Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Muhtasari
- Mkasa wa binti kubakwa Tanzania, uchunguzi umefikia hatua nzuri- Msemaji wa polisi
- Uchunguzi wa jinai waanzishwa dhidi ya viongozi wa upinzani Venezuela
- Wapalestina kumi wauawa katika ghasia za Ukingo wa Magharibi
- ‘Tumepata Medali zetu za dhahabu kwa njia safi sana’ – China
- Kwa nini Kamala Harris alimchagua Tim Walz
- Kamala Harris amchagua Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake
- Israel na Hezbollah zafanya mashambulizi ya kujibizana huku mvutano ukizidi kupamba moto
- Hifadhi ya maiti Marekani yatozwa faini ya $950m katika kesi ya miili iliyooza
- Waandamanaji wakamatwa Nigeria kwa kupeperusha bendera ya Urusi
- Bunge la Bangladesh lamevunjwa – Ofisi ya Rais
- Muhammad Yunus: Mpinzani mkuu wa Sheikh Hasina ambaye waandamanaji wanataka awe mshauri mkuu wa serikali Bangladesh
- Maandamano Bangladesh: Tunachokijua kufikia sasa
- Wadukuzi wa Korea Kaskazini wanajaribu kuiba siri za nyuklia na kijeshi, Marekani, Uingereza zasema
- Ukiritimba wa Google katika urambazaji mtandaoni ni kinyume cha sheria- jaji wa Marekani
- Rais Biden akutana na maafisa usalama wa Marekani wakati hofu ya mashambulizi ya Iran ikiongezeka
- Wakenya washinda medali 3 Paris 2024
- Wanajeshi wa Marekani wajeruhiwa katika shambulizi nchini Iraq
- Shangwe nchini Bangladesh baada ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina ku
- Mkasa wa binti kubakwa Tanzania, uchunguzi umefikia hatua nzuri- Msemaji wa polisi
Chanzo cha picha, - Polisi TanzaniaMaelezo ya picha,Msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania David MisimeJeshi la polisi nchini Tanzania limesema uchunguzi kuhusu mkasa wa kubakwa kwa binti mtanzania ulifanywa na kundi la wanaume watano umefikia pazuri na kuwataka wananchi kuwa na subira.Muda mfupi uliopita Mwandishi wa BBC, Martha Saranga amezungumza na Msemaji wa jeshi la polisi nchini Tanzania DavLinkid Misime na kwanza amemuuliza uchunguzi umefikia hatu agani?Hata hivyo taasisi mbalimbali zimekemea tukio hilo ikiwemo chama cha mawakili tanzania TLS, na tume ya kutetea haki za binadamu wakitaka sheria kali zichukuliwe.Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa nchini Tanzania Dr Stagomena Tax amenukuliwa na chombo cha habari nchini Tanzania akisema Serikali haitavumilia uvunjaji wa sheria,na atakayebainika kutekeleza ukatili huo atachukuliwa hatua stahiki.Mwishoni wa wiki iliyopita, video ikimuonesha binti akifanyiwa vitendo vya ukatili na kundi la vijana watano ilisambaa nchini Tanzania na kuzua gumzo na hasira miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Sikiliza hapa mahojiano hayo na msemaji wa polisiMshirikishe mwenzako, Mkasa wa binti kubakwa Tanzania, uchunguzi umefikia hatua nzuri- Msemaji wa pUchunguzi wa jinai waanzishwa dhidi ya viongozi wa upinzani Venezuela
Chanzo cha picha,Reuters - Maelezo ya picha,María Corina Machado, ambaye alizuiwa kuwania wadhifa huo, ameweza kuunganisha upinzaniMwanasheria mkuu wa Venezuela, mshirika wa karibu wa Rais Nicolás Maduro, ametangaza kuanzisha uchunguzi dhidi ya viongozi wa upinzani María Corina Machado na Edmundo González kwa madai ya “kuchochea uasi”.Viongozi hao wa upinzani hapo awali walitoa wito kwa vikosi vya usalama “kuunga mkono watu” na kupuuza maagizo yoyote ya kukandamiza maandamano dhidi ya serikali.Mvutano umekuwa ukiongezeka tangu halmashauri ya kusimamia uchaguzi, ambayo inashirikiana kwa karibu na serikali, kumtangaza Bw Maduro kuwa mshindi bila kutoa hesabu za kina za upigaji kura hadharani.Upinzani umetoa hesabu zake kuthibitisha kuwa Bw González alishinda uchaguzi huo na sio Rais Maduro kama ilivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi.Siku ya Jumapili, gazeti la Washington Post lilisema limekagua zaidi ya karatasi 23,000 za kujumlisha kura zilizokusanywa na upinzani – ambazo ni sawa na 80% ya mashine za kupigia kura kote Venezuela.Gazeti la The Post lilihitimisha kwamba Bw González “huenda alipata kura zaidi ya mara mbili ya Rais Nicolás Maduro”.Nicolás Maduro: Kiongozi ambaye ameapa kushinda uchaguzi ‘kwa njia yoyote ile’Mshirikishe mwenzako, Uchunguzi wa jinai waanzishwa dhidi ya viongozi Wapalestina kumi wauawa katika ghasia za Ukingo wa Magharibi
Chanzo cha picha,Getty Images. - Vikosi vya Israel vimewaua Wapalestina 10 katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina.Jeshi la Israel linasema lilifanya mashambulizi mawili tofauti ya anga kaskazini mwa eneo hilo likiwalenga wanachama wa makundi yenye silaha.Kumekuwa na ongezeko la ghasia katika Ukingo wa Magharibi tangu kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza, vilivyochochewa na shambulio baya la Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba.Wizara ya afya ya eneo hilo inasema Wapalestina wasiopungua 600 – wanachama wa makundi yenye silaha, wapiganaji na raia – wameuawa katika matukio yanayohusiana na migogoro katika Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki.Takriban Waisrael 17, wakiwemo maafisa 12 wa vikosi vya usalama, pia wameuawa katika Ukingo wa Magharibi, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.Msemaji wa Mamlaka ya Palestina Nabil Abu Rudeinah alilaani ghasia za hivi majuzi, pamoja na madai ya mateso na unyanyasaji wa wafungwa wa Kipalestina katika jela za Israel, kama hatua ya “kuvuka mistari yote ya rangi nyekundu”.Soma pia:Yafahamu baadhi ya mashambulizi makubwa yaliyoshuhudiwa na Iran katika miaka ya hivi karibuniNi nani atakayekuwa mrithi wa Haniyeh, na kwa nini jina lake linafichwa?Mfahamu kiongozi wa Hamas aliyewanyima usingizi IsraeliMshirikishe mwenzako, Wapalestina kumi wauawa katika ghasia za Ukingo wa ‘Tumepata Medali zetu za dhahabu kwa njia safi sana’ – Uchina yakashifu mashaka ya kutumia dawa za kusisimua misuli
Chanzo cha picha,Reuters”Shaka yoyote ni mzaha tu. Mafadhaiko hutufanya tuwe na nguvu zaidi,” Qin Haiyang – sehemu ya kikosi cha waogeleaji wanne wa timu ya wanaume ya 4x100m ya Uchina iliyoweka historia baada ya ushindi wao usio na kifani dhidi ya Marekani siku ya Jumatatu anasema.Kuonekana kwa kauli hiyo ya kukaidi kwa Qin kulikuja mwisho wa wakati ambao umekuwa changamoto kwa Uchina kwenye bwawa.Baadhi ya waogeleaji mashuhuri nchini – akiwemo Qin na mwenzake Sun Jiajun- wameangaziwa baada ya madai mengi ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli, na kufuatiwa na madai tata ya Marekani kwamba Shirika la Kupambana na Dawa za Zilizopigwa marufuku michezoni Duniani (Wada) lilikuwa likificha ushahidi.Walikuwa miongoni mwa waogeleaji 23 wa Kichina ambao waliripotiwa kupata matokeo chanya ya kutumia dawa hizo katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo.Na ingawa waogeleaji wa Kichina wamepimwa dawa za kulevya mara mbili zaidi ya mataifa mengine mwaka huu kabla ya kuelekea Paris, matokeo yao yamekabiliwa na shaka.Mara tu baada ya hafla ya medley siku ya Jumatatu, Adam Peaty wa Timu ya GB alifungua shutuma kwa timu ya Uchina, akisema“hakuna faida ya kushinda ikiwa haujashinda kwa haki”.Mshirikishe mwenzako, ‘Tumepata Medali zetu za dhahabu kwa njia safi sana’ – Uchina yakashifu mashaka ya kutumia dawa za kusis Kwa nini Kamala Harris alimcWatu wachache walikuwa na Gavana wa Minnesota Tim Walz kwenye orodha zao za awali za makamu wa rais wa Kamala Harris, lakini vyombo vya habari vya Marekani sasa vinaripoti kwamba atakuwa kwenye tiketi ya Democratic.Mwalimu huyo wa zamani wa shule ya upili na mkufunzi wa kandanda alivutia watu wa chama cha Democratic kwa mtindo wake wa kustaajabisha na uwezo wake wa kupambana na Donald Trump bila kuonekana kuwa mkali sana.Kumtaja Trump kama na mgombea mwenza wake kama ‘watu wa ajabu” likawa neno la chama cha Democratic katika muda wa siku chache – na sasa ni sehemu ya kawaida ya hotuba ya Harris.Ingawa Minnesota sio mojawapo ya majimbo yenye mapambano makali ya kura , Kambi ya Harris inaweza kutumaini kuwa Walz atawapa njia ya kuvuka mpaka wa katikati ya magharibi katika maeneo kama vile Wisconsin na Michigan, ambayo itasaidia kuamua mshindi wa uchaguzi huu.Walz pia ana rekodi ya kutunga sheria za ustawi katika jimbo lake huku akiitetea kwa njia ambayo wapiga kura wa wastani na huru wanaweza kuelewa. Katika kazi yake ya awali kama mbunge, aliweza kushinda katika wilaya ambayo ina idadi kubwa ya wapiga kura wa vijijini na wa Republican.Soma pia:Kocha wa zamani wa mpira wa miguu na mwalimu – sasa ndiye mgombea mwenza wa HarrisMshirikishe mwenzako, Kwa nini Kamala Harris alimchagua Tim Walz
- Saa 6 zilizopitaHabari za hivi punde,Kamala Harris amchagua Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake -ripotiKamala Harris amemchagua gavana wa Minnesota Tim Walz, kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa rais wa Marekani, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.Bi Harris na mgombea mwenza wake wanatarajiwa kuanza ziara ya kampeni katika majimbo yanayosadikiwa kuwa na ushindani mkali, mkutano wa kwanza ukipangiwa kufanyika huko Philadelphia baadaye leo.Kura ya maoni ya hivi punde ya kituo cha CBS, mshirika wa BBC wa Marekani, inawaonyesha Bi Harris na Trump wakiwa katika kinyang’anyiro kikali kitaifa, huku Mgombea huyo wa chama cha Democratic akiongoza kwa pointi moja dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump.Maelezo zaidi:Kamala Harris ni nani, makamu wa rais ambaye Biden anamuunga mkono kuwa rais?Je, Kamala Harris ana uwezo na sifa za kumshinda Trump?Nani anaweza kuwa mgombea mwenza wa Kamala Harris?Kijiji kidogo cha India kinachodai Kamala Harris ni ‘wao’Mshirikishe mwenzako, Kamala Harris amchagua Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake -ripoti
- Saa 6 zilizopitaIsrael na Hezbollah zafanya mashambulizi ya kujibizana huku mvutano ukizidi kupamba moto
Chanzo cha picha,IDFIsrael inasema imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya kile ilichosema ni “jengo linalofanana kama la kijeshi” linalotumiwa na kundi la waasi la Hezbollah kusini mwa Lebanon.Wizara ya afya ya Lebanon imesema watu wanne waliuawa katika shambulio hilo katika mji wa Maifadoun, karibu kilomita 30 kutoka mpaka wa Israel.Vyanzo vya usalama vililiambia shirika la habari la AFP kwamba watu hao wanne walikuwa wapiganaji wa Hezbollah. Katika jibu dhahiri, kundi hilo lilianzisha mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye miji ya kaskazini mwa Israel, na kuwajeruhi watu wawili.Inakuja huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya Israel na Hezbollah, na Iran ambayo inaunga mkono kundi hilo.Wiki iliyopita, shambulio la anga la Israel lilimuua kamanda mwandamizi wa Hezbollah Fuad Shukr katika kitongoji cha kusini mwa mji mkuu wa Lebanon Beirut, katika kile maafisa wa Israel walichokiita “kutokomeza kwa kutegema habari za kijasusi”.Maafisa wa Israel wanasema alihusika na shambulio la roketi katika eneo la Milima ya Golan inayokaliwa na Israel mwezi uliopita na kuua watoto na vijana 12. Hezbollah imekanusha kuhusika na shambulio hilo.Saa chache baada ya Shukr kuuawa, kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh aliuawa katika mji mkuu wa Iran Tehran – Iran ililaumu Israel kwa shambulio hilo .Hezbollah na Iran zimeapa kulipiza kisasi juu ya vifo hivyo, na hivyo kuzua hofu kwamba mapigano ya kujibizana yanaweza kuchochea mzozo mkubwa zaidi wa kikanda.Nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Marekani, zimewataka raia kuondoka Lebanon haraka iwezekanavyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo alisema Jumanne kwamba alikuwa anafanya kazi kuhakikisha kuwa Hezbollah haisababishi ongezeko kubwa la jibu lake kutokana na kifo cha Shukr.Shambulio la Israel dhidi ya Maifadoun lilitekelezwa na ndege za kivita, na liliongozwa na mashirika ya kijasusi, Jeshi la Ulinzi la Israel lilisema katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii.Kujibu, Hezbollah ilifyatua kile ilichokiita “kundi” la ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel, na kuwajeruhi watu wawili katika mji wa kaskazini wa Mazra’a. Lakini chanzo katika kundi hilo kililiambia shirika la habari la Reuters kwamba shambulio hilo halikuwa sehemu ya majibu yake kwa kifo cha Shukr.Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na timu yake ya juu ya usalama wa taifa siku ya Jumatatuhuku wasiwasi wa mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya Israel ukiongezeka.Mshirikishe mwenzako, Israel na Hezbollah zafanya mashambulizi ya kujibizana huku mvutano ukizidi ku - Hifadhi ya maiti Marekani yatozwa faini ya $950m katika kesi ya miili iliyooza
Chanzo cha picha,CBSHifadhi moja ya maiti Marekani ambapo miili 190 iliyoharibika ilipatikana imeagizwa kulipa $950m (£746m) kwa familia za waathiriwa.Hifadhi hiyo kwa jina Return to Nature, katika mji wa Penrose, Colorado, ilikuwa imewapa jamaa waliokuwa wakiomboleza majivu bandia badala ya mabaki ya wapendwa wao.Jaji aliamuru malipo hayo katika kesi ya madai, lakini hakuna uwezekano wa kulipwa kwa vile wamiliki wa hifadhi hiyo, Jon na Carie Hallford, walikuwa katika matatizo makubwa ya kifedha.Wawili hao pia hawakuhudhuria vikao. Bw Hallford yuko kizuizini, huku mkewe akiwa nje kwa dhamana.”Sitapata hata senti kutoka kwao, kwa hivyo, sijui, inasikitisha kidogo,” Crystina Page, ambaye aliajiri hifadhi hiyo ya maiti i kuchoma mabaki ya mtoto wake mnamo 2019, aliiambia Associated Press.Bi Page, ambaye alibeba kile alichodhani
WASHINGTON D.C, Amerika
MGOMBEA urais wa Chama cha Democrat Kamala Harris amemteua Gavana wa Minnesota Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa urais wa Novemba 5, mwaka huu.
Waltz anasifiwa kama mwenye kipawa cha usemi na mtetezi sugu wa sera endelevu nchini Amerika.
Anatarajiwa kumsaidia Harris kuvutia kura katika maeneo ya mashambani na kura za Waamerika weupe.
Hata hivyo, maafisa wa kikosi cha kampeni za makamu huyo wa rais walidinda kutoa maelezo zaidi kuhusu suala hilo.
Walz, 60, ambaye ni shujaa wa zamani wa Jeshi la Kitaifa la Amerika na mwalimu, alichaguliwa kama Mbunge katika Bunge la Wawakilishi mnamo 2006 ambako alihudumu kwa miaka 12 kabla ya kuchaguliwa Gavana wa Jimbo la Minnesota mnamo 2018.
Akihudumu kama Gavana, Walz alitetea ajenda endelevu zilizojumuisha utoaji wa lishe shule bila kulipiwa, malengo ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, punguzo la ushuru kwa watu wa tabaka la kati na kuanzishwa kwa sera za wafanyakazi kulipwa wakiwa likizoni katika jimbo la Minnesota.

Walz ametetea haki za uzazi za wanawake
Aidha, kwa muda mrefu, Walz ametetea haki za uzazi za wanawake, masilahi ya wadau katika sekta ya kilimo na kuunga mkono haki kuhusu umiliki wa bunduki na raia.
Aliendeleza utetezi huo alipohudumu kama mwakilishi wa eneo la mashambani katika Bunge la Wawakilishi.
Harris, ambaye ni binti ya wahamiaji kutoka Jamaica na India, anatarajia kuwa mwanasiasa kutoka jimbo ambalo wapiga kura wake wengine huunga mkono chama cha Republican katika chaguzi za urais, atamfaa zaidi.
Jimbo hilo la Minnesota pia linapakana na majimbo mawili ya Wisconsin na Michigan, ambayo hushindaniwa kwa ukaribu na chama hicho na kile cha Republican.
Majimbo kama hayo huonekana kama muhimu katika kuamua mshindi katika chaguzi za urais zilizopita sawa na uchaguzi ujao.
Walz anaonekana na wengi kama mwenye ujuzi wa kuwavutia wapiga kura weupe na wale wa maeneo ya mashambani ambao katika miaka michache iliyopita wamemuunga mkono mgombeaji wa chama cha Republican Donald Trump.
Harris alimteua Walz badala ya gavana wa Pennsylvania Josh Shapiro, ambaye alitarajiwa kumpa ushindi katika jimbo hilo muhimu.
Makamu huyo wa Rais aliteuliwa mgombeaji urais wa Chama cha Democrat baada ya bosi wake, Rais Joe Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro cha kutafuta muhula wa pili Ikuluni mwezi jana.
Tangu wakati huo, amechangiwa fedha nyingi za kufadhili na kutoa mwelekeo mpya katika kampeni dhidi ya Trump.
Jumanne jioni, Harris alitarajiwa kujitokeza na mgombea mwenza wake katika mkutano wa kampeni katika mji wa Philadelphia.
Inatarajiwa kuwa tajriba pana ya Walz jeshini na ufanisi wake kama kocha wa kandanda katika shule ya upili itavutia wapiga kura ambao hawataki Trump ahudumu kwa muhula wa pili katika Ikulu ya White House.
Aidha, imeripotiwa kuwa Gavana huyo wa Minnesota alikuwa akiungwa mkono na aliyekuwa Spika wa Bunge Nancy Pelosi, aliyechangia pakubwa katika kumshawishi Rais Biden, 81, ajiondoe kinyang’anyironi.
Harris na Walz sasa watakabana koo na Trump na mgombea mwenza wake JD Vance, ambaye pia ni mwanajeshi wa zamani, katika uchaguzi wa Novemba.
donald trump
joe biden
Josh Shapiro
Kamala Harris
Minnesota
Tim Walz

GAVANA wa Kaunti ya Bungoma, Kenneth Lusaka, Jumatatu, Agosti 5, 2024 alisimamisha kwa muda kikao cha Seneti akitaka Seneta aliyemdhalilisha kwa kumtusi kumuomba msamaha.
Bosi huyo wa gatuzi la Bungoma alifika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu Ugatuzi ambapo alitakiwa kujibu maswali kuhusu akaunti za Benki ya Commercial (KCB) zinazoendeshwa na kaunti yake.
Hata hivyo, kabla ya kikao hicho kuanza, Gavana Lusaka alieleza Kamati hiyo kwamba Seneta wa Kisii, Richard Onyonka, alimkosea heshima kwa kumwita ‘mpumbavu” na kumtaka aombe radhi.
Haya yalijiri kufuatia ripoti kuwa usimamizi wa kaunti ya Bungoma ulitumia kitita cha Sh25 milioni kwa urembeshaji, ikiwemo kununua maua wakati wa Sikukuu ya Madaraka, mwaka huu, 2024.
Kulingana na Gavana Lusaka, madai hayo hayana msingi wowote kumruhusu Seneta wa Kisii kumshambulia kwa maneno mazito.
“Mialiko hutokana na ripoti ya mdhibiti wa bajeti, ndiposa tuko hapa. Lakini wakati ambapo suala hata halijashughulikiwa na kamati yoyote, mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, mdhibiti bajeti wala EACC, ni uvumi mitaani. Kisha tunalitumia kuunda taswira fulani si haki kabisa ukijua kuwa nitafika hapa,” alisema Gavana Lusaka.
“Mimi ni binadamu na nilihisi nimedhalilishwa kwa kuitwa mpumbavu. Nataka Seneta aombe radhi kwa matamshi hayo.”
Akijitetea, Seneta Onyonka alifafanua kwamba matamshi yake yalitokana na ghadhabu kuhusu ubadhirifu wa fedha uliokithiri Kaunti ya Bungoma akisema hakulenga nafsi ya Gavana.
“Gavana Lusaka wewe ni mwanamme ninayeheshimu mno, hakuna shaka kuhusu hilo. Nilipoona ripoti kuwa Gavana wa Bungoma alinunua maua ya Sh25 milioni nilipandwa na mori. Haikuwa kukuhusu, kauli hiyo haikukulenga. Ikiwa kauli hiyo ilikukwaza ninaomba radhi kwa dhati,” alisema Seneta Onyonka.
“Lakini nitakwambia leo Gavana, nikija leo katika Kituo cha Afya Bungoma nilipokuwa tukiandamana na mwenyekiti, tulipopata wanawake wamelala sakafuni, nakwambia bado nitasema, ‘hawa ni wapumbavu wanaofanya kazi katika kituo kama hiki.’ Mahali tunapowachukulia watu wetu maskini kwa kiwango duni zaidi kuliko tunavyowatendea mbwa wetu.”
Alisema matamshi yake hayakumlenga Gavana Lusaka bali “mifumo mibovu ya taifa langu, Kenya ambapo unasimamia karibu bilioni moja za kufadhili huduma za matibabu na wanawake wote katika kituo hicho…”
“Ukija hapa, huji ili tukueleze jinsi tulivyo safi nawe una hatia. Ni mdahalo jinsi ulivyosema. Uhalisia ni kuwa tulikuwa Bungoma na watu walikuwa wamelala sakafuni tulipoingia. Ukweli ni ule ule ila matamshi, tukizingatia hadhi yako, ninataka kusema samahani kwamba nilikusawiri hivyo.”
Kamati hiyo inayoongozwa na Seneta wa Kaunti ya Wajir, Abass Mohamed, ilielezwa kuwa, Gavana Lusaka vilevile amenukuliwa akitoa matamshi ya kudhalilisha viongozi wengine wakiwemo maseneta.
“Natoka kaunti anayotoka Gavana. Juzi alisema ukiona kobe juu ya meza bila shaka kuna mtu aliyeiwekelea hapo. Lakini sitaichukulia binafsi kwa sababu hatimaye kobe yuko hapa. Tusichukulie mambo kwa kibinafsi,” alisema Seneta Onyonka.
bungoma
Mpumbavu
Richard Onyonka

MIAKA miwili iliyopita, Boniface Mwaka, 63, kutoka eneo la Ndithini, Kaunti ya Machakos, aliambiwa kwamba jicho lake la kulia lingepofuka, baada ya kugundulika kuugua ukungu wa macho, yaani cataracts.
Kabla ya hapo, Bw Mwaka ambaye alistaafu kama mtumishi wa umma, asema kwamba kwa miaka kadhaa alikumbwa na changamoto ya kusoma bila kutumia miwani.
“Tatizo la kuona pia lilikuwa likinikumba wakati wa usiku hasa kila nilipomulikwa na taa ya gari. Kando na hayo, jicho langu lilikuwa na maumivu ya macho kila mara,” aeleza.
Masaibu haya yalimlazimu kusaka huduma za kimatibabu katika hospitali kadhaa ambapo alikaguliwa na madaktari mbali mbali kabla ya kushauriwa kutafuta matibabu zaidi.
“Kila mara, nililazimika kuzuru hospitali ya macho ya Nairobi’s City Eye Hospital kufuatia ushauri wa wataalam,” aeleza.
Kulingana na Dkt George Ohito, mtaalam wa upasuaji wa kutibu maradhi ya ukungu wa macho,hali hii hutokea protini inapojiunda kwenye lenzi ya jicho na kulifanya lionekane kana kwamba imefunikwa na wingu.
“Wingu hili huzuia mwangaza kuingia jichoni na kumsababisha mgonjwa kupoteza uwezo wa kuona kwa kiwango fulani,”aeleza.
Kuna aina tofauti za ukungu wa macho, kulingana na mtaalam huyu.
“Kuna ukungu wa macho unaosababishwa na umri. Aidha kuna aina ingine inayofahamika kama congenital cataracts, ambapo huwakumba watoto wachanga hasa baada ya kukumbwa na maambukizi, majeraha au matatizo ya kukua kabla ya kuzaliwa au hata kukumbwa na hali hii wanapokua,” aeleza Dkt Ohito.
Mwanamume akijizatiti kusoma kwa sababu ya matatizo yaliyosababishwa na ukungu wa macho. Picha|Maktaba
Kisha kuna secondary cataracts, hali ambayo hujitokeza kutokana na matatizo ya kiafya kama vile kisukari au kuathiriwa na kemikali za sumu, aina fulani ya dawa, mwangaza au mnururisho.
“Pia, kuna traumatic cataracts. Aina hii hutokea baada ya jicho kukumbwa na jeraha,” aeleza Dkt Ohito.
Baadhi ya ishara za hali hii, asema mtaalam huyu, ni pamoja na kushindwa kuona vizuri, kushindwa kutofautisha rangi fulani, matatizo unapoendesha gari hasa wakati wa usiku, huku wakati mwingine mgonjwa akishindwa kuona vizuri kwenye mwangaza mwingi.
“Pia, ukishauriwa na daktari kubadilisha aina ya miwani unayotumia kila mara, unapaswa kufanyiwa uchunguzi zaidi kwani hii pia ni ishara,” aeleza.
Kulingana na Shirika la Afya Duniani WHO, watu milioni 28 duniani kote wanakumbwa na matatizo ya kuona, miongoni mwao wakiwa Wakenya 750,000.
Kati ya watu milioni 39 wanaokumbwa na tatizo la upofu duniani kote, 224,000 ni Wakenya.
Aidha, asilimia 80 ya visa vya upofu nchini Kenya ni kutokana na sababu ambazo zaweza kuzuiwa hasa kupitia utambuzi na tiba ya mapema, na mojawapo ya sababu kuu ni ukungu wa macho.
Hali hii yaweza kuzuiwa?
Kutokana na sababu kuwa chanzo kikuu cha hali hii hakijatambuliwa vyema, wataalam wanasema kwamba hakuna njia kamili ya kuzuia hali hii.
Dkt Ohito asema, kutokana na sababu kuwa ukungu wa macho na matatizo mengine ya macho kama vile glaucoma huwakumba sana watu wenye umri mkubwa, ni muhimu kufanyiwa uchunguzi wa macho kila wakati.
“Hii ni muhimu hasa ikiwa uko katika hatari ya kukumbwa na hali hii, au iwapo kuna historia ya maradhi haya kwenye familia,” asema.
Kulingana na wataalam, watu wenye umri mkubwa wanapaswa kukaguliwa na daktari wa macho angalau mara mbili kwa mwaka.
Utafiti unaonyesha kwamba watu wenye umri mkubwa wamo katika hatari kubwa ya kupofuka kutokana na ugonjwa huu.
Lakini licha ya kuwa maradhi haya kusababisha upofu miongoni mwa asilimia moja ya Wakenya, kuna teknolojia mpya ya upasuaji unaofahamika kama Phacoemlusification (phaco) surgery.
“Upasuaji huu ni teknolojia ya kisasa ya kutibu upofu unaosababishwa na maradhi ya ukungu wa macho. Utaratibu huu unahusisha matumizi ya mwangaza wa leza ambapo lenzi ya jicho lililoathirika linaondolewa na kuwekwa jipya, katika upasuaji unaochukua dakika 15 pekee,” aeleza Dkt Ohito.
Bw Mwaka ni mmoja wa watu walionufaika na tiba hii. Julai 7, 2024 , alibahatika kufanyiwa upasuaji huu.
“Nilibahatika kufanyiwa utaratibu huu ambapo dakika chache baadaye jicho langu lilikuwa sawa,” aeleza Bw Mwaka.
Dkt Ohito asema kwamba habari njema ni kwamba Wakenya wengi wanaokumbwa na tatizo hili wanatafuta matibabu mapema, na kulingana naye, teknolojia hii ni habari njema kwa wagonjwa humu nchini.
Ikiwa una wasiwasi kuhusu gharama ya matibabu, mtaalam huyu asema kwamba usiogope kwani itakugharimu tu kati ya Sh30,000 na Sh60,000.
congenital cataracts
Dkt George Ohito
Nairobi’s City Eye Hospital
Phacoemlusification surgery
traumatic cataracts
Ukungu wa macho
WHO
Je, eneo la Mashariki ya Kati linakaribia kugubikwa na vita vikubwa?

6 Agosti 2024, 07:09 EAT
Eneo la Mashariki ya Kati limeingia katika kipindi hatari, likisubiri jibu la Iran kwa mauaji ya Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu mjini Tehran, na jibu la Hizbullah nchini Lebanon kwa mauaji ya kiongozi wa pili wa Hizbullah, Fouad Shukr, katika viunga vya kusini mwa mji mkuu, Beirut.
Khamenei aamuru mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya Israel

Nchini Iran, wito wa jibu kali la kijeshi dhidi ya Israel umetolewa na viongozi wakuu wa utawala wa Iran.
Ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, Ayatollah Ali Khamenei, ameamuru shambulio la moja kwa moja dhidi ya Israel na kutayarishwa mipango ya mashambulizi na ya kujihami katika tukio ambalo vita na Israel vitaenea.
Khamenei alisema kwamba “kulipiza kisasi cha damu ya shahidi Haniyeh ni jukumu la Iran kwa sababu aliuawa katika ardhi yake.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi wa Iran, Meja Jenerali Mohammad Bagheri, aliapa kuijibu Israel na kusema: “Taasisi ya Kizayuni itajuta.” Kwa mujibu wa ripoti katika vyombo vya habari vya Marekani, Iran inafikiria kufanya mashambulizi yaliyoratibiwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani katika Haifa na Tel Aviv, kwa uratibu wa makundi ya Syria, Yemen na Iraq.
Mjini Beirut, Katibu Mkuu wa Hezbollah Hassan Nasrallah aliapa kuilipiza kisasi Israel kwa mauaji ya kamanda wa kijeshi wa chama hicho, Fouad Shukr.
Alisema makabiliano hayo na Israel yameingia katika awamu kubwa ya vita, na kuongeza kuwa “jibu kwa Israel haliepukiki, na litakuwa kubwa, la kweli na la haki.
Nasrallah alisisitiza katika hotuba yake wakati wa mazishi ya Fouad Shukr kwamba “adui na wale walio nyuma yake lazima wangoje majibu yetu yasioepukika, na hakutakuwa na mjadala au mijadala.
Kuna siku na uwanja kati yetu … Tunatafuta jibu la kweli, lisilo rasmi…
Eneo hili linakabiliwa na vita vikubwa ambavyo vitakuwa na athari ambazo wengine hawatambui kuhusu mustakabali wa adui… Kujisalimisha kwa Hamas au Lebanon ni suala lisilowezekana.
Nasrallah aliwahutubia Waisraeli kwa vitisho akisema, “Cheka kidogo kwa sababu utalia sana na hujui umeingia kwenye mtego gani.”
Mjini Sanaa, Abdul-Malik al-Houthi, kiongozi wa kundi la Ansar Allah nchini Yemen, aliapa kujibu mauaji ya Ismail Haniyeh, akisema: “Lazima kuwe na jibu la kijeshi kwa uhalifu uliotekelezwa na Israel.’’
Israel inajiandaa kwa hatua kali za kiusalama

Nchini Israel, Mamlaka ya Utangazaji ya Israel inasema kuwa mamlaka imechukua hatua za kipekee za usalama na kuimarisha hali ya tahadhari kwa kutarajia jibu kutoka kwa Iran, Hamas na Hezbollah.
Jeshi lilighairi likizo ya wanajeshi katika vitengo vya mapigano na kuweka mfumo wa ulinzi wa anga katika hali ya tahadhari ili kuzuia tishio lolote kutoka kaskazini, kusini, mashariki au magharibi.
Channel 12 ilisema kuwa huduma ya usalama ya Shin Bet imeimarisha kiwango cha usalama kwa waziri mkuu na mawaziri wa serikali.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Israel, Israel inaweza kukabiliwa na vita vya pande nyingi ambavyo vinaweza kusukuma Mashariki ya Kati katika vita vya kikanda, na lazima ijiandae kukabiliana na mashambulizi ya makombora na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kutoka Lebanon na Yemen, na hata kutoka Iran, ambayo itajaribu kuhamasisha makundi yenye silaha kutoka Iraq na Syria hadi upande wa kaskazini kuunga mkono Hezbollah.
Mchambuzi wa kijeshi wa Israel Amos Harel, akiiandikia Haaretz, alisema kuwa Israel inakabiliwa na dharura ya kuongezeka kwa vita hivyo vinavyotishia kuzua mzozo mkubwa zaidi wa kikanda.
Alisema, “Tel Aviv inatumai kuudhibiti mzozo huo na kuuzuia kuzidi kuwa vita kamili kwenye eneo la kaskazini, kwa sababu Netanyahu havutiwi na makabiliano kamili na Hezbollah na eneo la Gaza tayari linawaka moto.”
Mchambuzi huyo wa masuala ya kijeshi alihitimisha kuwa serikali na jeshi la Israel hawana suluhu za kutuliza hali na kujiondoa katika mgogoro wa kimkakati wa kaskazini na miji ya mpakani ambayo imehamisha wakazi wake tangu Oktoba mwaka jana, na kwamba hatari ya kugeuka kuwa vita vikubwa dhidi ya mauaji ya Haniyeh huko Tehran imetimia.
KIPENGA CHA MICHEZO
Wakati Michezo ya Olimpiki ya kisasa ilipoanza huko Athene, Ugiriki mwaka 1896, ilikuwa ni michezo ya kujifurahisha bila wanamichezo wataalamu au tuzo za pesa.
Lakini jijini Paris, Ufaransa msimu huu wa kiangazi, baadhi ya wana michezo huenda wakapata pesa, kwa wale ambao watashinda katika Olimpiki hiyo.
Wana michezo ya Olimpiki wanaweza kupata pesa kutoka vyanzo mbalimbali; wafadhili, tuzo za kifedha zinazotolewa na nchi zao, na sasa kwa mara ya kwanza, tuzo za pesa zinazotolewa kwenye mashindano yenyewe.
Lakini si kila mchezo utapata pesa, na hilo limesababisha mabishano kuhusu njia bora ya kugawanya mapato ambayo michezo hiyo inazalisha.
Ndondi na mbio tu

Kati ya michezo 32 iliyoshindaniwa huko Paris 2024, zawadi ya pesa itatolewa katika michezo miwili tu – mbio na ndondi.
Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Mbio, lilitoa tangazo la kushangaza mwezi Aprili kwamba washindi wa medali za dhahabu huko Paris 2024, watapokea dola za kimarekani 50,000 kwa atakayeshinda.
Mwezi mmoja baadaye, Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBA), lilisema pia litatoa zawadi ya dola 100,000 kwa mabingwa wa Olimpiki – ingawa robo moja ya pesa hizo itakwenda kwa mashirikisho ya kitaifa ya wakimbiaji na robo nyingine kwa makocha wao.
Katika michezo yote miwili, washindi wa medali za fedha na shaba watapata kiasi kidogo cha pesa, huku washindi katika ndondi wakituzwa hadi mshindi wa tano.
Zawadi ya pesa hazitoki moja kwa moja kutoka kamati ya Olimpiki, bali kutoka kwa mashirika mbalimbali yanayosimamia michezo hiyo.
Shirikisho la Kimataifa la Michezo ya Mbio linatumia baadhi ya fedha ambazo inapokea kutoka kwa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), kama sehemu ya mapato yanayotokana na Michezo ya Olimpiki. Hapo awali, pesa hizi zilitumika zaidi katika maendeleo ya wakimbiaji.
Pesa zitawasaidia?

Olga Korbut, nguli wa mazoezi ya viungo wa Sovieti ambaye alishinda medali nne za dhahabu na mbili za fedha wakati wa maisha yake ya Olimpiki, alilazimika kuuza medali zake tatu kwa dola 333,500 mnamo 2017.
Kuna njia nyingine nyingi ambazo wanamichezo hupata pesa. Wengi huzawadiwa na nchi zao. Singapore inaaminika kuwa ndio taifa linalotoa zawadi zaidi, kila mmoja wa washindi wa medali za dhahabu hupata dola 750,000.
Kwa wenyeji, Ufaransa, washindi hupewa dola 87,000. Wanamichezo wa Morocco wako juu zaidi kwani hupewa dola 200,000. Marekani kupitia mfuko wake wa “Operation Gold” hutoa dola 37,500.
Baadhi ya nchi, kama vile Uingereza, hazitoi zawadi yoyote ya fedha.
Timu ya GB hutoa ufadhili kwa wanariadha wakati wa kuelekea katika Olimpiki na wale wenye nafasi kubwa ya kushinda dhahabu hupata hadi dola 28,000 kwa mwaka.
Ingawa pesa hizi si kidogo lakini haziwafanyi wana michezo hao kuwa matajiri, kama wale wanamichezo matajiri maarufu duniani.
Changamoto za kifedha

Mcheza gofu wa Uhispania Jon Rahm ndiye mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi Paris 2024 kulingana na orodha ya kila mwaka ya matajiri wa michezo iliyochapishwa na Forbes.
Jarida hilo linakadiria kuwa alipata dola milioni 218 mwaka uliopita, huku pesa nyingi zikitoka katika safari ya gofu ya LIV iliyofadhiliwa na Saudia.
Haishangazi, mchezaji wa pili anayelipwa vizuri zaidi ni nyota wa mpira wa vikapu wa Marekani – Lebron James. Anaaminika kulipwa dola milioni 128.
Kwa wana michezo wa chini, kushinda medali katika Olimpiki kunaweza kuwasaidia kuwapa nyongeza inayohitajika katika mapato yao. Mara nyingi huwa na mikataba inayosema watapokea bonasi kutoka kwa wafadhili ikiwa watashiriki na kushinda.
Mikataba hii mara nyingi ni siri, lakini ilifichuliwa wakati wa mzozo wa kisheria kati ya Nike na New Balance mwaka 2016, mwanamichezo wa Marekani Boris Berian alitarajia kupokea dola 150,000 ikiwa angeshinda dhahabu kwenye Olimpiki.
Kuna wanariadha wengi ambao wanatatizika kufanikiwa. Utafiti uliofanywa nchini Australia miaka michache iliyopita uligundua 40% ya wana michezo ya Olimpiki ya 2032 wanafanya kazi za muda au wameajiriwa mikataba ya kudumu.
Utafiti wa hivi karibuni wa Kamati ya Olimpiki na Olimpiki ya Walemavu ya Marekani uligundua 26.5% ya wana michezo wake wa sasa wanapata chini ya dola 15,000 kwa mwaka.

Medali ya mshindi wa mwaka huu ina gramu 505 za fedha na gramu sita za dhahabu (medali za dhahabu sio dhahabu tupu tangu 1912) na thamani yake ni dola 950.
Lakini mabingwa wa Olimpiki wa Paris watakuwa na matumaini kwamba kumbukumbu zao za ushindi zitakuwa na thamani zaidi.
All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.