Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 27, 2026 16:44 (EAT)


Umoja wa Mataifa unaonya kuwa hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika majimbo ya Kivu Kusini na Kaskazini, inaendelea kuwa mbaya.

Hili limebainishwa na Naibu Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO,Vivian van de Perre wakati wa kikao maalum kwenye Baraza la Usalama Alhamisi usiku, kujadili hali ya usalama Mashariki ya DRC.
Mapigano yameendelea licha ya kuwepo kwa mktaba wa kusitisha vita.
Massad Boulos, mshauri wa rais wa Marekani Donald Trump kuhusu masuala ya Afrika, anaishtumu Rwanda kwa kuendelea kwa vita.
“Tumesikitishwa na machafuko yaliyozuku hivi majuzi yaliyochochewa na Rwanda, hii ni ukiukaji moja kwa moja wa makataa yetu kwenye mkataba wa Washington. Na ndiyo maana Marekani ilisimama na kuchukua hatua mwanzo wa mwezi huu.Tuliweka vikwazo kwa majeshi ya Rwanda na majenerali wao ,wanne. Tutafanya kadri ya uwezo wetu kuhakikisha wanaovuruga Amani wanawajibishwa,leo tunatoa wito wa kuondolewa kwa vikosi vya Rwanda.” Amesema Massad Boulos.
Hata hivyo, Rwanda kupitia balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa Martin Ngoga inakanusha.
“Tukiwa na lengo wazi la kutatua chanzo cha matatizo yanayokabili ukanda, tumejitolea kuendelea kushiriki kikamilifu michakato inayolenga kuleta suluhu endelevu na ya kudumu, bwana rais mzozo wa mashariki mwa DRC haujasababishwa na Rwanda, hofu ya Rwanda imekuwa ni FDLR na wazo la mauaji ya kimbari yanayohusishwa nayo, ni wazo linalosambaa kwa umma sasa.” Amesema Martin Ngoga.
Balozi wa DRC kwenye Umoja wa Mataifa, Zénon Mukongo, anasisitiza kuwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, wameendelea kudhibiti maeneo waliyopaswa kuondoka.
“Waasi wa M23 RDF wanaendelea kuchukua maeneo zaidi na kuweka utawala huku wakitishia hatua zaidi za kijeshi. Matokeo yake ni raia wamewauwa,wakiwemo watoto na wanawake na mamilioni kuwa wakimbizi huku pia ukiukaji wa haki za binadaam ukiendelea kuripotiwa.” Alisema Zenon Mukongo.
Haya yanajiri, wakati huu Umoja wa Mataifa ukionya kuwa watu Milioni 26.6 nchini DRC wanakabiliwa na baa la njaa huku hali ya usalama ikiendelea kuwa mbaya.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.