliwa na Mkataba wa Roma na Katiba ya Kenya,” akasema.
Bw Masengeli alizungumza wakati wa mkutano na makamanda wa Polisi wa Kenya, Polisi tawala na Idara ya Upelelezi wa Jinai katika Chuo cha Kitaifa cha Mafunzo ya Polisi, Embakasi Jumanne, Agosti 6, 2024.
Mkutano huo ulifanyika kabla ya maandamano ya Nane Nane yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi, Agosti 8, 2024.
Maandamano hayo yatakuwa mtihani kwa makamanda wa polisi huku huduma hiyo ikilaumiwa vikali kwa jinsi ilivyoshughulikia maandamano ya hapo awali.
Bw Masengeli aliwaambia maafisa wa polisi wanaoendesha shughuli zao wakivalia kama raia kujitambulisha kila mara huku akibainisha kuwa huduma ya polisi ina nia ya kushughulikia masuala ya usalama nchini na kuhakikisha usalama wa Wakenya.
Kuhusu Gen Z, alisema, ujumbe wao umesikika na ni jukumu la polisi kutofautisha kati ya Gen Z na wanaotumia maandamano kusababisha fujo, uharibifu wa mali na vurugu ambazo haziruhusiwi kisheria.
Alisema watakaotumia maandamano kushiriki uhalifu watashughulikiwa kwa uthabiti na kutoa wito kwa umma kushirikiana na polisi kudumisha usalama wa nchi.
Pia aliwahimiza polisi kukumbatia ubunifu katika kukabiliana na uhalifu unaojitokeza kama vile uhalifu wa mtandaoni, ugaidi, itikadi kali za kikatili na ujangili.
Alisisitiza kujitolea kwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) kushirikiana na idara nyingine ndani ya mfumo wa Haki ili kuwahudumia Wakenya vyema na kutaja Idara ya Mahakama, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) na magereza kama washirika wakuu.
Mkutano huo ulioangazia, “Hali ya Usalama wa Kitaifa-Changamoto, Fursa na Mikakati” ulikusudiwa kupitia baadhi ya changamoto kubwa za usalama zinazoikabili nchi na zinazohitaji uangalizi wa haraka miongoni mwao kuongezeka kwa machafuko ya kiraia, uhalifu wa mtandaoni na vitendo vya kigaidi.
Wakati huo huo, Katibu wa Masuala ya Kigeni, Dkt Korir Sing’oei ameitaka Serikali kudhibiti mikusanyiko na maandamano nchini, akisema inasababisha changamoto za kiuchumi.
Katika taarifa kwenye akaunti yake ya X, katibu huyo, alisema maandamano hayo yameathiri uchumi, hasa katika sekta ya kibinafsi.
“Moja ya sababu za kudhibiti na kukabiliana na maandamano na machafuko ni kwamba waandamanaji hawazingatii gharama za vitendo vyao,” alisema.
“Gharama hizi zinabebwa na watu wengine – sekta ya kibinafsi. Kama vile uchafuzi wa mazingira, maandamano yenye vurugu yanahitaji kudhibitiwa kabla ya kusababisha gharama zisizoweza kurekebishika.

BWANYENYE Yagnesh Devani aliyekwepa kushtakiwa kwa miaka 15 katika kashfa ya Sh7.6 bilioni ya mafuta ya ndege amezuiliwa katika Gereza la Viwandani kwa siku 13 baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma (DPP) kupinga kuachiliwa kwa dhamana.
Hakimu mkuu wa mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Milimani Thomas Nzioki aliagiza Devani afungwe katika gereza hilo baada ya kukwepa kufika kortini kwa miaka 15.
Kibali cha kumtia nguvuni kilitolewa 2009 na alikuwa akisakwa na polisi wa humu nchini na wale wa kimataifa.
Devani aliyetorokea Uingereza 2009 aliwasilisha kesi katika Mahakama Kuu Ulaya akipinga kurudiswa nchini akidai “magereza ya Kenya ni machafu kupindukia.”
Pia alieleza mahakama Uingereza kwamba “hatapata haki katika mahakama za Kenya endapo atarudishwa kufunguliwa mashtaka ya ulaghai wa kiubiki 126,000,000 za mafuta ya ndege ya thamani ya Sh7.6 bilioni.”
Devani alikanusha mashtaka 11 aliyoshtakiwa ya ulaghai wa mafuta ya ndege kiubiki 19,186,130 ambayo kampuni yake Triton Petroleum Company ilidaiwa kuilaghai kampuni ya ng’ambo ya Emirates National Oil Company iliyoko nchini Singapore.
Bw Nzioki aliamuru idara ya urekebishaji tabia imhoji Devani kubaini masuala kadhaa kuhusu tabia yake tangu arudishwe nchini Januari 23, 2024 na kufunguliwa mashtaka mbele ya hakimu mwandamizi Robinson Ondieki.
Pia hakimu aliagiza idara ya urekebishaji tabia ichunguze pasipoti zake.
Na wakati huo huo, Bw Nzioki aliamuru afisi ya DPP ichunguze na kuwasilisha orodha ya wakurugenzi wa Triton kufikia 2009 ili mahakama ijue ikiwa itamwagiza Bw Devani kujibu mashtaka kwa niaba hiyo ya Triton.

KAMATI ya Bunge la Kitaifa kuhusu Uteuzi imekataa kumwidhinisha Waziri Mteule wa Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Turathi Stella Soi Lang’at kwa wadhifa huo.
Kwenye ripoti iliwasilishwa bungeni Jumatano alasiri, kamati hiyo iliyowapiga msasa mawaziri 20 wateule kwa siku nne wiki jana, hata hivyo, imeidhinisha uteuzi wa wengine 19.
Wabunge hao walifikia uamuzi wa kumkataa Bi Lang’at baada ya kutoridhishwa na uwezo na ufahamu wake wa masuala yanayohusu wizara aliyopendekezwa kuhudumu.
“Ijumaa wiki jana, alipofika mbele yetu, Bi Lang’at alionekana kama mtu asiyeelewa kabisa masuala yanayohusu Wizara hiyo licha ya kwamba yeye ni mwanamke. Mara sio moja alitatanika alipokuwa akijibu maswali kutoka kwa wanachama wa kamati yetu. Hii ndio maana tumeamua kwa kauli kumkataa,” akasema Mbunge wa Saboti Caleb Amisi, ambaye ni mwanachama wa kamati hiyo.
Hata hivyo, kamati hiyo imeidhinishwa uteuzi wa mawaziri wateule wafuatao katika nyadhifa walizoteuliwa:
Profesa Kithure Kindiki (Usalama), Dkt Debra Barasa (Afya), Alice Wahome (Ardhi), Julius Migos (Elimu), Soipan Tuya (Ulinzi) na Eric Muuga (Maji).
Wengine ni pamoja na Aden Duale (M inazingira), Davis Chirchir (Barabara) Margaret Nyambura (ICT), John Mbadi (Fedha), Salim Mvurya (Biashara), Rebecca Miano (Utalii), Opiyo Wandayi (Kawi), Kipchumba Murkomen (Michezo), Hassan Ali Joho (Uchumi wa Baharini), Alfred Mutua (Leba), Wycliffe Oparanya (Vyama vya Ushirika) na Justin Muturi (Utumishi wa Umma).
Endapo wabunge watakubaliana na mapendekezo ya kamati hiyo, Rais atahitajika kupendekeza mtu mwingine kwa Wizara ya Jinsia kuchukua mahala pa Bi Lang’at.
Aidha, atawateua rasmi mawaziri hao wateule baada bunge kuwapitisha.
HABARI KWINGINEKO DUNIANI.
1.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken amesema kiongozi mkuu mpya wa kisiasa wa Hamas aliyechaguliwa na kundi hilo kuchukua nafasi ya Ismail Haniyeh aliyeuwawa nchini Iran ana mamlaka ya kuhakikisha makubaliano ya kusitisha mapigano yanapatikana katika vita vya Israel na Hamas vinavyoendelea katika Ukanda wa Gaza.
2.Mkuu wa jeshi Bangladesh ametangaza kuwa serikali ya mpito itakayoongozwa na mshindi wa Tuzo ya Nobel Yunus Muhammad, itaapishwa hapo kesho usiku. Muhammad atawasili kesho bangladesh kutoka Paris, ili kujaribu kurejesha uthabiti katika nchi hiyo baada ya maandamano yaliyomuondoa madarakani Waziri Mkuu Sheikh Hasina.
3 Daktari mmoja nchini Ujerumani anakabiliwa na mashtaka ya jinai kwa kuwauwa wagonjwa 4 wazee, waliokuwa katika uangalizi wake mnamo mwezi Juni na Julai. Daktari huyo mwenye umri wa miaka 39 anadaiwa kuwa alijaribu kuzichoma nyumba za wagonjwa hao baada ya kuwauwa, ili apoteze ushahidi. Wazee hao walikuwa kati ya umri wa miaka 72 na 94.
4.Kundi la Hamas limemteua mkuu wake katika Ukanda waa Gaza Yahya al-Sinwar kuchukuwa nafasi ya marehemu Ismail Haniyeh kama kiongozi mkuu wa kisiasa, mnamo wakati kanda ya Mashariki ya Kati ikijiandaa kwa uwezekano wa wimbi jipya la mashambulizi ya Iran na washirika dhidi ya Israel.
DHAKA,BANGLADESHI
Sheikh Hasina alipoitisha kikao cha usalama na mgogoro ili kumaliza machafuko yanayoendelea nchini Bangladesh siku ya Jumapili, alionekana kutokukubali kuwa muda wake umeisha kama waziri mkuu.
Ndani ya saa chache, alifurushwa kwa nguvu za umma- kwa kweli, ni wachache wangeweza kutabiri kasi ya kuondoka kwake.
Alishauriwa na familia yake kutoroka na sio maafisa wakuu wa usalama, Radio Fortune Africa iliambiwa na mwanawe.
Bi Hasina alichukua uamuzi wakati muafaka, kisha umati wa watu uliingia katika makazi yake ndani ya saa chache baada ya kutoroka.
Kikao cha Kamati ya Usalama ya Kitaifa – kilichoitishwa Jumapili asubuhi – kiliwakutanisha Waziri Mkuu pamoja na wakuu watatu wa kijeshi wa nchi hiyo, maafisa wakuu wa usalama na polisi.
Shinikizo dhidi ya Waziri Mkuu lilikuwa likiongezeka kwa wiki kadhaa huku maandamano ya kuipinga serikali yakiendelea kote nchini.
Mamia wameuawa katika ghasia mbaya zaidi kuwahi kutokea nchini Bangladesh tangu vita vyake vya kupata uhuru mwaka 1971.
Siku ya Jumapili pekee, takribani watu 90 walipoteza maisha, wengi wao wakiwa waandamanaji waliopigwa risasi na vikosi vya usalama – lakini pia kuna idadi kubwa ya polisi waliouawa na umati wa watu.Bangla imeelezwa na maafisa kwamba Sheikh Hasina alitaka kuwepo mambo mawili. Maandalizi ya kuondoka nchini na kusalia madarakani kwa nguvu hadi dakika ya mwisho.
Viongozi wa kijeshi hawakukubali. Siku ya Jumapili, waandamanaji walichangamana na askari waliokuwa mitaani na maafisa wengine wa jeshi katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Baada ya kuona hali hiyo, maafisa wakuu wa jeshi waligundua kuwa mambo yako nje ya udhibiti wao.
Wakuu wa jeshi mmoja baada ya mwingine katika mkutano huo walimwambia Waziri Wkuu kwamba wanajeshi hawawezi kuwafyatulia risasi raia – lakini wanaweza kutoa msaada wa kiusalama kwa polisi, duru ziliiambia BBC.
Pia ilibainika baadaye kuwa wakuu wa polisi, walilalamika kuwa walikuwa wakiishiwa na risasi.
Hata hivyo Sheikh Hasina, hakutaka kusikiliza na hakuna mtu aliyekuwa tayari kupingana naye ana kwa ana.
Baada ya mkutano, mwandishi wake wa habari aliwasilisha ujumbe wake wa dharau. Aliwaita waandamanaji hao “magaidi” na kuwataka watu kuwapinga wale aliowataja kuwa “wachomaji moto.”
Vikosi vya usalama vilihofia kuwa baada ya muda mfupi vinaweza kukabiliwa na hali inayokaribia kuwa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe.
gChanzo cha picha,Reuters
Maelezo ya picha,Ghasia ziliongezeka siku ya Jumapili. Hapa muandamanaji anakimbia karibu na kituo cha polisi kilicho chomwa moto na waandamanaji mjini Dhaka
Picha za ghasia za Jumapili zilikuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii huku idadi ya waliofariki ikiongezeka mara kwa mara.
Picha za vijana waliokuwa na majeraha ya risasi, waliopigwa risasi na polisi na wanachama wa tawi la vijana la chama tawala cha Awami League, zilikuwa zikizua hasira zaidi.
Wakati mapigano hayo yalipodhihirika kuwa ni makali, viongozi wa wanafunzi waliwasilisha wito wa maandamano makubwa ya siku moja huko Dhaka, na kuishangaza serikali.
Taarifa za kijasusi zilionyesha kuwa madai ya wanafunzi yalikuwa yakiungwa mkono zaidi na zaidi na maelfu ya watu walikuwa wakipanga kuingia kwenye mji mkuu siku iliyofuata.
Taarifa hizo ziliashiria kuwa iwapo vikosi vya usalama vitajaribu kuwazuia waandamanaji, kungekuwa na umwagaji mwingine wa damu. Kwa hiyo mkuu wa jeshi Waker-Uz-Zaman aliamua kuzungumza na waziri mkuu tena.
Vyanzo vya kuaminika vilisema wakuu watatu wa jeshi walikutana naye Jumapili jioni na wakamweleza kwa upole kwamba hali ilikuwa inaendelea kuwa tete zaidi na zaidi, na maelfu ya watu wanatarajiwa kuingia Dhaka Jumatatu asubuhi na wasingeweza kumhakikishia usalama wa makazi yake.
Sheikh Hasina hakukubali ushauri wao, lakini waandishi wa habari huko Dhaka walisema walikuwa wakihisi kuwa serikali inabadilika. Kufikia Jumapili usiku, polisi hawakuwepo katika maeneo mengi na vizuizi vingi vya usalama havikuwa na mtu.
Siku ya Jumatatu asubuhi, umati mkubwa wa watu ulikuwa umeanza safari ya kuelekea Dhaka. Jenerali Zaman alikuwa kwenye makazi ya Bi Hasina kwa mara nyingine tena akimwelezea uzito wa hali hiyo. Watu walikuwa wakivunja amri ya kutotoka nje na vurugu zilikuwa tayari zimeanza.
Polisi walikuwa wakiondolewa sehemu nyingi za Dhaka na Jenerali Zaman alimwambia kuwa hawawezi kuzuia umati wa watu kufika Gono Bhaban, makao rasmi ya Waziri Mkuu katika mji mkuu, kwa muda mrefu zaidi.
Katika hatua hii, wakuu wa kijeshi waliamua kuwaita wanafamilia kuingilia kati.
Polisi na wakuu wa kijeshi walifanya mazungumzo na dada yake Sheikh Hasina, Rehana Siddiq, kuona kama angeweza kumshawishi dada yake mkubwa kuondoka.
“Viongozi hao walifanya mazungumzo na Sheikh Rehana kwenye chumba kingine, wakamtaka amweleze Sheikh Hasina. Kisha Sheikh Rehana akazungumza na dada yake mkubwa, lakini Sheikh Hasina alidhamiria kushikilia madaraka,” Gazeti la kila siku Prothom Alo la lugha ya Kibengali lilisema.
Kisha mwana wa kiume wa Bi Hasina, Sajeeb na binti yake Saima, ambao wote wanaishi nje ya nchi, walizungumza naye kwa simu na kumsisitiza kwamba aondoke. Wakati wa mazungumzo haya ya kifamilia, mkuu wa jeshi, ambaye ni jamaa na Bi Hasina kwa ndoa, alikuwepo muda wote.
“Mama yangu hakutaka kuondoka nchini hata kidogo. Ilibidi tumshawishi,” Sajeeb Wazed Joy aliambia BBC siku ya Jumanne, na kuongeza kuwa mama yake alianza kufikiria kujiuzulu Jumamosi jioni.
“Sisi wanafamilia tulimsihi, tukamsihi, hili ni kundi la watu, wako nje kwa vurugu na watakuuwa na tunahitaji kukupeleka kwenye usalama. Muda wa waandamanaji kufika katika kasri lake ndio uliokuwa umebaki tu. Hatimaye, waliondoka tu bila maandalizi yoyote.
“Nilimpigia simu jana huko Delhi. Yuko imara lakini amevunjika moyo sana. Amekatishwa tamaa sana na watu wa Bangladesh.”
wChanzo cha picha,Reuters
Maelezo ya picha,Watu wakitembea karibu na magari yaliyoharibiwa katika kituo cha polisi huko Dhaka siku ya Jumanne
Jumatatu asubuhi, vyanzo vya habari vilisema, Sheikh Hasina aliwasiliana na maafisa wa serikali mjini Delhi, India kuomba hifadhi.
Ushauri kutoka India, nchi mshirika mkubwa katika maisha yake yote ya kisiasa, ulikuwa ni kwamba aondoke.
Siku moja kabla, inaelezwa kuwa Marekani iliwaambia maafisa wa Wizara ya mambo ya nje ya India kwamba wakati wa Bi Hasina umekwisha. Hana chaguo.
Lakini mara tu alipokubali kwa kusita kusaini hati za kuachia wadhifa wake, bado kulikuwa na swali la jinsi ya kumtoa nje ya nchi kwa usalama.
Afisa mmoja mkuu wa jeshi ambaye hakutaka jina lake litajwe, aliiambia BBC Bangla kwamba ni Kikosi Maalumu cha Usalama, Kikosi cha Walinzi wa Rais na baadhi ya maafisa wakuu wa jeshi katika makao makuu ya jeshi waliojua muda ambao Sheikh Hasina alitia saini barua ya kujiuzulu na kupanda helikopta ya kijeshi ambayo ingeweza mpeleke nje ya makazi yake.
Kila kitu kilifanyika kwa usiri mkubwa.
Mnamo saa nne unusu kwa saa za eneo hilo (05:00GMT), mamlaka ilizima intaneti ili kuzuia habari kuhusu mienendo ya Sheikh Hasina kuenea kwenye mitandao ya kijamii.
Ilifunguliwa tu baada ya yeye kutoroka.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya juu vya jeshi, mipango iliwekwa ili kumfikisha Sheikh Hasina uwanja wa ndege akiwa salama.
Kulikuwa na wasiwasi kwamba msafara wake unaweza kushambuliwa, kwa hivyo njia nzima iliwekwa ulinzi na mahali pa kuondokea pakalindwa.
Lakini ikaonekana kuwa haikuwa salama kumpitisha barabarani, kwa hiyo helikopta ilitumiwa kumuondoa kwenye makazi yake.
Hadi wakati wa kuondoka, Sheikh Hasina alisitasita kuingia, mtoto wake alisema.
“Alitaka shangazi yangu ndio aondoke,” mwanawe alisema. “Mama yangu hakutaka kupanda helikopta. Nilikuwa kwenye simu, nikimshawishi mama yangu, nikimwambia shangazi, lazima waondoke wote wawili.
Mara baada ya kupanda, walisafirishwa kutoka Gono Bhaban hadi kwenye ndege ya Bangladeshi Air Force C-130 Hercules ambayo ilikuwa imetayarishwa.
Sajeeb Wazed Joy anasema anaamini walikwenda Agartala, mji mkuu wa jimbo la mashariki mwa India la Tripura na walisafirishwa kwa ndege kutoka huko hadi Delhi.
India tayari ilikuwa imefahamishwa na kukubali kumpokea, maafisa walisema.
Duru nyingine zinasema alichukuliwa kwa helikopta hadi uwanja wa ndege huko Dhaka, kisha akasafirishwa kwa ndege hadi Delhi.
Karibu saa sabu na nusu mchana kwa saa za huko, Bi Hasina, dada yake na mbunge mkuu wa chama cha Awami, Salman Fazlur Rahman, walihamishwa kutoka kwenye helikopta na kuwekwa kwenye ndege iliyowapeleka Delhi, maafisa walisema.
Video kwenye mitandao ya kijamii ilionyesha masanduku manne au matano yakisubiri kupakiwa. Mali nyingine alizoziacha zilikuwa zikisukumwa na umati wa watu waliovamia makazi yake, akiwa angani.
Saa kadhaa baadaye, ndege hiyo ilitua Delhi. Huko Dhaka, mtandao ulikuwa umerejea na kote Bangladesh, sherehe zilikuwa zikianza kuashiria mwisho wa utawala wa miaka 15 wa Sheikh Hasina.
Mwanamke ambaye aliyetazamwa kama mwanademokrasia lakini baadaye akalaaniwa na watu wengi kama dhalimu, alikimbia kama mkimbizi huku mitandao ikiwa imezimwa.
KIPENGA CHA MICHEZO
Je, wajua kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya kwenye mashindano ya kimataifa kama vile Olimpiki inayoendelea, ni maafisa wa vikosi vya usalama nchini humo?




Mshindi wa medali ya shaba mbio za Mita 800 Mjini Paris, Moraa, mwanariadha wa mbio za mita 100 Ferdinand Omanyala, mkimbiaji wa mbio za Mita 1500 Timothy Cheruiyot, mrusha mkuki Julius Yego, pamoja na wanariadha wa zamani kama vile David Rudisha, Ezekiel Kemboi Asbel Kiprop, Catherine Ndereba na Hellen Obiri ni baadhi ya wanaoiwakilisha uwanjani kwenye riadha, na vilevile kuimarisha usalama huku wakihudumu katika vikosi mbalimbali kama vile polisi, magereza, ulinzi na polisi wa utawala.




Wanariadha hao wamekuwa wakitunukiwa na serikali ya Kenya kwa kuvikwa madaraka pindi wanapoiletea nchi hiyo sifa kwenye mashindano ya kimataifa.


5.Bingwa wa Olimpiki Joshua Cheptegei na mwanariadha mwenzake wa Uganda Jacob Kiplimo wamejiondoa kutoka ushiriki wa mbio za mita 5,000 kwenye michezo ya Olimpiki. Cheptegei na Kiplimo wanasema ni wachovu baada ya kushiriki mbio za mita 10,000 ambazo Cheptegei alinyakua dhahabu. Bingwa huyo atashiriki mbio za marathon pia pamoja na Eliud Kipchoge wa Kenya na Kenenisa Bekele wa Ethiopia.

“Nilikuwa tayari kuwakilisha Kenya lakini siku zote sikuchaguliwa.”
Taifa la Bahrain linazidi kusherehekea ushindi wa kihistoria wa Winfred Mutile Yavi, Mwanariadha wa Bahrain aliyezaliwa Kaunti ya Makueni nchini Kenya ambaye alitwaa dhahabu katika mbio za mita 3000 upande wa wanawake.
Yavi alihamisha uraia wake kutoka Kenya hadi Bahrain mwaka 2016, akitaja kutokuwepo kwa nafasi za kutambua kipaji chake Kenya kama sababu ya kubadilisha uraia.


“Nilikuwa tayari kuwakilisha Kenya lakini siku zote sikuchagulia.”
Mwaka 2016, nilikuwa tayari kuiwakilisha Kenya, lakini nilipokosa nafasi iliniuma sana. Nilifanya mazoezi mengi na nilikuwa na matumaini ya matokeo bora, lakini sikufanikiwa. Hapo ndipo nilipata nafasi ya kuiwakilisha Bahrain”, alisema.
Yavi Mwenye umri wa miaka 24, aliweka rekodi mpya ya Olimpiki ya muda wa 8:52.76.
Mwanariadha chipukizi kutoka Nchini Kenya,Faith Cherotich ameonyesha usogora wake katika michezo ya olimpiki Hadi kubandikwa Faith Kadogo.Faith alinyakua nishani ya shaba katika mbio za mita 3000 kuruka viuzi na kidimbwi cha maji,mahindi alikua Winfred Mutile Yavi wa Bahrain.



KipengaChaMichezo
TheHeartBeatofAfrica
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.