Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya kuizuru Urusi

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Musalia MudavadiPicha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya Musalia Mudavadi atasafiri na kuelekea Moscow mwezi ujao, kufuatia sakata la Wakenya kulaghaiwa na kujiunga na jeshi la Urusi katika vita vya Ukraine.

Mudavadi amesema kuwa katika ziara yake hiyo, atafuatilia na kuhakikisha kuachiwa kwa Wakenya wanaoshikiliwa kama wafungwa wa kivita nchini Ukraine na kufahamu pia hali ya wale walio mahospitalini.

Waziri huyo amesema zaidi ya Wakenya 30 wamerejeshwa nyumbani kutoka Urusi katika kipindi cha siku miezi miwili iliyopita na mashirika feki ya ajira kufungwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

“Ombi letu kwa serikali ya Urusi ni kuhakikisha Wakenya hawako katika orodha ya wanaotarajiwa kusajiliwa. Tunataka hilo liwe wazi kabisa,” alisema Mudavadi.

Ripoti katika wiki kadhaa zilizopita zinaonesha kuwa Wakenya waliolaghaiwa kwenda Urusi kufanya kazi zenye malipo ya juu, wanafariki dunia katika uwanja wa mapambano na kupata majeraha mabaya.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment