Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Spika wa bunge la Ujerumani Bundestag, Julia KlöcknerPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance
Spika wa bunge la Ujerumani, Bundestag, Julia Klöckner ameishauri Israel dhidi ya kuirejesha hukumu ya kifo.
Klöckner ambaye yuko ziarani nchini Israel, katika mazungumzo yake na Spika wa Knesset Amir Ohana mjini Jerusalem amesema hukumu ya kifo hailingani na kulindwa kwa utu na kwamba taifa halistahili kulipiza kisasi.
“Naelewa ziara yangu Israel kama Rais wa Bundestag kwanza kama ishara ya mshikamano na usuhuba na taifa lenu la Israel. Pili ni kama ishara ya vita vy akupinga chuki dhidi ya Wayahudi na tatu ni dhamira ya mustakabali ambao watu katika eneo hili wanaweza kuishi salama na kwa heshima,” alisema Klöckner.
Wabunge wa Israel wanajadili mswada wenye utata wa kuanzisha tena hukumu ya kifo kwa magaidi.
Mswada huo unaoungwa mkono na serikali ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ulipita hatua ya kwanza mwezi Novemba.
Ili kuwa sheria, mswada huo unastahili kupita hatua nyengine mbili zaidi katika bunge la Israel.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.