JIFUNZE KUPITIA KISA HIKI
Mvuvi mmoja alikwenda kuvua samaki na boti yake akaenda mahali kwenye kina kirefu sana ili apate samaki wakubwa wakubwa akafanikiwa kuwapata,wakati anarudi gafla boti yake ikapata hitilafu ya injini akiwa ndani ya maji na boti ikazima,alijitahidi sana kuiwasha bila mafanikio,akangoja msaada kama kuna meli au boti inaweza pita maeneo aliyopo bila mafanikio pia usiku ukafika,bahari ikachafuka kwa upepo na mawimbi makubwa makubwa yakaanza kumpeleka ambako alikua hataki kwenda alijitahidi sana kuokoa maisha yake kwa kuchota maji yaliyo kuwa yanaingia ndani ya boti hiyo mwishowe akajikuta amesogezwa mbali kabisa na alipokuwa anapajua akakosa kabisa tumaini
Kuna habari fulani kwenye biblia ukisoma kitabu cha Marko 4:35 wanafunzi walikuwa wanasafiri na chombo ndani ya maji na Yesu akalala
Mlokole bila nguvu ndani yake hawezi kufanikiwa,Yesu ni injini ndani yetu na sisi ni vyombo ukikosa hiyo nguvu huwezi kwenda upepo utakuja kukugeuza na kukupeleka muelekeo mwingime upepo ni majaribu ambayo mtu anayapata yanamfanya anakuwa bize mpaka ana sahau yuko injini ndani yake,kuna wakati unaweza ukapoa sana kiimani ukafanya nguvu iliyopo ndani yako isiweze kufanya kazi kuna kipindi ulikuwa una uwezo wa kuomba lkn kuna dhoruba imekupiga huna hamu ya kuomba na wala maombi yako hayana nguvu hapo ujue nguvu imepungua kwako,angalia hawa wanafunzi walitembea na Yesu wakamfanya aka lala wakakosa tumaini wakaogopa upepo na mawimbi walisahau wako na awezaye kutuliza hivyo vyote,usimfanye Yesu alale kwako kama Yesu akilala utafanana na mvuvi upepo utakupeleka mbali.Nakuombea ile nguvu ya Yesu iliyopo ndani yako uanze kuitumia kwa kumuita Yesu aamke.
Yesu akiamka atakuponya
Yesu akiamka atakubariki
Yesu akiamka atawapiga adui zako
Yezu akiamka atakemea dhoruba na upepo mkali
CantonaJoseph’s contacts
Facebook https://www.facebook.com/CantonaJoseph/
Instagram https://www.instagram.com/Cantona.Joseph.
Twitter https://twitter.com/@CantonaJoseph
LinkedIn https://www.linkedin.com/in/CantonaJo…
Management Fortune Baraka Entertainments
Website https://CantonaJoseph.Wordpress.Com
Email:fortunebaraka.entertainmentsltd@gmail.com
cantona.online254@gmail.com
Contacts +254748836127
Wewe ni wa maana sana!
All Rights Reserved @2019/FortuneBarakaEntertainments.
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.