Afrika Leo Mchana -Agosti 6,2024

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Natumai U buheri wa afya Popote pale ulipo duniani,kwa moyo mkunjufu na mikono miwili, Agosti 6 2024,Hujambo na karibu. Naitwa Cantona Joseph.

Muhtasari

  • Muhammad Yunus: Mpinzani mkuu wa Sheikh Hasina ambaye waandamanaji wanataka awe mshauri mkuu wa serikali Bangladesh
  • Maandamano Bangladesh: Tunachokijua kufikia sasa
  • Wadukuzi wa Korea Kaskazini wanajaribu kuiba siri za nyuklia na kijeshi, Marekani, Uingereza zasema
  • Ukiritimba wa Google katika urambazaji mtandaoni ni kinyume cha sheria- jaji wa Marekani
  • Rais Biden akutana na maafisa usalama wa Marekani wakati hofu ya mashambulizi ya Iran ikiongezeka
  • Wakenya washinda medali 3 Paris 2024
  • Wanajeshi wa Marekani wajeruhiwa katika shambulizi nchini Iraq
  • Shangwe nchini Bangladesh baada ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina kukimbia nchi

Moja kwa moja

Kamala Harris atarajiwa kumtangaza mgombea mwenza wakeKamala HarrisChanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Kamala Harris atafanya kampeni katika miji saba wiki hii, akianza na mkutano wa Philadelphia Jumanne.Makamu wa Rais Kamala Harris anatarajiwa kumtangaza mgombea mwenza wake leo Jumanne, katika hatua itakayohitimisha uvumi wa ni nani atakayekuwa mgombea mwenza wake wakati Marekani ikielekea kwenye uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.Bi Harris aliwahoji washindani kadhaa wakuu huko Washington DC mwishoni mwa juma, wakiwemo Josh Shapiro, Tim Walz na Mark Kelly.Mgombea mwenza atakayemchagua ataungana naye katika ziara ya siku tano ya miji saba wiki hii huku Bi Harris akiendeleza kampeni yake katika majimbo muhimu yanayotarajiwa kushuhudia kinyang’anyiro kikali.Kura ya maoni ya hivi punde ya kituo cha CBS, mshirika wa BBC wa Marekani, inawaonyesha Bi Harris na Trump wakiwa katika kinyang’anyiro kikali kitaifa, huku Mgombea huyo mtarajiwa wa chama cha Democratic akiongoza kwa pointi moja dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump.

Maelezo zaidi:Kamala Harris ni nani, makamu wa rais ambaye Biden anamuunga mkono kuwa rais?Je, Kamala Harris ana uwezo na sifa za kumshinda Trump?Nani anaweza kuwa mgombea mwenza wa Kamala Harris?Kijiji kidogo cha India kinachodai Kamala Harris ni ‘wao’

Wimbi la Siasa-Bangladesh….

  1. Muhammad Yunus: Mpinzani mkuu wa Sheikh Hasina ambaye waandamanaji wanataka awe mshauri mkuu wa serikali BangladeshMuhammad YunusChanzo cha picha,Getty Images. Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Muhammad Yunus, ambaye waandamanaji wanataka ateuliwe kuwa mshauri mkuu wa serikali ya mpito ya Bangladesh, amekuwa akichukuliwa kwa muda mrefu na Sheikh Hasina kama mpinzani wa kisiasa.Mzee huyo mwenye umri wa miaka 84, anayejulikana kimataifa kama “benki kwa maskini”, anasifiwa kwa kuwaondoa mamilioni ya watu kutoka kwenye umaskini kutokana na matumizi yake ya kwanza ya mikopo midogo midogo.Prof Yunus na Benki yake ya Grameen walitunukiwa kwa pamoja Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kazi yao nzuri mwaka wa 2006.Lakini Bi Hasina alikuwa amemtaja Prof Yunus mara kwa mara kama “mnyonyaji damu” wa maskini na akashutumu Benki yake ya Grameen kwa kutoza viwango vya juu vya riba.Mwezi Januari, mahakama ya Bangladesh ilimhukumu Prof Yunus kifungo cha miezi sita jela kwa kukiuka sheria za kazi za nchi hiyo, ambazo Prof Yunus amekosoa kuwa hukumu ilichochewa kisiasa.Unaweza kusoma;Sheikh Hasina: Waziri Mkuu wa Bangladesh aliyekimbia nchi ni nani?
  2. Saa 1 iliyopitaMaandamano Bangladesh: Tunachokijua kufikia sasaMuandamanajiChanzo cha picha,ReutersKuna hali ya sintofahamu miongoni mwa wananchi wengi wa Bangladesh kuhusu kitakachotokea baadaye, siku moja baada ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina kulazimishwa kujiuzulu na kuikimbia nchi kufuatia maandamano makubwa.Hasina, 76, anaaminika kuwa bado yuko katika nchi jirani ya India, lakini uvumi umeenea kwamba anaweza kuwa anajiandaa kwenda katika nchi nyingine ya kigeni.Siku ya Jumatatu, mkuu wa jeshi la Bangladesh aliahidi kwamba serikali ya mpito itaundwa hivi karibuni, lakini hakutoa maelezo kuhusu nani anaweza kuiongoza. Viongozi wa wanafunzi wanasema hawatakubali serikali inayoongozwa na jeshi, wakishinikiza mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Muhammad Yunus kuwa mshauri mkuu wa baraza jipya la mawaziri.Baadhi yao wamemtaka rais wa Bangladesh Mohammed Shahabuddin kulivunja bunge ifikapo saa 15:00 kwa saa za huko leo (09:00 GMT), na wameonya kwamba “watachukua hatua kali” ikiwa matakwa yao hayatatekelezwa.Endelea kuwa nasi tunapokuletea habari za hivi punde na uchambuzi kutoka Bangladesh.
  1. zilizopitaMaandamano Bangladesh: Tunachokijua kufikia sasaMuandamanajiChanzo cha picha,Reuters
  2. Kuna hali ya sintofahamu miongoni mwa wananchi wengi wa Bangladesh kuhusu kitakachotokea baadaye, siku moja baada ya Waziri Mkuu Sheikh Hasina kulazimishwa kujiuzulu na kuikimbia nchi kufuatia maandamano makubwa.Hasina, 76, anaaminika kuwa bado yuko katika nchi jirani ya India, lakini uvumi umeenea kwamba anaweza kuwa anajiandaa kwenda katika nchi nyingine ya kigeni.Siku ya Jumatatu, mkuu wa jeshi la Bangladesh aliahidi kwamba serikali ya mpito itaundwa hivi karibuni, lakini hakutoa maelezo kuhusu nani anaweza kuiongoza. Viongozi wa wanafunzi wanasema hawatakubali serikali inayoongozwa na jeshi, wakishinikiza mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Muhammad Yunus kuwa mshauri mkuu wa baraza jipya la mawaziri.Baadhi yao wamemtaka rais wa Bangladesh Mohammed Shahabuddin kulivunja bunge ifikapo saa 15:00 kwa saa za huko leo (09:00 GMT), na wameonya kwamba “watachukua hatua kali” ikiwa matakwa yao hayatatekelezwa.Endelea kuwa nasi tunapokuletea habari za hivi punde na uchambuzi kutoka Bangladesh.
  3. Saa 2 zilizopitaWadukuzi wa Korea Kaskazini wanajaribu kuiba siri za nyuklia na kijeshi, Marekani, Uingereza zasemaUdukuziChanzo cha picha,Getty Images
  4. Wadukuzi wa Korea Kaskazini wanajaribu kuiba siri za nyuklia na kijeshi kutoka kwa serikali na makampuni binafsi duniani kote, Uingereza, Marekani na Korea Kusini zimeonya.Wanasema kundi hilo, linalojulikana kwa majina Andariel, Onyx Sleet na DarkSeoul, miongoni mwa mengine linalenga vyombo vya ulinzi, anga, nyuklia na uhandisi ili kupata taarifa za siri, kwa lengo la kuendeleza mipango na malengo ya kijeshi na nyuklia ya Pyongyang.Kundi hilo limekuwa likitafuta habari katika sekta mbalimbali, kuanzia urutubishaji wa urani hadi mizinga, nyambizi na torpedo na limelenga Uingereza, Marekani, Korea Kusini, Japan, India na nchi nyingine, kwa mujibu wa mwandishi wa usalama wa BBC Gordon Corera.Iinashukiwa kushambulia vituo vya anga vya Marekani, NASA na makampuni ya ulinzi.Onyo la hali ya juu kuhusu kundi hili linaonekana kuwa ishara kwamba shughuli yao, ambayo inachanganya ujasusi na faida, inatia wasiwasi mamlaka kwa sababu ya athari zake kwa teknolojia nyeti na maisha ya kila siku.Marekani inasema kundi hilo linafadhili shughuli zake za ujasusi kupitia operesheni dhidi ya taasisi za afya nchini humo.Unaweza kusoma;Wachezaji wa mchezo wa video wanaovujisha siri mtandaoniWalaghai wanavyoweza kukuibia akiba yako ya maishaUkiritimba wa Google katika utafutaji mtandaoni ni kinyume cha sheria- jaji wa MarekaniGoogleChanzo cha picha,Getty Images. Jaji wa Marekani ameamua kwamba Google ilikwenda kinyume cha sheria ili kukandamiza washindani wake na kudumisha ukiritimba wa urambazaji mtandaoni na utangazaji unaohusiana.Uamuzi wa kihistoria wa Jumatatu ni pigo kubwa kwa Alphabet, kampuni mama ya Google, na unaweza kurekebisha jinsi makampuni makubwa ya teknolojia yanavyofanya biashara.Google ilishtakiwa na wizara ya Haki ya Marekani mwaka 2020 kuhusu udhibiti wake wa takribani 90% ya soko la urambazaji mtandaoni.Ni mojawapo ya mashtaka kadhaa ambayo yamewasilishwa dhidi ya makampuni makubwa ya teknolojia huku mamlaka ya Marekani ikijaribu kuimarisha ushindani katika sekta hiyo.Kesi hii wakati fulani imeelezewa kuwa ni tishio kwa Google na mmiliki wake kutokana na utawala wake wa utafutaji na biashara ya utangazaji mtandaoni.Bado haijafahamika ni adhabu gani Google na Alphabet zitakabiliana nazo kutokana na uamuzi huo.Faini au masuluhisho mengine yataamuliwa katika kesi ya baadaye.
  5. Saa 5 zilizopita Rais Biden akutana na maafisa usalama wa Marekani wakati hofu ya mashambulizi ya Iran ikiongezekaRais Biden mkutanoniChanzo cha picha,White House/ XRais wa Marekani Joe Biden amekutana na timu yake ya masuala ya usalama wa taifa siku ya Jumatatu huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya Israel.Bw Biden alisema alikuwa amefahamishwa kuhusu maandalizi ya kuunga mkono Israel iwapo itashambuliwa, huku Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken akisema maafisa walikuwa wakifanya kazi “usiku na mchana” ili kuzuia kuongezeka.Mvutano uliongezeka wiki iliyopita baada ya mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh, ambapo Iran imeilaumu Israel na kuapa kulipiza kisasi “kikali”.Israel haijadai kuhusika na mauaji hayo.Nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Marekani na Uingereza, pia wamewaambia raia wao kuondoka Lebanon, kukiwa na hofu kuwa Hezbollah inaweza kuchukua hatua yoyote kujibu mashambulizi.Wakati wa mkutano wa Jumatatu, Bw Biden aliambiwa wakati na asili ya shambulio la Iran bado haijulikani, kulingana na tovuti ya habari ya Marekani ya Axios.Siku moja kabla, Bw Blinken aliripotiwa kuwaambia viongozi wenzake wa G7 kwamba Iran na Hezbollah zinaweza kushambulia Israel ndani ya saa 24 hadi 48.Unaweza kusoma;Yafahamu baadhi ya mashambulizi makubwa yaliyoshuhudiwa na Iran katika miaka ya hivi karibuniJe, eneo la Mashariki ya Kati linakaribia kugubikwa na vita vikubwa Wakenya washinda medali 3 Paris 2024WanariadhaChanzo cha picha,Getty ImagesBeatrice Chebet wa Kenya alishinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki mbio za mita 5,000.Amekuwa miongoni mwa wanawake mjini Paris baada ya kushinda mbio hizo ambazo zilimfanya bingwa wa mita 1500 Faith Kipyegon kupokonywa medali ya fedha kabla ya kurejeshewa.Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 alivuka utepe katika dakika 14 na sekunde 28.56 mbele ya Kipyegon aliyechukua nafasi ya pili.Kipyegon awali alinyang’anywa medali yake ya fedha baada ya kudaiwa kumzuia mwanariadha wa Ethiopia Gudaf Tsegay walipogongana katika kinyanganyiro hicho cha mita 5000.Hata hivyo, Kipyegon hatimaye alirejeshewa medali hiyo baada ya kulalamika kwa mamlaka.Wakati huohuo bingwa wa mbio za mita 800 Mkenya Mary Moraa alishinda medali ya shaba katika fainali ya mita 800 kwa wanawake, huku Tsige Duguma wa Ethiopia akishinda fedha nyuma ya Keely Hodgkinson wa Uingereza aliyenyakuwa dhahabu katika mbio hizo.
  6. Saa 7 zilizopitaWanajeshi wa Marekani wajeruhiwa katika shambulizi nchini IraqNdegeChanzo cha picha,Getty Images Wafanyakazi kadhaa wa Marekani wamejeruhiwa baada ya shambulio la roketi linaloshukiwa kutokea katika kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq, maafisa wa Marekani wamesema.Shambulio hilo limetokea huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akisema kuwa Mashariki ya Kati iko katika wakati mgumu baada ya mauaji ya viongozi wakuu wa Hamas na Hezbollah.Maafisa waliambia mshirika wa BBC, CBS News kwamba uwanja wa ndege wa Al Asad magharibi mwa Iraq ulishambuliwa na kwamba bado wanatathmini uharibifu uliofanyika.Bado hawajasema nani alitekeleza shambulio hilo.Vyanzo vya usalama viliiambia CBS kwamba roketi mbili za Katyusha zilirushwa kwenye kambi hiyo, na kwamba moja ilikuwa imeanguka ndani ya kambi hiyo.”Tunaweza kuthibitisha kwamba kuna tuhuma za shambulio la roketi leo dhidi ya vikosi vya Marekani na Muungano katika Al Asad, Iraq,” alisema msemaji wa Idara ya Ulinzi.”Dalili za awali zinaonesha kwamba wafanyakazi kadhaa wa Marekani walijeruhiwa.Wafanyakazi wanafanya tathmini ya uharibifu wa baada ya shambulio, “msemaji huyo aliongeza. Haijulikani ni wafanyikazi wangapi wa Marekani walijeruhiwa.Afisa mkuu wa jeshi la Marekani alisema hakuna majeraha makubwa, kama kupoteza miguu na mikono, ambayo yameripotiwa wakati huu, na hakuna wahudumu waliouawa.Rais Joe Biden alifahamishwa kuhusu shambulio hilo, afisa wa Ikulu ya White House alisema.Katika taarifa yake kwenye ukurasa wa X, Bw Biden alisema yeye na makamu wa rais Kamala Harris walipewa taarifa kuhusu “yanayojiri katika Mashariki ya Kati.”Unaweza kusoma;Kwa nini Marekani inakataa kuiunga mkono Israel katika kulipiza kisasi dhidi ya I Shangwe nchini Bangladesh baada ya Waziri Mkuu kuikimbia nchiWaandamanajiChanzo cha picha,Getty ImagesWaziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina amejiuzulu baada ya wiki kadhaa za maandamano mabaya dhidi ya serikali, na kukomesha zaidi ya miongo miwili ya kutawala siasa za nchi hiyo.Bi Hasina, 76, alikimbia nchi, akiripotiwa kutua India siku ya Jumatatu.Umati wa watu walioshangilia walijitokeza barabarani kusheherekea taarifa hizo, huku wengine wakivamia ikulu ya waziri mkuu, wakiripotiwa kupora na kuharibu sehemu za makazi yake ya zamani.Saa chache baada ya Bi Hasina kujiuzulu, Rais Mohammed Shahabuddin aliamuru kuachiliwa kwa waziri mkuu wa zamani Khaleda Zia aliyefungwa jela na wanafunzi wote waliokuwa wamezuiliwa wakati wa maandamano ya hivi karibuni dhidi ya mfumo wa upendeleo wa nafasi za kazi serikalini.Rais Shahabuddin alisema alikuwa ameongoza mkutano wa wakuu wa jeshi na wawakilishi wa kisiasa.Alisema serikali ya mpito itaundwa, uchaguzi mpya utaitishwa na amri ya kutotoka nje ya kitaifa kuondolewa.Mjini Dhaka siku ya Jumatatu, polisi na majengo mengine ya serikali yalishambuliwa na kuchomwa moto.Waandamanaji walijaribu kubomoa sanamu ya kiongozi wa uhuru Sheikh Mujibur Rahman, baba yake Bi Hasina.Vikosi vya jeshi na polisi vilisambazwa katika jiji lote. Huduma ya simu za mkononi iliripotiwa kukatika kwa saa kadhaa kabla ya kurejeshwa.Siku ya Jumatatu, waandamanaji walionekana wakibeba samani kutoka kwenye makazi ya waziri mkuu.Makumi waliripotiwa kuuawa siku ya Jumatatu, ingawa idadi kamili bado haijafahamika. Shirika la habari la AFP liliripoti idadi ya waliofariki kuwa 66, ingawa shirika la habari la Dhaka Tribune lilisema kuwa watu 135 wameuawa.Unaweza kusoma;Sheikh Hasina: Waziri Mkuu wa Bangladesh aliyekimbia nchi ni nani?Tazama: Waandamanaji wa Bangladesh wavamia makazi rasmi ya Waz

KIPENGA CHA MICHEZO

Paris, Ufaransa

SAA chache tu baada ya kupokonywa usindi wa nishani ya Fedha katika mbio za mita 5,000, Bingwa wa Dunia, Faith Kipyegon Jumatatu, Agosti 5, 2024 alipewa medali hiyo baada ya maafisa wa timu ya Kenya kushinda kesi dhidi ya madai kwamba Kipyegon alimsukuma Gudaf Tsegay wa Ethiopia ikibakia mizunguko miwili.

Mshindi, Beatrice Chebet katika mbio hizo alimaliza kwa muda wa dakika 14:28.56, mbele ya Kipgyegon aliyetumia muda wa dakika 14:29.60, huku Sifan Hassan wa Uholanzi akimaliza katika nafasi ya tatu kwa dakika 14:30.61.

Dhahabu ya Chebet ilikuwa ya pili ya Olimpiki kwa Kenya tangu Vivian Cheruiyot aibuke bingwa mnamo 2016 Michezo hiyo ilipofanyika Rio De Janeiro.

Muda mfupi baadaye, Mary Moraa alijinyakulia nishani ya Shaba katika mbio za mita 800 akitumia muda wa dakika 1:57.42.

Mshindi wa mbio hizo alikuwa Keely Hodgkinson wa Uingereza aliyemaliza kwa dakika 1:56.72, wakati Tsiye Duguma wa Ethiopia akishinda medali ya Fedha.

Matokeo haya yanadhihirisha kuwa Kenya haijashinda nishani ya dhahabu katika mbio hizo tangu Pamela Jelimo aibuke mshindi mnamo 2008.

Faith Kipyegon
Gudaf Tsegay
Olympics2024
Paris

BINGWA wa dunia mbio za mita 800, Mary Moraa ameridhika na medali ya shaba kwenye Michezo ya Olimpiki baada ya kumaliza mizunguko hiyo miwili katika nafasi ya tatu kwa dakika 1:57.42 mjini Paris nchini Ufaransa, Jumatatu, Agosti 5, 2024.

Moraa, ambaye alibanduliwa katika nusu-fainali katika makala ya 2020 mjini Tokyo, Japan mwaka 2021, alijaribu kufyatuka baada ya kupiga kona ya mwisho, lakini bila mafanikio.

Muingereza Keely Hodgkinson, ambaye alipata nishani ya fedha mjini Tokyo, alitwaa dhahabu kwa 1:56.72, huku fedha ikimwendea Muethiopia Tsige Duguma (1:57.15).

Moraa, ambaye ni bingwa wa Jumuiya ya Madola na alikuwa Mkenya pekee katika fainali Jumatatu, Agosti 5, 2024 baada ya Vivian Kiprotich na Lilian Odira kubanduliwa katika nusu-fainali, ni Mkenya wa tatu tu kupata medali katika 800m kwenye Olimpiki tangu mbio hizo zijumuishwe mashindanoni mwaka 1928.

Pamela Jelimo alinyakua dhahabu mwaka 2008 mjini Beijing, Uchina na kisha shaba mwaka 2012 mjini Londo, Uingereza.

Margaret Wambui aliambulia shaba katika makala ya 2016 mjini Rio de Janairo, Brazil.

Baada ya medali hizo mbili, Kenya sasa ni nambari 34 duniani kwa dhahabu moja na shaba moja kutoka orodha ya zaidi ya mataifa 200 yanayoshiriki.

Mary Moraa
olimpiki
Paris

Yego katika Fainali Urushaji mkuki.

Mkenya JULIUS YEGOOOOOOO!!🗣️🔊 Amefuzu katika fainali ya mchezo kurusha mkuki baada ya kurusha umbali wa mita 85.97,🇰🇪🎯

Hongera Kila la kheri, Bwana YouTube!

TeamKenya

HesabikaNaMabingwa

KipengaChaMichezo

TheHeartBeatofAfrica

Makala Maluum ya Olimpiki.

Kitendo cha Gudaf Tsigey kugonga na Faith Kipyego si Cha mara ya kwanza,ni hulka yake maana Muhabeshi Tsigey alifahamu fika kwamba huyu ndiye ana mbio kasi kuletea Kenya dhahabu. Na hivi ndivyo adui hutumia kila mbinu kukutoa Katika mstari wa hatima yako.Ukiwa Mkombozi wa familia…

Wacha nivute kumbukumbuku yako Tsigey alifanya kitendo hicho hicho mwaka Jana alipogundua Sifan Hassan wa uholanzi anamzidi kasi na hekima wakati huo,alijaribu kosa hilo kule Budapest mwaka Jana dhidi ya Faith, hii ni mbinu yake ya kijanja ni hulka yake,na tabia tabia ni ngozi
Hawa watu wapo,usiondoke Katika malengo Yako kwa kivutwa nje ya mstatili wa maono yako
Tazama hizi picha Tsigey anapowasili jukwani ana malengo fiche.Yeye hawazinkumimbia macho yake yote yapo kwa mpinzani wake.

KipengaChaMichezo

TheHeartBeatofAfrica

Wimbi La Siasa Kenya

NAIBU Rais Rigathi Gachagua sasa anasema kuwa yuko tayari kumkumbatia kisiasa Kinara wa Upinzani Raila Odinga na atamfikia ili washirikiane naye katika uchaguzi wa 2027.

Kauli hiyo ya Bw Gachagua inakuja wakati ambapo Bw Odinga ameanza kushirikiana kisiasa na Rais William Ruto na hata wandani wake wakateuliwa serikalini.

Naibu Rais alisema kuwa mwanasiasa huyo wa upinzani si adui wa Mlima Kenya jinsi ambavyo imekuwa ikifasiriwa huku akidai alipotoshwa ndiposa amekuwa akimpinga katika siasa za nchi.

“Mimi nimekuwa nikibeba ile dhana kwamba Bw Odinga sio mtu wa kuaminiwa au wa kushirikiana naye kisiasa. Ndiyo sababu sisi katika eneo la Mlima tumekuwa tukijitenga naye,” akasema Bw Gachagua.

Alikuwa akizungumza mnamo Jumapili usiku, Agosti 4, 2024 wakati alipokuwa akihojiwa na runinga ya Inooro ambayo inapeperusha matangazo yake kwa lugha ya Kikuyu.

“Kwa sasa nataka ieleweke kwamba Bw Odinga ni mmoja wa marafiki wetu ambao hata tunaweza kushirikiana naye kisiasa siku zijazo. Tumemkumbatia kama jamii kwa sababu Rais Ruto amemleta ndani ya serikali na tutachapa kazi pamoja na hatimaye muda ukifika, tuongee kuhusu ndoa kwa siku zijazo za miereka ya kisiasa,” akaongeza.

Bw Gachagua amekuwa hasimu mkubwa wa kisiasa wa waziri huyo mkuu wa zamani na alikuwa kati ya wanasiasa waliomtahadharisha Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta dhidi ya kufanya kazi na kiongozi huyo wa ODM.

Kile ambacho kimeunganisha Naibu Rais na Bw Odinga kimtazamo ni wote kuunga mkono ugavi wa mapato kwa kutegemea idadi ya watu wala si ukubwa wa eneo.

Wito huo umemweka Bw Gachagua pabaya na baadhi ya wanasiasa katika kambi ya Kenya Kwanza, wengi wakimwona kama anayepigania tu maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya.

“Tumefunguka macho sasa na nitaongoza harakati za kumpendekeza Bw Odinga kama mshirika wetu wa dhati Mlimani kama ilivyokuwa katika kinyang’anyiro cha 2022 akisaidiana na Bw Kenyatta,” akasema.

Wakati wa mahojiano hayo, Naibu Rais alirejelea kauli yake kuwa alikuwa amemwekea Bw Odinga mtego kwenye ikulu.

Alisema ni Rais Ruto ndiye alimshauri ayatoe matamshi hayo na kwa kweli aliwajibika kwa kuwa kiongozi wa nchi na Bw Odinga walikutana Uganda kwa Rais Yoweri Museveni.

Alifunguka na kusema kuwa hatua ya Bw Odinga kuunga kauli yake kuhusu mgao wa rasilimali ni ishara tosha kuwa waziri huyo mkuu wa zamani anafahamu masuala ya uongozi wa nchi hii.

“”Nilikemewa sana hata na viongozi wenzangu wa Mlima Kenya. Lakini nilishangaa kumsikia Bw Odinga akiniunga mkono hadharani,

“Bibi yangu aliniambia kwamba roho imemfunulia kwamba Bw Odinga ni yule malaika wa nia njema ambaye kumtambua ni lazima kuwe na ufunuo. Ufunuo huo ndio hatujawahi kuwa nao kama watu wa Mlima na ndipo tukamchukia,” akasema.

Sifa hizi kochokocho ambazo Bw Gachagua amemiminia Raila zinakuja wakati ambapo kumekuwa na madai kuwa naibu rais anapanga kuanzisha ndoa ya kisiasa na Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Licha ya kukita sana siasa zake eneo la Mlima Kenya, wakati wa mahojiano hayo, Bw Gachagua alifunguka na kusema yupo tayari pia kuanzisha ushirikiano na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na Kiongozi wa DAP Kenya Eugene Wamalwa.

Kumkumbatia Bw Odinga kuna kuja wakati ambapo washirika wa mbunge huyo wa zamani wa Lang’ata nao wameteuliwa ndani ya serikali kutokana na ukuruba wake na Rais Ruto.

Kando na kutunukiwa mawaziri watano, mwanasheria mkuu mteule Dorcas Oduor pia anatoka Nyanza, ngome ya kisiasa ya Raila.

Pia kuna mabadiliko yanayotarajiwa ya makatibu wanaodumu serikalini ambapo inadaiwa kinara huyo wa upinzani atavuna vinono.

Bw Gachagua mwenyewe amekuwa akilalamika kuwa wandani wake wanahangaishwa na makachero wa Idara ya Upelelezi Nchini (DCI) pamoja na maafisa kutoka Shirika la Kijasusi (NIS).

Kati ya wandani wake aliosema wamekuwa wakifuatiliwa, kuhangaishwa na mawasiliano yao kurekodiwa ni Mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya na mwenzake wa Embakasi ya Kati Benjamin Gathiru maarufu kama Meja Donk.

Wakati wa mahojiano hayo, Naibu Rais alionekana kuwa na tofauti kubwa na bosi wake akisema kuwa hata hakuhusishwa au kushauriwa wakati ambapo katibu mkuu wa chama cha UDA, Bw Cleophas Malala aling’atuliwa mamlakani wiki jana.

gachagua
raila odinga
Uchaguzi 2027

KIONGOZI wa upinzani Raila Odinga kwa mara ya kwanza ameitetea serikali inayoshirikisha wanachama wa upinzani baada ya Wakenya kumkosoa Rais William Ruto kwa kuteua viongozi watano wa ODM katika baraza lake la mawaziri.

Akiongea jana katika eneo bunge la Kibra, Nairobi, Bw Odinga alisema utawala wa Kenya Kwanza ulimwomba usaidie kuleta utulivu nchini kufuatia msururu wa maandamano ya kuupinga uliofanywa na vijana wa Gen Z.

“Walikuwa wamelemewa ndiposa wakavunja baraza la mawaziri. Wakatuomba usaidizi. Na tukakubali kuwapa wataalamu. Sasa mtaona mambo yakibadilika,” Bw Odinga akasema.

Alikuwa akirejelea mawaziri watano wateule ambao juzi walipendekezwa na Rais Ruto kushikilia nyadhifa mbalimbali za uwaziri.

Wao ni pamoja na aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya aliyependekezwa kuwa Waziri wa Ustawi wa Vyama vya Ushirika, aliyekuwa Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho aliyendekezwa kuwa Waziri wa Uchumi wa Majini, Uchumbaji na Masuala ya Majini, Opiyo Wandayi aliyependekezwa kuwa Waziri wa Kawi na Bidhaa za Petroli na John Mbadi aliyependekezwa kuwa Waziri wa Fedha.

Mwingine ni mwanachama wa Kamati ya Kusimamia Uchaguzi katika ODM Beatrice Askul Moe aliyependekezwa kuwa Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda.

Akiwahutubia wafanyabiashara waliathiriwa na mkasa wa moto ulioteketeza mali yao katika Soko la wazi la Toi, Bw Odinga aliamuru ua la saruji ujengwe kulizunguka soko hilo.

“Namwamuru Gavana Sakaja (Johnson) kuanzisha mara moja ujenzi wa ua na soko la kisasa hapa. Serikali inazo pesa za kuanzisha ujenzi huu ili wale ambao wamekuwa wakipania kunyakua ardhi hii waambulie patupu,” Bw Odinga akasema.

Kiongozi huyo wa upinzani alieleza kuwa kwa miongo mitatu iliyopita, amekuwa akipambana na wanyakuzi wa ardhi ambao walitaka kutwa Soko la Toi wakisaidiwa na maafisa fulani wa Wizara ya Ardhi.

“Nipigania wafanyabiashara hawa kwa miaka 30 sasa. Nataka kusema kuwa hawatafaulu kunyakua kipande hiki cha ardhi. Wanyakuzi hao wanataka kuchukua nafasi, kujigawanya kisha wajenge nyumbani. Mara nyingi wao huenda katika Afisi ya Ardhi kuvuruga rekodi.” Bw Odinga akaeleza.

Aliamuru kwamba Sh100 milioni ambazo Bunge la Kaunti ya Nairobi ilitenga kufadhili ujenzi wa vibanda vya kisasa katika Soko la Toi zinapasa kuanza kutumika mara moja.

Bw Odinga alitoa msaada wa Sh1.5 milioni, pesa taslim, kuwasaidia wale walioathirika katika mkasa huo wa moto. Aidha, alitoa mabati 1000 za ujenzi wa vibanda vipya vitakavyotumiwa na wafanyabiashara kabla ya ujenzi wa soko jipya kuanza.

Kwa upande wake, Seneta wa Nairobi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna alitoa Sh250,000 huku Mbunge wa Kibra Peter Orero akatoa vifaa

mawaziri
raila odinga
Rais WilliamRuto

KUNDI la wapiganiaji wa haki za kibinadamu sasa wameelekea kortini kuzuia kuteuliwa tena kwa Profesa Kithure Kindiki na Aden Aduale na pia uteuzi wa Opiyo Wandayi kwenye Baraza la Mawaziri.

Wanachama 12 wa makundi hayo ya haki chini ya Muungano wa Kenya Bora Tuitakayo, wanasema uteuzi wa watatu hao unaenda kinyume na Katiba.

Kuhusu Profesa Kindiki ambaye aliteuliwa tena kama Waziri wa Usalama wa Ndani, wamesema uteuzi huo utavuruga uchunguzi ambao unaendelea dhidi ya maafisa wa usalama walioua raia wakati wa maandamano ya Gen Z.

Isitoshe, wanahoji uteuzi wa Profesa Kindiki utazima uchunguzi dhidi ya wahalifu wanaodaiwa kukodishwa na serikali kuwakabili waandamanaji na pia wahalifu wengine walioingilia maandamano miezi ya Juni na Julai, 2024.

Wakiongozwa na mwanaharakati Cyprian Nyamwamu, wamesema Tume ya Kitaifa Kutetea Haki za Kibinadamu kwenye ripoti yake mnamo Julai 24, 2024 ilisema watu 60 walifariki na wengine 666 bado walikuwa hawajapatikana.

“Ni ukiukaji wa sheria na ukosefu wa utu kwa Profesa Kithure Kindiki kurejeshwa katika wizara ya usalama ilhali kwa kipindi cha miezi 20 alioushikilia wadhifa huo, kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu,” akasema Bw Nyamwamu katika stakabadhi za kesi alizowasilisha.

Pia wanaharakati hao wamesema uteuzi wa Bw Wandayi unaangamiza demokrasia kwa kuwa alikuwa kiongozi wa wachache bungeni.

Hali kadhalika, wanaharakati hao walisema Rais Ruto alikiuka Katiba kwa kuteua Bw Duale, Bi Alice Wahome na Kipchumba Murkomen kama mawaziri mwanzoni mwa utawala wake ilhali wakati huo walikuwa wabunge.

Wanasema chaguzi ndogo ambazo ziliandaliwa katika maeneo ambapo wanasiasa hao walikuwa wakiwakilisha yaligharimu wapigakura pesa ambazo zingeelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Pia walisema uteuzi wa Bw Wandayi utasababisha mlipa ushuru agharimike kwa kuwa uchaguzi mdogo lazima utaandaliwa katika eneobunge alilokuwa akiliwakilisha la Ugunja.

Wanaharakati hao wamesema Profesa Kindiki ametajwa sana na anastahili kujukumika kutokana na visa vya watu kutokomea kwa njia ya kutatanisha, matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji, kujeruhiwa kwa waandamanaji, kutekwa nyara na haki zao kukiukwa.

“Profesa Kindiki anastahili kurejeshwa katika baraza la mawaziri iwapo uchunguzi kuhusu ukiukaji wa haki unaomkabili utatamatika kisha apatikane hana hatia. Ni matumizi mabaya ya mamlaka kwa Rais kuwarejesha Duale na Kindiki katika baraza la mawaziri,” akasema Bw Nyamwamu.

Hasa alimkemea Profesa Kindiki kwa kutoomba msamaha au kujutia ukiukaji mkubwa wa haki za raia wakati ambapo alikuwa akipigwa msasa na kamati teule ya Bunge la Kitaifa.

“Mahakama hii inafaa kutoa amri kuwa Katiba ya Kenya ina mamlaka hata kuliko Rais na kuzima uteuzi wa Profesa Kindiki,” akasema wakili Kibe Mungai ambaye pia anawakilisha wanaharakati hao.

Wanaharakati hao 12 pia wanataka korti iamuru kura ya maamuzi ifanyike hapa nchini kubaini iwapo Rais Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua wanastahili kusalia afisini.

MaandamanoYaGenZ

Wanaharakati

Baraza la Mawaziri
Kithure Kindiki
maafa

All Rights Reserved © Cantona Group Ltd||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment